Serikali kuendelea kufanya mageuzi ya sera – Dkt. Mwigulu

Serikali kuendelea kufanya mageuzi ya sera – Dkt. Mwigulu

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
532
Reaction score
364
SERIKALI KUENDELEA KUFANYA MAGEUZI YA SERA – DKT. MWIGULU

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kufanya mageuzi ya sera zinazogusa moja kwa moja maslahi na ustawi wa maisha ya wananchi.

Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wa Serikali wanaotoa visingizio, wasiowajibika na wenye hulka ya kufanya kazi kwa mazoea, ujanja ujanja na kutoa taarifa za michakato badala ya majibu yanayotakiwa.

Amesema hayo Bungeni leo (Jumanne, Januari 27, 2026) wakati akitoa hoja ya kujadili hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jijini Dodoma wakati akizindua Bunge la 13 Novemba 14, 2025.

“Tunapozungumzia utendaji Serikalini, msisitizo ni uadilifu na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi waliotuchagua ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za nchi pamoja na kupata huduma wanazostahili.”

Dkt. Mwigulu amesema kuwa hotuba aliyoitoa Rais Dkt. Samia ilitoa mwelekeo na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha pili. “Hotuba ya Mheshimiwa Rais ilitoa maelekezo na kubainisha changamoto pamoja na majukumu yanayotupasa kuyatekeleza kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa maendeleo.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kutekeleza vipaumbele vyote vilivyoainishwa. “Serikali imeainisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji na kupanga mipango kazi ya utekelezaji wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, na tayari utekelezaji wake umeshaanza kutekelezwa kwenye maeneo kadhaa”.
 

Attachments

  • db6b81d196cd44f2870e9c299a55c344.jpg
    db6b81d196cd44f2870e9c299a55c344.jpg
    260 KB · Views: 21
  • 3067eb46b49b4c0b8dbdf84a1acc9dce.jpg
    3067eb46b49b4c0b8dbdf84a1acc9dce.jpg
    251.8 KB · Views: 26
Bunge la majizi na wauaji halina mvuto wala uhalali.
 
TUNATAKA UMILIKI WA BUS ZA ESTER NA TIMU YA SINGIDA UNITED
 
Mwambieni Dar hatuna maji na mwakani kuna afcon.
Mjulisheni maji yako hapo Rufiji tu na gharama ya kuyaleta ni chini ya magari ya mawaziri kombaini
 
Back
Top Bottom