Serikali yajikanyaga yenyewe

Serikali yajikanyaga yenyewe

Weka ushahidi basi manake ninavyofahamu mm siku hizi hakuna matibabu ya bure,ispokua kwa makundi maalum,(wazee wa umri fulani na watoto wa Chini ya Miaka 5) wengine waliobakia wanapata matibabu kwa kuchangia gharama za matibabu kwa mantiki hiyo ukiacha makundi niliyotaja na wale wa chanjo,mtu mwingine anaweza kwenda kutibiwa hospitali tofauti na za Serikali kwa kutumia kulipa cash au bima ya Afya.Hivi sasa bima ya inapatikana kwa waajiriwa na waliojiajiri kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa kila mtanzania kujitahidi kuhakikisha anajiunga na bima ya afya ili awe na Uhuru wa kutibiwa sehemu tofauti na hospitali za umma iwapo kutakua na changamoto za uhaba wa dawa.
mkuu umezungumza vizuri sana na hii iwekwe bayana tu kwa wananchi kuwa wanapaswwa kuchangia kiasi gani kwa kila mwananchi ambaye si mtumishi wa afya na itudumu kwa kipindi gani. na ili wanacnhi waweze kulipa basi serikali iweke namna bora ya kuwalipa fedha zao kwa mazo wanayoyauza na si kuwakopa na kisha kulipa baadae hii haitaingaia akilini.
 
Acha matusi kwakua hakuna unachoweza kubadilisha kwa kutukana,jazba hazitakusaidia kwa lolote,ni wagonjwa wangapi waliokufa kwa kukosa dawa hadi ufikie hatua ya kutokwa na povu jingi hivyo?

Hakuna matusi hapo ndugu. Kama unachosema hakileti maana lakini tuseme hivyo. Huu ni ukumbi wa kuelimishana pia si kupiga tu porojo. Umesimama upande gani? Viongozi wa serikali wawili, mmoja amesema kuna upungu na hakuna upungufu wa dawa na ni wa mpito, na mwingine akasema hakuna upungufu. Wewe umechukua hoja ipi kati ya hizo mbili? maana sisi wengine hapa tunarudia tu kilichosemwa...
 
mkuu umezungumza vizuri sana na hii iwekwe bayana tu kwa wananchi kuwa wanapaswwa kuchangia kiasi gani kwa kila mwananchi ambaye si mtumishi wa afya na itudumu kwa kipindi gani. na ili wanacnhi waweze kulipa basi serikali iweke namna bora ya kuwalipa fedha zao kwa mazo wanayoyauza na si kuwakopa na kisha kulipa baadae hii haitaingaia akilini.
Kuna baadhi ya mazao ya chakula Serikali hununua kwa ajili ya akiba ya taifa ya chakula,kiasi kinachobakia hununuliwa na watu binafsi sasa kwa hiki kipengele cha pili sijui Serikali inahusikaje?
 
Hakuna matusi hapo ndugu. Kama unachosema hakileti maana lakini tuseme hivyo. Huu ni ukumbi wa kuelimishana pia si kupiga tu porojo. Umesimama upande gani? Viongozi wa serikali wawili, mmoja amesema kuna upungu na hakuna upungufu wa dawa na ni wa mpito, na mwingine akasema hakuna upungufu. Wewe umechukua hoja ipi kati ya hizo mbili? maana sisi wengine hapa tunarudia tu kilichosemwa...
Ya Waziri mwenye dhamana
 
FB_IMG_1476349271228.jpg
Wewe unaongea zaidi kwa mhemkoa ndiyo maana unatumia maneno ya kejeli ebu tuambie ni hospitali ipi ulienda ukakosa dawa?
 
Ya Waziri mwenye dhamana

Unafikiri ukisema Waziri mwenye dhamana utathibitisha kwamba kauli ya waziri ndiyo ya kweli zaidi? Makamu wa Rais ni Mamlaka ya juu sana, na hawezi kusema kitu bila kuwa taarifa za hicho anachokisema.
 
Kuna baadhi ya mazao ya chakula Serikali hununua kwa ajili ya akiba ya taifa ya chakula,kiasi kinachobakia hununuliwa na watu binafsi sasa kwa hiki kipengele cha pili sijui Serikali inahusikaje?
Uwe unasoma kwanza kabla kupost hueleweki
 
Heshima kwenu wana JF.
Serikali yajikanyaga yenyewe

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaa tiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuna dawa za kutosha nchini, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi.

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaatiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na ya Samia aliyoitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya wazazi Hospitali ya Mwananyamala.

Samia alisema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi, kwani Serikali inajipanga kuondoa tatizo vifaatiba.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu kuwa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa dawa.

Samia amesema licha ya Serikali kujipanga kukabiliana na tatizo hilo, uongozi wa hospitali hiyo unatakiwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
#My take -hizi ndo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka watapishana sana kauli mwaka huu dawa ni kweli hamna hospital lakini sijui wanaficha nini?
Zile pesa za kununua ndege mngeenda kununua dawa ni aibu sana.
Vigogo wanaruka na kukanyagana........
 
Fast track government
 
Mwisho wa Siasa ni wapi???

Na watendaji nao wanakazi gani kama matamko waliopaswa wayatoe wao yanatolewa na wana Siasa????
 
Back
Top Bottom