Serikali yajikanyaga yenyewe

Serikali yajikanyaga yenyewe

Uongo wowote unakosa baraka za Mungu , ndio maana wamepoteana hawa .

Kupanga ni kuchagua uhaba unaosemekana unatiliwa chumvi tu hali si mbaya kiasi hicho na hilo swala linashughulikiwa kwa karibu,hata kama huna mpango wa kupanda hizo ndege zilizonunuliwa kuna watu wengi tu zitawahudumia kwa hakuna sababu ya msingi ya kujali kuzibeza tu km vile hatuna kitu kingine cha kufanya.Kuna baadhi ya watu wana chuki na Serikali na kazi yao wao ni kuikandia tu kwa kile inachokifanya kwa nia njema.
Utatetea hadi pumba mwaka huu !

Hospital ya rufaa mkoa Wa Kagera hata panadol tunanunua pharmacy za watu. Sasa utasemaje madawa yapo? Au yapochumbani kwako????

[quote uid=89950 name="Emma." post=18015919]Heshima kwenu wana JF.
Serikali yajikanyaga yenyewe

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaa tiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuna dawa za kutosha nchini, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi.

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaatiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na ya Samia aliyoitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya wazazi Hospitali ya Mwananyamala.

Samia alisema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi, kwani Serikali inajipanga kuondoa tatizo vifaatiba.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu kuwa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa dawa.

Samia amesema licha ya Serikali kujipanga kukabiliana na tatizo hilo, uongozi wa hospitali hiyo unatakiwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
#My take -hizi ndo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka watapishana sana kauli mwaka huu dawa ni kweli hamna hospital lakini sijui wanaficha nini?
Zile pesa za kununua ndege mngeenda kununua dawa ni aibu sana.[/QUOTE]
Wewe unaongea zaidi kwa mhemkoa ndiyo maana unatumia maneno ya kejeli ebu tuambie ni hospitali ipi ulienda ukakosa dawa?
Wewe upo wapi ambapo kuna dawa?

Hiv kuna siku hospital zikawa na dawa za kutosha??
Tangu nianze kupata faham nikienda hospital sijawahi kupata dawa zote! Labda siku hiyo niambiwe nikanunue panadol na flagil

Utatambua wangapi kwa style hiyo?
Wewe itetee tu kwa kuwa ni mgeni wa nchi hii usiyejua taarifa zinavyofichwa. Ukitaka wakuambie walikufa wangapi ili ukawafufue? Taarifa hizo kwa awamu ungezipata bjla shida.
Isitoshe, udhibiti huu uwe na maeneo na idara. Siyo hivi unavyotetea wewe! Unaudhi unavyotetea kwa kujipendekeza sijui umealikwa kuzima mwenge?

Bi Ummy anatuma ujumbe kwa bwana mkubwa naye sijui amwelewi alianza kwa kusema kufyatua watoto ni utani ..bwana mkubwa jiongeze basi kidogo

Wewe itetee tu kwa kuwa ni mgeni wa nchi hii usiyejua taarifa zinavyofichwa. Ukitaka wakuambie walikufa wangapi ili ukawafufue? Taarifa hizo kwa awamu ungezipata bjla shida.
Isitoshe, udhibiti huu uwe na maeneo na idara. Siyo hivi unavyotetea wewe! Unaudhi unavyotetea kwa kujipendekeza sijui umealikwa kuzima mwenge?
Hata kama nimealikwa kuzima mwenge lkn mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni hali si mbaya kama watu wanavyojaribu kuonyesha

we nimeshakujua ndo maana kila kitu unaenda kinyume laiti yangekufika ndo ungejua kinachoongelewa ni kweli ama si kwel,bora tu unyamaze maana yalotufika tunataman tukurukie tukung"ate hata pua

Ebu toa scenario moja tu iliyokukuta wewe binafsi ili kusaidia wahusika kuchukua hatua.

Ile U-TURN iliyopigwa inahitaji maelezo kidogo, si kwa unafiki ule. Nimemuita akafanye clearance ya ule uchafu kule at least he/she has to admit
Tuyamalize kwanza haya ya ukosefu wa dawa unaopelekea ndugu zetu kufa kama panzi kila kukicha. Je, wewe unaona ni sahihi serikali kuudanganya umma wa watanzania kwamba kuna dawa TELE huku wananchi wakiendelea kuzikwa kila siku? Huoni hii ni laana ya kujitakia? Je, kulikuwa na ulazima wa kununua ndege zitakazotumiwa na mafisadi peke yao huku wanachi hawana dawa hospitalini?

Heshima kwenu wana JF.
Serikali yajikanyaga yenyewe

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaa tiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuna dawa za kutosha nchini, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi.

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaatiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na ya Samia aliyoitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya wazazi Hospitali ya Mwananyamala.

Samia alisema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi, kwani Serikali inajipanga kuondoa tatizo vifaatiba.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu kuwa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa dawa.

Samia amesema licha ya Serikali kujipanga kukabiliana na tatizo hilo, uongozi wa hospitali hiyo unatakiwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
#My take -hizi ndo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka watapishana sana kauli mwaka huu dawa ni kweli hamna hospital lakini sijui wanaficha nini?
Zile pesa za kununua ndege mngeenda kununua dawa ni aibu sana.
Hivi ni lini serikali hii ya CCM itaacha kuwaua raia wake kwa kufanya maamuzi na usanii wa ovyoovyo?

Wewe unaongea zaidi kwa mhemkoa ndiyo maana unatumia maneno ya kejeli ebu tuambie ni hospitali ipi ulienda ukakosa dawa?
Wewe QUMER usinitafutia ban ya lazima. Sasa hv nimelazwa hospitali moja ya serikali na hapa hakuna hata kidonge kimoja cha panadol...dawa zote tunaenda kununua na huko ndani ya famasi dawa nyingi muhimu hazipatikani. Acha siasa kwenye maisha ya watu wewe maiti. Usinitafutie ban nakuambia.

Umenitukana tayari,umepata shs ngapi? Kama kweli wewe mgonjwa hiyo akili ya kutukana huku JF unaipata wapi?Ebu taka hiyo hospital uliyolazwa na ueleze kwa ufasaha tatizo lako manake matusi hayatusaidii hapa.

Kwani mada kama hizi haziwezi kuunganishwa ili tupate mwendelezo wa mawazo?
Kwani ukichangia kabla ya kuunganushwa uzi wako utapotea pindi ukiunganushwa? Acha unafiki...serikali ya CCM inaua wananchi kimyakimya halafu mnakuja kutukejeli hapa?

Back
Top Bottom