Serikali yajikanyaga yenyewe

Serikali yajikanyaga yenyewe

Hivi nchi hii ni moja kama tunavyoaminishwa au vipo vinchi vingine vidogovidogo ninavyiviona sasa? Juzi kuhusu tukio la walimu tarajali kule mbeya vinchi vilijionyesha dhahiri. Jana na juzi navina tena vinchi vingine. Hali hii inaniaminisha kutokuwepo kwa collectiveness katika uongozi wa nchi.
Wanoitwa viongozi hawana mawasiliano chanya hata kidogo.
Haiwezekani makamu wa rais aseme uongo na waziri wa afya ndio awe mkweli.
Kuna haja ya kuwasiliana kwa viongozi wetu juu ya mambo yenye shida ili ikitokea umealikwa uwe na angalau la kuficha au kuanika kama sio kutetea.
Mama Suluhu, ukweli utakuweka huru. Kama kuna tatizo liweke bayana ili tujue namna ya kujibadilisha. Nikuombe umfukuze kazi huyo dadake Ally chemical wa enzi za Saddam kule Iraq kwa kuudanganya umma na kusababisha vifo vilivyowza kuepukika.
Huu si wakati wa kulialia na kulaumu kila kinachofanywa na Serikali,jiulize kwanza wewe umeifanyia nini Serikali,hili swala la upungufu wa dawa baadhi ya watu wanaliongezea chumvi sana kana kwamba kuna wagonjwa wamekufa kwa kukosa dawa.
 
Mleta mada ana hoja. Ktk kipindi cha Dakika 45 cha ITV Kigwangala sawa na makamu wa Rais, alikiri upungufu wa dawa upo nchini.
 
Wewe unaongea zaidi kwa mhemkoa ndiyo maana unatumia maneno ya kejeli ebu tuambie ni hospitali ipi ulienda ukakosa dawa?
Zahanati ya Matema, shinyanga, hospital ya wilaya kyela ni mwezi wa tatu sasa mpaka chanjo tunanunua maduka binafsi. dawa ambazo ni lazima utazipata hospital ni PANADO. Just come u gona see dis
 
Huu si wakati wa kulialia na kulaumu kila kinachofanywa na Serikali,jiulize kwanza wewe umeifanyia nini Serikali,hili swala la upungufu wa dawa baadhi ya watu wanaliongezea chumvi sana kana kwamba kuna wagonjwa wamekufa kwa kukosa dawa.
Me serikali kikubwa nilicho ifanyia ni kulipa kodi zote ninazostahili, tozo na shuru zinginezo then wao waniletee huduma that's all. Mgahawani nadai risiti, msalani nadai risiti, barabarani kwa traffic nadai risiti kwa muktadha huo nikienda hospital ntadai dawa,matibabu na risiti but budluck enough dawa hakuna na risit cpati.
 
Jiunge na bima ya afya hata kama umelipa Kodi zote haimanishi kua utatibiwa bure.
 
Misunderstanding mkuu na si kwamba nataka nitibiwa bure no tunataka assurance tukifika hospital tupate dawa, ktk hospital za uma kunakitu kinaitwa COST SHARING, sisi masikini tunachangia gharama za uendeshaji na serikali yetu pia inachangia kwa hiyo kwa kua na budget ndogo tunaweza pata huduma mkuu. otherwise gharama zikiwa hivyokama zilivyo ss kwenda kwenye maduka & hospital binafsi tutegemee vifo vingi sana vinavyoweza kuepukika. ipo haja ya serikali kuleta dawa na ukizingatia makusanyo serikali kuu (TRA) ni makubwa na kila mwezi tunavuka lengo. HAPA KAZI TU bila utimamu wa akili na mwili ni ngumu kutekelezeka mkuu.
 
Kwani mada kama hizi haziwezi kuunganishwa ili tupate mwendelezo wa mawazo?
Mbona unapaniki?
Screenshot_2016-10-12-12-44-39.png
 
Lazima tukubali kuwa kuna kupatwa kwa serikali pia kama ilivyokuwa kupatwa kwa jua. Mimi nilidhani sasa tumeahirisha kuugua halafu kipaumbele chetu ni kununua ndege 2 za abiria. Au nyie mnsasemaje ?
 
Huyu mama atumbuliwe tu, hana tofauti na yule WAZIRI WA YA NJE WA IRAQ, kipindi cha Sadam Hussein.

Watu wanashambuliwa, yeye anasema kesho wamarekani kwisha kazi yao..... kumbe wao ndio wanateketea....
 
Ummy uzuri wake ndio wambakiza ila hana kituyule
 
Misunderstanding mkuu na si kwamba nataka nitibiwa bure no tunataka assurance tukifika hospital tupate dawa, ktk hospital za uma kunakitu kinaitwa COST SHARING, sisi masikini tunachangia gharama za uendeshaji na serikali yetu pia inachangia kwa hiyo kwa kua na budget ndogo tunaweza pata huduma mkuu. otherwise gharama zikiwa hivyokama zilivyo ss kwenda kwenye maduka & hospital binafsi tutegemee vifo vingi sana vinavyoweza kuepukika. ipo haja ya serikali kuleta dawa na ukizingatia makusanyo serikali kuu (TRA) ni makubwa na kila mwezi tunavuka lengo. HAPA KAZI TU bila utimamu wa akili na mwili ni ngumu kutekelezeka mkuu.
Bima ya afya kwa sasa ina cover mambo mengi sana,na pia huduma za hospitali binafsi no nzuri zaidi
 
Huu si wakati wa kulialia na kulaumu kila kinachofanywa na Serikali,jiulize kwanza wewe umeifanyia nini Serikali,hili swala la upungufu wa dawa baadhi ya watu wanaliongezea chumvi sana kana kwamba kuna wagonjwa wamekufa kwa kukosa dawa.
mbona unakuwa na upofu wa kufikiri uliopitiliza? Ni nani analia na anamlilia nani? Jipangeni mnaojipa kazi mzisozimudu! Na kwanini mkurupuke kama mnafukuzwa? Huyu anasema hivi baada ya dk moja mwingine anasema kitu kilekile kwa kukanusha. Be collectively na sio hivi halafu unasema hakuna wanaokufa. Una uhakika na hilo?
 
Ngoja tukuone siku utaingia kwenye uongozi utafanya nini,ingekua kuna uhaba wa dawa kiasi inavyosemekana basi tungekua na vifo vya wagonjwa waliokufa kutokana na kukosa dawa lkn hali si mbaya kiasi hicho,siku za nyuma hali ilikua mbaya zaidi na kuna mambo ambayo awamu hii imeyarithi kutoka awamu iliyopita na inajaribu kurekebisha hali lkn watu wengine wanalialia na kulalamika kana kwamba hakuna kinachofanyika.Mh Rais siyo mjinga anajua anachokifanya ila kwakua una Uhuru wa kukosoa wee kosoa tu mpk hapo hamu itakapoisha.
 
Lazima tukubali kuwa kuna kupatwa kwa serikali pia kama ilivyokuwa kupatwa kwa jua. Mimi nilidhani sasa tumeahirisha kuugua halafu kipaumbele chetu ni kununua ndege 2 za abiria. Au nyie mnsasemaje ?
Kupanga ni kuchagua uhaba unaosemekana unatiliwa chumvi tu hali si mbaya kiasi hicho na hilo swala linashughulikiwa kwa karibu,hata kama huna mpango wa kupanda hizo ndege zilizonunuliwa kuna watu wengi tu zitawahudumia kwa hakuna sababu ya msingi ya kujali kuzibeza tu km vile hatuna kitu kingine cha kufanya.Kuna baadhi ya watu wana chuki na Serikali na kazi yao wao ni kuikandia tu kwa kile inachokifanya kwa nia njema.
 
Huyu mama atumbuliwe tu, hana tofauti na yule WAZIRI WA YA NJE WA IRAQ, kipindi cha Sadam Hussein.

Watu wanashambuliwa, yeye anasema kesho wamarekani kwisha kazi yao..... kumbe wao ndio wanateketea....
Utatambua wangapi kwa style hiyo?
 
Back
Top Bottom