Serikali yajikanyaga yenyewe

Serikali yajikanyaga yenyewe

Srikali ya Magufuli inajulikana haina msemo mmoja ni serikali ya hovyo kuwahi kutokea wanaishi kwa propaganda mara uchumi umeanguka Ndulu Mpango kesho wanaenda kukanusha mara Muhimbili inavifaa tiba vyote na Magufuli Mkurugenzi Mseru anawaambia wananchi kulipa kila huduma mara mahindi yasiuzwe nje uuzwe unga Majaliwa Tizeba wananchi wauze mahindi yao, Marafedha za mikopo zipo Ndalichako wazazi wachangie serikali haiwezi kulipa kila kitu Magufuli , nchi ina ombwe la uongozi serikali dhaifu mno
 
Hata kama nimealikwa kuzima mwenge lkn mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni hali si mbaya kama watu wanavyojaribu kuonyesha
hivi hali mbaya unaitafsirije wewe? Bidhaa ikiadimika kwako hakuna shida? Hebu vaa viatu vya wagonjwa au wenye wagonjwa waliokosa dawa uyaone machungu na maumivu yao kisha urudi tena hapa kuutetea uzembe wako na wao. Huenda hutambui maana ya uwepo wa huduma muhimu kwenye hospitali zetu ndio maana unatetea uzembe.
 
hivi hali mbaya unaitafsirije wewe? Bidhaa ikiadimika kwako hakuna shida? Hebu vaa viatu vya wagonjwa au wenye wagonjwa waliokosa dawa uyaone machungu na maumivu yao kisha urudi tena hapa kuutetea uzembe wako na wao. Huenda hutambui maana ya uwepo wa huduma muhimu kwenye hospitali zetu ndio maana unatetea uzembe.
Fafanua
 
Heshima kwenu wana JF.
Serikali yajikanyaga yenyewe

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaa tiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuna dawa za kutosha nchini, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi.

Waziri Ummy amekanusha taarifa zilizokuwa zimeenea kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu na kusisitiza kuwa, zipo nyingi na zinaendelea kuingia nchini. Pia, Waziri huyo alithibitisha kuwapo vifaatiba vya kutosha na kwamba, chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini hivi sasa tayari zimeletwa.

Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na ya Samia aliyoitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya wazazi Hospitali ya Mwananyamala.

Samia alisema ukosefu wa dawa unaojitokeza hivi sasa ni wa muda mfupi, kwani Serikali inajipanga kuondoa tatizo vifaatiba.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu kuwa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa dawa.

Samia amesema licha ya Serikali kujipanga kukabiliana na tatizo hilo, uongozi wa hospitali hiyo unatakiwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato.
#My take -hizi ndo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka watapishana sana kauli mwaka huu dawa ni kweli hamna hospital lakini sijui wanaficha nini?
Zile pesa za kununua ndege mngeenda kununua dawa ni aibu sana.
Hawajatofautiana. Ni mtazamo wako tu.
 
Back
Top Bottom