Serikali yabaini ubadhirifu mabilioni ya fedha za malipo ya korosho. Wakulima wasiolipwa watakiwa kujitokeza na CAG kuikagua bodi ya Korosho

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,150
Waziri wa kilimo mh Hasunga amesema mabilioni ya fedha za korosho yameliwa na wajanja hivyo ameunda tume ya uchunguzi kufuatilia ubadhirifu huo.

Pia mh Hasunga amemtaka CAG kuikagua bodi ya korosho kwani kuna kiasi cha zaidi ya sh bilioni 55 hazijulikani ziliko.

Kadhalika Waziri amewataka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wajitokeze wakiwa na vielelezo vyao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Kumbe hata wanajeshi nao wezi?!

Wao ndio walikusanya korosho kutoka kwa wakulima, ukichukua mzigo kwangu lazima tuandikishane umechukua nini na kiasi gani na nakudai kiasi gani, sasa iweje zipotee ikiwa jeshi lilitoa list lilipoikusanya korosho?!

Kwanini wasilipwe, kwanini aliye kusanya hakulipa papo kwa papo?!

Waliutengeneza wizi halafu wanamtafuta mwizi.
 
Waziri wa kilimo mh Hasunga amesema mabilioni ya fedha za korosho yameliwa na wajanja hivyo ameunda tume ya uchunguzi kufuatilia ubadhirifu huo.

Pia mh Hasunga amemtaka CAG kuikagua bodi ya korosho kwani kuna kiasi cha zaidi ya sh bilioni 55 hazijulikani ziliko.

Kadhalika Waziri amewataka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wajitokeze wakiwa na vielelezo vyao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Fedha zimeliwa na wajanja au wezi mkuu?
 
Hizi ni siasa tena siasa uchwara, malipo yanalipwa kwa njia ya benki. Na utaratibu uulikua kila mkulima analipwa kupitia akaunti yake na serikali ilikua inamuingizia mkulima moja kwa moja bila kupitia chama kikuu au chama cha msingi (Amcos). Sasa hizo fedha zipotee zinapotea kwa njia ipi.

Serikali ilkili adharani tu kwamba haitoweza kumalizia madeni sababu ilipata hasara!.
Korosho ilizoutangazia umma kwamba imenunua kwa tsh 3,300/-wamekuja kuuza 2700 hadi tsh 2000/-. na hadi sasa bado hazijaisha!.

Lakini hizi siasa za kuamisha goli ili kutafuta huruma ya wananchi ni kutuona wakulima wa korosho ni mazumbukuku.
 
Serikali iliyojaa watakatifu imekwiba hela tena za Wakulima? Yaani wafanyakazi wamedhulumiwa nyongeza ya mishahara na wakulima wamedhulumiwa fedha ya mauzo ya mazao yao? Halafu kuna chama kina alama zikiwakilisha Wakulima na Wafanyakazi? What a Joke!!!
Labda CHAMA CHA WAKUNA NAZI TANZANIA.
tapatalk_1570180785087.jpeg
 
hajasema ni kwa msimu upi,watazunguka wee lakini msimu unaosemwa ni wa 2017/2018 lakini msimu wa magufuli wa 2018/2019/hausemwi na huu ndio kuna wakulima wengi wamepata hasara na baadhi kutolipwa
Ni mimi sijaukelewa au? Kawahiyo unamaanisha 2017/18 kilikua cha Mwinyi?
 
Back
Top Bottom