Zitto Kabwe: Tangu mwaka 2015 Serikali imepeleka Mabilioni ya fedha Mwanza ambayo haijulikani yanapokelewa na nani, CAG atueleze!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,138
ACT Wazalendo leo wamefanya uchambuzi wa Ripoti ya CAG.

KC Zitto Kabwe amesema kuanzia mwaka 2015 Serikali imekuwa ikipeleka fedha kwa mabilioni Mkoani Mwanza ambazo hazijulikani ni za nini na huwa zinapokelewa na nani.

Zitto Kabwe amemtaka CAG kutolea maelezo ya kina yalipo mabilioni hayo ya walipakodi huko Mwanza.

Kadhalika Zitto Kabwe ametaka Polisi, TAKUKURU na TISS waongezewe uwezo ili waweze kudhibiti kabla ufisadi na wizi haujatokea kwani hali ni mbaya sana.

Source: ITV habari
 
Zitto wa ajabu sana, anajua mambo mabaya kama hayo lakini haitaki Katiba Mpya hasa ile rasimu ya Warioba, yeye anataka Tume Huru ya uchaguzi ili ajihakikishie kurudi bungeni akatafune posho.

Naiona tofauti ndogo sana kati yake na huyo aliyepeleka hayo mabilioni Mwanza, wote ni wabinafsi, wote wanaweka maslahi yao mbele zaidi ya wengine, wanatofautiana kwenye viwango vya pesa tu.
 
Zitto wa ajabu sana, anajua mambo mabaya kama hayo lakini haitaki Katiba Mpya hasa ile rasimu ya Warioba, yeye anataka Tume Huru ya uchaguzi ajihakikishie kurudi bungeni akatafune posho.

Naiona tofauti ndogo sana kati yake na huyo aliyepeleka hayo mabilioni Mwanza, wote ni wabinafsi, wote wanaweka maslahi yao mbele zaidi ya wengine, wanatofautiana kwenye viwango vya pesa tu.
Zitto ni kichaa kama vichaa wengine
 
Anajua pesa zilikuwa zikipelekwa, halafu hajui zilikuwa zikienda kwa Nani, kwa nini aseme zilikuwa zikipelekwa Mwanza na wakati hajui mpokeaji wa hizo fedha Mwanza? Hivi anafahamu kwamba Mwanza kuna tawi la BoT?

Na Je kama zilikuwa zikipita tuu njia na kwenda Mara au Bukoba?

Kwanini siku hizi uwezo wa Zitto kupambanua mambo umeshuka kiasi hiko?

Ukiwa mtafiti wa habari, angalau ulete zilizokamilika kwa kiasi!

Hii tarifa kama ni ya chama, basi walilishana matango pori, inaonyesha ni jinsi gani ACT walivyo weupe chama chote,
 
Zitto wa ajabu sana, anajua mambo mabaya kama hayo lakini haitaki Katiba Mpya hasa ile rasimu ya Warioba, yeye anataka Tume Huru ya uchaguzi ajihakikishie kurudi bungeni akatafune posho.

Naiona tofauti ndogo sana kati yake na huyo aliyepeleka hayo mabilioni Mwanza, wote ni wabinafsi, wote wanaweka maslahi yao mbele zaidi ya wengine, wanatofautiana kwenye viwango vya pesa tu.
Cc Zitto
 
Hizo pesa kwa mabilioni zinazopelekwa Mwanza haijulikani zinaingia akaunti zipi?
Zitto wa ajabu sana, anajua mambo mabaya kama hayo lakini haitaki Katiba Mpya hasa ile rasimu ya Warioba, yeye anataka Tume Huru ya uchaguzi ajihakikishie kurudi bungeni akatafune posho.

Naiona tofauti ndogo sana kati yake na huyo aliyepeleka hayo mabilioni Mwanza, wote ni wabinafsi, wote wanaweka maslahi yao mbele zaidi ya wengine, wanatofautiana kwenye viwango vya pesa tu.
 
Mwanza wanavimbiwa?😁😁😁
EQyRK.jpeg
 
ACT wazalendo leo wamefanya uchambuxi wa ripoti ya CAG.

KC Zitto Kabwe amesema kuanxia mwaka 2015 serikali imekuwa ikipeleka fedha kwa mabilioni mkoani Mwanza ambazo hazijulikani ni za nini na huwa zinapokelewa na nani.

Zitto Kabwe amemtaka CAG kutolea Maelezo ya kina yalipo mabilioni hayo ya walipakodi huko Mwanza.

Kadhalika Zitto Kabwe ametaka Polisi, Takukuru na Tiss waongezewe uwezo ili waweze kudhibiti kabla ugisadi na wizi haujatokea kwani hali ni mnaya sana.

Source: ITV habari
Siku zote BOT imekuwa ikisafirisha pesa zake kwa njia ya Barabara kuelekea kwenye Tawi lake la BOT-MWANZA.

Huwa sio siri,huwa magari yale na Escort yake huwa iko wazi na wala utaratibu huo sio mpya ni wa miaka mingi.

@Zittokabwela ni mtafuta kick kama kawaida yake tu.

Sio siri kwamba kwa kanda zote za nchi hii.
Kanda ya ziwa ndio hub ya uchangiaji wa Uchumi wa nchi hii.

Kutokana na miradi mikubwa ya kiuchumi iliyoko huko pamoja na maliasili watu na pia Maliasili Madini.

Huko ndio kuna Almasi,Dhahabu,Pamba,
Samaki na pia hifadhi za taifa.

Hivyo mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kuliko porojo za @Zittokabwela.
 
Back
Top Bottom