funluverx
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 480
- 342
Hata salamu sitoi.
Leo nina hasira kupitiliza
Ninaweza kumzaba kibao yeyete ambae naweza kukutana naye barabarani nikihisi tu kuwa kwa namna moja ama nyingine amehusika na 'Utopolo' huu, bila ya kujali yeye ni nani ama ana nini.
Ni hivi; kwenye uchambuzi wa magazeti asubuhi hii ya leo, kupitia CLOUDS FM-Radio. Wanasema kwa kifupi kuwa 'Serikali yenu ya Wanyonge' inao mpango mkakati wa kuzuia matumizi ya kupiga na kupokea 'Simu na Video' kupitia Wavuti yaani mfano. WhatsApp, FB na huduma nyingine za aina hiyo.
Sababu kubwa eti, 'Serikali hiyo ya Wanyonge' inakosa mapato kwakuwa huduma hizo ni za gharama ya chini.
Iwapo hii ni kweli.
Huduma kupiga video na simu kwa wapendwa wetu italazimu kutumia gharama tofauti na 'mabando ya Intanet' ambayo kwa kawaida tunaweka yaani 'vifurushi vya intaneti'.
Kwa maneno mengine, ni kuwa gharama itakuwa mara dufu iwapo utahitaji kutumia huduma hizo.
Nikuulize, je, umewahi kutumia Mtandao kwa kutumia salio lako la kawaida?
Mlioko maeneo yanapopatikana Magazeti tafadhalini tafuteni mjiridhishe kwa Undani maana kilichofanywa na Clouds ni ule wanaita 'udanduzi' wa Magazeti leo tar.10/3.
Itakuwa ni Habari iliyopamba magazeti ya leo, hivyo usiniulize ni gazeti gani.
Jamani, mawasiliano si anasa na hii ni Karne ya 21. Hawa watu hawalijui hili?
Argrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.