Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,421
Reaction score
133,801
Wanabodi,

Wenye access na TBC, angalieni live, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bennard Membe, ametoa msimamo wa Tanzania kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Libya, Col. Muammar Ghadafi.

Waziri Membe, ametoa msimamo huo leo asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa moja kwa moja na TBC-1.

Waziri Membe amesema
  1. Tanzania haijafurahishwa na kifo hicho kwa vile Watanzania hatuna utamaduni wa kufurahia kifo chochote. Na kifo cha umwagaji damu ni kifo kibaya. (Japo Tanzania haijafurahia kifo hicho, ila pia haijalaanio mauaji hayo).
  2. Membe amesema, kwa vile Ghadafi ilikamatwa akiwa hai, huo ni uthibitisho kuwa aliuwawa mikononi mwa waliomkamata. Tanzania ingependa kuona Ghadafi akifikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili kumtendea haki.
  3. Tanzania imeitaka serikali ya mpito ya Libya kudumisha amani na kuanza maandalizi ya kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  4. Pia amesema, Umoja wa Afrika, utatoa tamko lake leo, nalo halitakuwa tofauti na msimamo wa Tanzania, kutounga mkono mauaji ya Ghadafi ila nao utasisitiza kuundwa kwa serikali ya mpito na kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia.
  5. Amesema hizo shamrashamra za kushangilia kifo cha Ghadafi zinazoonekana mitaani Libya ni short lived, kwa vile pamoja na mapungufu ya Ghadafi ya kutoruhusiu demokrasia, wanaompenda pia ni wengi kutokana na maendeleo makubwa aliyoiletea Libya hivyo isitegemewa maadam Ghadafi amekufa sasa ndio amani ya kudumu itapatikana Libya.
Waziri Membe, aliendelea kumsifia Ghadafi kwa michango yake kwa umoja wa Afrika na kueleza jinsi alivyotaka kuunganisha bara la Afrika kuunda United States of Africa ambapo alijenga makao makuu yake mjini Sirte, mahali alipozaliwa.

Membe pia alisifia maendeleo makubwa yaliyopigwa na Libya katika ujenzi wa nyumba za kisasa na miundo mbinu bora kabisa barani Afrika, na kueleza kuwa Tangu mwaka 2006, amekuwa akiwaalika viongozi wa Afrika kila mwaka kupiga kambi huko Sirte. (Naamini ni kula maraha).

My Take.
Kwanza nampongeza Waziri Membe kujitokeza waziwazi kuonyesha Tanzania kama nchi, tunamlilia Ghadafi.
Rafiki ni wakati wa dhiki, Membe alitakiwa hayo aliyoyasema leo kuhusu Ghadafi, angetakiwa ayasema pale Mabeberu na wale vibaraka wao, walipoanza chokochoko Libya.
Ningefurahi kama Membe na Tanzania, tungeonyesha kulaani uwamizi wa demokrasia ya Kiafrika inayoshambuliwa na wakoloni mamboleo na mabeberu wa ulaya wenye uchu na utajiri wa Afrika na kuwaondoa viongozi vikwazo kwa kisingizio cha kulinda demokrasia.
Kauli ya Membe kuwa Marehemu alikuwa mtu mzuri kwa Bara la Afrika, came 'too late' ila hata hivyo Tanzania imefanya uungwana wa kutoa kauli hii kwenye kifo hiki, ili angalau kuituliza 'karma' ya Ghadafi isitushukie Watanzania kwa ukosefu wa fadhila.

Binafsi, sijafurahishwa na kifo cha namna ile cha Ghadafi, vile ambavyo sikufurahishwa na kifo cha Osama, Saddam , Doe, ets. Kwa kifupi sipendi kabisa hata kuona tuu rangi ya damu ya binadamu!.

RIP Ghadafi!.

Pasco
 
Benard Membe leo umeumbuka. Alisema nchi haiwezi kutetwa kwa PICK UP. Libya imetekwa sasa kwa PICK UP. God bless libya

Tatizo la Membe haamini katika nguvu ya umma, anaamini vifaru na mizinga! Historia inatamka wazi "PEOPLE CAN DEFEAT THE STRONG ARMY". Tanzania ina Defence Force haina ARMY, kwa hiyo wananchi tukiamua tunaweza kumtoa fisadi kwa marungu na mishare tu siyo Pick-up tena. Aibu imrudie Mende kwa kutotambua Nguvu ya Umma iliyomkimbiza Quaddafi Tripoli.
 
Benard Membe leo umeumbuka. Kwa dharau kabisa na kuwabeza waasi na balozi wa libya wa hapa nchi, Alisema nchi haiwezi kutetwa kwa PICK UP. Libya imetekwa sasa kwa PICK UP. NGUVU YA UMMA HAIZUIRIWI KWA MIZINGA YANA HATA KAMA UNAJESHI KUBWA. Membe anaamini kutumia mizinga ndio unakuwa mshindi lakni keo walibya wameonyesha haiitaji mamagari makubwa na mizinga kuteka nchi. MEMBE TAMBUA LEO PICK UP ZIMETEKA NCHI.God bless libya.
 
"Rais Mtarajiwa Membe kulikoni Maslahi ya Taifa Kwenye Sakata la Rada?

Kumekuwa na imani isiyo rasmi kuwa waziri wa mambo ya nje kwa kawaida ndiye rais mtarajiwa, hata Mkapa na Kikwete walianzia kwenye wizara hiyo hivyo ukiongezea na fununu za mitaani si dhambi tukisema waziri wa mambo ya nje wa sasa Bernard Membe amelalia mlango wazi wa kuwa binadamu wa tano kukalia kiti cha urais wa Tanzania na imani hata wapambe wake wanampamba hivi.
Tangu kuibuka kwa sakata la rada na jnsi kasi ya Membe katika kulishughulikia tayari malalamiko yameanza kusikika kila pembe ya nchi watu wakihoji juu ya uwezo wa rais huyu mtarajiwa katika kutetea maslahi ya taifa.
Membe haonyeshi hamu ya serikali kuwashughulikia watanzania waliohusika kwenye dili la rada na hata waingereza wanapogoma kulipa hizo fedha yeye anazungumza kisiasa kuwa lazima watulipe lakini ukipima mchoko wa kauli zake unamaizi kuwa ni kama anacheza makida ule mchezo wa kitoto kwa maana hata mimi ningekuwa nadaiwa kisha anayenidai haonyeshi kuwa kweli anataka nimlipe fedha zake basi sitamlipa hivyo ndivyo Membe anavyofanya.
Mimi nilitegemea atumie vizuri nafasi hii kujing'arishia nyota yake ya kwenda Ikulu lakini naona ameanza kupwaya mapema kwa kauli zake za kisiasa, hakuna haja ya kuwabembeleza wezi wala madalali wa Tanzania walioshirikiana na wezi dawa ni kuwashughulikia ipasavyo mpaka wajue kuwa Tanzania si shamba la bibi lakini naona Membe anatuchezea akili labda nimalize kwa kumtaka Membe mara atokezapo mbele ya umma na vyombo vya habari hatutaki tena mchezo wa kitoto bali tunataka tuambiwe ni lini? juma ngapi? na tarehe ngapi? wezi walikwapua jasho letu wataturudishia vinginevyo nitashawishika kuweka kulikoni? kwenye uwezo wa Membe kutetea maslahi ya Taifa.

NOVA KAMBOTA
0717 709618 / +255717 709618
novakambota@gmail.com
Nova Tzdream -"
 
Kwahiyo unasema hata TZ tuteke nchi kwa PICK UP?.Alikataa kuwatambua kwa kuzingatia sheria za kimataifa na si vinginevyo.Kitendo walichofanya waasi wa Libya si cha ubinadamu.Huwezi ukamuua kwa aibu hivyo kiongozi wenu.waarabu si watu waungwana hata kidogo.
 
nadhani ni muda mwafaka kwa wanaafrica wote kwa ujumla wake kusikitika coz 2mepoteza kiongozi mwenye ujasiri wa kusimamia kile anachokiamini ni sahii licha ya mazingira kuwaje. suala la kuuwawa kwa gadaffi c la kufurai hata kidogo kwani kwa kufanya hvyo 2nazika uhuru we2 na kukaribisha ukoloni mamboleo
poleni wote
 
Ni kweli inasikitisha kwa kiongozi shupavu wa Afrika kuuwauwa hivi na watu wake, sasa unazungumziaje hawa raia wa Libya waliojitokeza wengi hivi wakishangilia na bendera mpya ya zamani ya libya?
[
 
Ni kweli inasikitisha kwa kiongozi shupavu wa Afrika kuuwauwa hivi na watu wake, sasa unazungumziaje hawa raia wa Libya waliojitokeza wengi hivi wakishangilia na bendera mpya ya zamani ya libya?
[[/QUOTE Tatizo Gaddafi alijifanya kung'ang'anizi sana. angeachia madaraka mapema haya yote yasingemkuta. masiki Gaddafi Mungu akulaze mahala pema peponi
 
nadhani ni muda mwafaka kwa wanaafrica wote kwa ujumla wake kusikitika coz 2mepoteza kiongozi mwenye ujasiri wa kusimamia kile anachokiamini ni sahii licha ya mazingira kuwaje. suala la kuuwawa kwa gadaffi c la kufurai hata kidogo kwani kwa kufanya hvyo 2nazika uhuru we2 na kukaribisha ukoloni mamboleo
poleni wote

Ukoloni mambo upi ambao haujaingia Tanzania ? Pinda na hekari 800,000 kaweka mkataba .Madini yetu na watu wanavyo uawa na hao unaowaona kwamba hawajafika .Au unaongelea nini mkuu ?Wachina wanapiga hata polisi .Mchina mmoja kufa hata Membe na mke wa rais wanafika kuomba msamaha wakati ni ujambazi wa kawaida .Ukoloni upi kaka unao ongelea wewe ?
 
Benard Membe leo umeumbuka. Kwa dharau kabisa na kuwabeza waasi na balozi wa libya wa hapa nchi, Alisema nchi haiwezi kutetwa kwa PICK UP. Libya imetekwa sasa kwa PICK UP. NGUVU YA UMMA HAIZUIRIWI KWA MIZINGA YANA HATA KAMA UNAJESHI KUBWA. Membe anaamini kutumia mizinga ndio unakuwa mshindi lakni keo walibya wameonyesha haiitaji mamagari makubwa na mizinga kuteka nchi. MEMBE TAMBUA LEO PICK UP ZIMETEKA NCHI.God bless libya.

Mwenye akili timamu huwezi kushabikia kilichotokea Libya. Dharau kwa sovereign state siyo kitu cha kushangiliwa na watu makini na wenye akili timamu kama wanaJF, kama ninavyolazimika kuamini kwa misingi ya falsafa iliyounda jukwaa hili ya 'great thinking'
 
Benard Membe leo umeumbuka. Kwa dharau kabisa na kuwabeza waasi na balozi wa libya wa hapa nchi, Alisema nchi haiwezi kutetwa kwa PICK UP. Libya imetekwa sasa kwa PICK UP. NGUVU YA UMMA HAIZUIRIWI KWA MIZINGA YANA HATA KAMA UNAJESHI KUBWA. Membe anaamini kutumia mizinga ndio unakuwa mshindi lakni keo walibya wameonyesha haiitaji mamagari makubwa na mizinga kuteka nchi. MEMBE TAMBUA LEO PICK UP ZIMETEKA NCHI.God bless libya.

ghadafi alikuwa dikteta mkubwa sana , aliwanyamazisha wapinzani wake kwa gharama yoyote huku akijifanya anaendesha nchi kwa demokrasia, aliwaibia mali wananchi wa libya akaishi maisha ya kifahari kupita maelezo angalia majumba yake yalichukuliwa yalivyokuwa ndio utajua huyu mtu aliwaibia wana libya, na bado alitaka kuridhisha madaraka kwa watoto wake,
kumbuka alipeleka majeshi kumsaidia nduli idi amini kupigana na nyerere mwaka 1979 akimtetea nduli kwa unyama wake
alitaka nigeria igawanywe kusini na kaskazini alijiona yeye ni raisi wa afrika
aliyeua kwa upanga atauwawa kwa upanga malipo ni hapa hapa duniani
sadam na wanawe, osama, ghadafi, hitler.............
 
Back
Top Bottom