Serikali ya Tanzania yakopa Dola Milioni 140 kujenga mradi wa kufua umeme wa Mto Malagarasi

Si Prof. Muongo alisema eti sasa hivi ushamba kuwekeza kwenye umeme wa maji?
 
Binafsi naona gavamenti inajipa mzigo kwa kuwa na miradi mingi, kwanini tusingeongeza nguvu pale stigilaji goji na kulikamilisha kwa ubora mzuri, na tuliambiwa tutakuwa na saplasi ya umeme ambao tutauuza pia.Ndiyo maana miradi yote huwa inaishia hewani tu haikamiliki hata ikikamilika inakuwa chini ya kiwango
 
Bora mama anaweka wazi,

Sio lile jamaa limesimama juu ya gari, linatafuna muhindi wa kuchoma uku likijipiga piga kifuani

"Tunajenga kwa pesa zetu za ndani"

Kumbe limekopa, likibanwa eti "ili Deni Ni stahimilivu"
 
Hii mikopo tunaambiwa wakati wa kukopa tu wakati wa kulipa au hata kupunguza deni hatuambiwi
Kila mwezi ni kama bilioni 600, zinatumika kulipia mikopo hiyo mkuu!!hao TRA, wanapokwambia makusanyo ni trilioni 1.2 kwa mwezi husika jua kuwa bilioni 600, zinatumika kulipia hayo madeni, ni hatarii
 
Barabara zenyewe kuangalia mpaka saivi mashimo tupu Uneza fugia na samaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…