Serikali ya Tanzania yakopa Dola Milioni 140 kujenga mradi wa kufua umeme wa Mto Malagarasi

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani Milioni 140 (Tshs Bilioni 323) kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa ajili ya kugharamia Mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa Mto Malagalasi Mkoani Kigoma.

Mkataba huo wa mkopo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Emanuel Tutuba na Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa AFDB Nnenna Nwabufo.
Si Prof. Muongo alisema eti sasa hivi ushamba kuwekeza kwenye umeme wa maji?
 
Binafsi naona gavamenti inajipa mzigo kwa kuwa na miradi mingi, kwanini tusingeongeza nguvu pale stigilaji goji na kulikamilisha kwa ubora mzuri, na tuliambiwa tutakuwa na saplasi ya umeme ambao tutauuza pia.Ndiyo maana miradi yote huwa inaishia hewani tu haikamiliki hata ikikamilika inakuwa chini ya kiwango
 
Bora mama anaweka wazi,

Sio lile jamaa limesimama juu ya gari, linatafuna muhindi wa kuchoma uku likijipiga piga kifuani

"Tunajenga kwa pesa zetu za ndani"

Kumbe limekopa, likibanwa eti "ili Deni Ni stahimilivu"
 
Hii mikopo tunaambiwa wakati wa kukopa tu wakati wa kulipa au hata kupunguza deni hatuambiwi
Kila mwezi ni kama bilioni 600, zinatumika kulipia mikopo hiyo mkuu!!hao TRA, wanapokwambia makusanyo ni trilioni 1.2 kwa mwezi husika jua kuwa bilioni 600, zinatumika kulipia hayo madeni, ni hatarii
 
Unajua dhambi hiyo? kumsingizia marehemu! labda hujui historia ya marehemu tukukumbushe,mwendazake aliwahi kushusha bei ya kujenga barabara za lami chipping kutoka bilioni 1.2 hadi moja kwa miaka mingi bei ikaendelea kuwa ileile aliokoa shilingi ngapi hadi leo kwa nini asingechukua hongo kama wenzake tukaendelea kupigwa.
Mwendazake aliwashusha waturuki kujenga reli mpaka wakenya wakataka kushikiana bunduki baada ya kupigwa na wachina kwa kujengewa reli SGR isiyotumia umeme kwa bei kubwa kuliko ya kwetu ya umeme lakini kwa bei ndogo kuliko wao, kuhusu upigaji mwendazake mtamuonea.
Barabara zenyewe kuangalia mpaka saivi mashimo tupu Uneza fugia na samaki
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom