Serikali ya Tanzania yakopa Dola Milioni 140 kujenga mradi wa kufua umeme wa Mto Malagarasi

Kwani huu wa Rufiji hautoshi?
Hapo sasa, tunaambiwa mradi wa SG utazalisha 2,115mg, yaani tutakuwa na ziada ya umeme maradufu. Sasa hii mikopo ya umeme mwingine ni ili iweje? Utapeli mwingine bana ni hatari kabisa.
 
Sioni dhambi yoyote kuwa na vyanzo vingi vya umeme kwa nchi kama yetu. Vitatusaidia sana huko mbeleni.

Tatizo letu ni mawazo ya kisiasa kutangalizwa mbele kila wakati. Nchi ya viwanda, yenye kutegemea kuwa na treni za kisasa haiwezi kuzitegemea megawatts 2115 tu.
 
Binafsi naona gavamenti inajipa mzigo kwa kuwa na miradi mingi, kwanini tusingeongeza nguvu pale stigilaji goji na kulikamilisha kwa ubora mzuri, na tuliambiwa tutakuwa na saplasi ya umeme ambao tutauuza pia.Ndiyo maana miradi yote huwa inaishia hewani tu haikamiliki hata ikikamilika inakuwa chini ya kiwango
Sahau kuhusu hilo. Mnadungwa sindano pole pole. Mtakuja kushtuka imeisha ingia yote.
1. Corona chanjo imekubaliwa
2. Wawekezaji wameombwa msamaha na kurudishwa
3. Mahusiano na kenya yameimarishwa
4. Walipa kodi wamepunguziwa makali na kubembelezwa
5. Ulaya wameanza kuupenda uongozi wa sasa

We hushtuki tu
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani Milioni 140 (Tshs Bilioni 323) kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa ajili ya kugharamia Mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa Mto Malagalasi Mkoani Kigoma.

Mkataba huo wa mkopo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Emanuel Tutuba na Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa AFDB Nnenna Nwabufo.
Sawasawà
 
Mahitaji ya umeme nchi nzima bwawa la nyerere kukamilika tunabakiwa na ziada tutauza kwa majirani

Malagarasi ya nini Tena?ikiwa nyerere dam haijakamilika?tukamilishe rufiji ikiwa hautishi tutatafakari muda ukifika hiyo peas ya mikopo........
Tunakuwa na mipango mingi sana ya kuendeleza umeme nchini lakini hatuoni umuhimu wa kuwa na mradi mmoja tu kuweza kufanya hivyo. JNHEP ukikamilika utawezesha kuwa na umeme wa ziada. Sasa fedha hii badala ya kutumika kukamilisha mradi huo, tunaanzisha mradi mpya kabisa.
 
Back
Top Bottom