Abu Dhabi kuikopesha Tanzania Tsh Bilioni 70 kujenga njia ya kusafirisha umeme Benako hadi Kyaka mkoani Kagera

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana Saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Msongo wa kV 220 kutoka Benaco hadi Kyaka na Upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kyaka mkoani Kagera.

Mkataba huo umetiwa saini Makao Makuu ya Mfuko huo Mjini Abu Dhabi na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi huo utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme umbali wa kilometa 167 kutoka Benaco hadi Kyaka na kwa mujibu wa Wizara ya Nishati, hadi mradi huo utakapo kamilika unatarajia kugharimu dola za Marekani milioni 119.4.

“Mkopo huu tuliosaini utachangia nguvu zilizotolewa na Mifuko mingine ukiwemo OPEC Fund for International Development uliotoa dola za Marekani milioni 60, Mfuko wa Maendeleo wa Saudia uliotoa dola za Marekani milioni 13 na Serikali ya Tanzania iliyochangia dola za Marekani milioni 2.4” Alisema Dkt. Nchemba

Imeelezwa kuwa, kukamilika kwa mradi wa umeme wa Benaco-Kyaka, kutaimarisha hali ya upatikanaji umeme katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo kumekuwa na changamoto ya kuwepo kwa umeme pungufu na usio wa uhakika na pia kuufanya Mkoa wa Kagera kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa badala ya kutumia umeme kutoka nchi jirani ya Uganda.

Dkt. Nchemba aliupongeza Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, za kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi ya nishati ambao utakuza uchumi na ajira kwa wakazi wa maeneo ambayo umeme utapitishwa.

“Mpaka sasa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi umewekeza nchini Tanzania kiasi cha dola za Marekani milioni 96.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii na umekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya nchi kwa muda mrefu” aliongeza Dkt. Nchemba

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mohammed Saif Al Suwaidi, amesema kuwa Mfuko wake utaendelea kufadhili miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Tanzania ili nchi ifikie malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kuoitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

“Mradi huu wa kimkati wa kusambaza nishati ya umeme kwa wananchi ni hatua muhimu kwa ajili ya kufikia malengo na matamanio ya wananchi ya kujiletea maendeleo lakini ni kielelezo pia cha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Nchi za falme za Kiarabu ambao wameweka mipango ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa ni mdau mkuu wa maendeleo” Alisema Mhe. Suwaidi

Alisema kuwa Mfuko huo utaendelea kuangalia fursa nyingine za ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana Tanzania ikiwemo sekta ya utalii, kilimo, ujenzi wa makazi ya kisasa kwa ajili ya watumishi katika Serikali ya Mapinduzi-Zanzibar, miundombinu ya barabara, kilimo pamoja na nishati.

Miongoni mwa miradi ambayo Mfuko huo umetoa fedha kwa Tanzania ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Wete-Pemba, barabara ya Kidawe hadi Uvinza (km 77), ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Kagera na mradi wa maji Zanzibar vijijini ambayo imekamilika na hivi sasa wanafadhili ujenzi wa barabara ya Uvinza-Ilunde hadi Malagarasi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 15.

PIX 4.jpg

PIX 5.jpg
 

Attachments

  • PIX 1.jpg
    983.2 KB · Views: 4
Mkataba unasemaje?

Tunawapa nini in exchange?, maana tunajua hakuna free lunch

Usije ukakuta mmewapa concenssions ya rasilimali zetu kibao ili mpate tu hivyo vijisenti vya bilion 70 ambavyo hata sisi tunaweza kuvipata tukibana mianya ya ufisadi na kubana matumizi!

Leteni habari za mchakato na si event!
 
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana Saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha
Ni jambo Jema la maendelea Ili muache kuwachekea Wana Kagera kwamba ni maskini kumbe hata umeme hawana.
 
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana Saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya Ujenzi wa njia ya kusafirisha

Kagera hasa Bukoba waache watumie umeme wa Uganda mana huo umeme uko stable sana haukatiki hovyo kama huu wa gridi,naona sasa bkb wanaenda kuhangaika na mgao mana huko mgao huwa wanausikia tu.
 
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa KV 220 kutoka Benaco hadi Kyaka na upanuzi wa

Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba akitiliana saini mkataba wa mkopo huo na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu

Mkataba huo umetiwa saini makao makuu ya mfuko huo Mjini Abu Dhabi na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi.

Waziri Nchemba amesema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme umbali wa kilometa 167 kutoka Benaco hadi Kyaka na kwa mujibu wa Wizara ya Nishati mradi huo utakapokamilika unatarajia kugharimu dola za Marekani milioni 119.4.

"Mkopo huu tuliosaini utachangia nguvu zilizotolewa na mifuko mingine ukiwemo OPEC Fund for International Development uliotoa dola za Marekani milioni 60, Mfuko wa Maendeleo wa Saudia uliotoa dola za Marekani milioni 13 na serikali ya Tanzania iliyochangia dola za Marekani milioni 2.4," amesema Dkt. Nchemba

Imeelezwa kuwa, kukamilika kwa mradi wa umeme wa Benaco-Kyaka, kutaimarisha hali ya upatikanaji umeme katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo kumekuwa na changamoto ya kuwepo kwa umeme pungufu na usio wa uhakika na pia kuufanya mkoa wa Kagera kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa badala ya kutumia umeme kutoka nchi jirani ya Uganda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mohammed Saif Al Suwaidi, amesema kuwa mfuko wake utaendelea kufadhili miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Tanzania ili nchi ifikie malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kuoitia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

Miongoni mwa miradi ambayo mfuko huo umetoa fedha kwa Tanzania ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Wete-Pemba, barabara ya Kidawe hadi Uvinza (km 77), ujenzi wa kiwanda cha Sukari Kagera na mradi wa maji Zanzibar vijijini ambayo imekamilika na hivi sasa wanafadhili ujenzi wa barabara ya Uvinza-Ilunde hadi Malagarasi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 15.

Chanzo: East Africa Radio
 
20230809_175227.jpg

Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu zimetiliana saini mkataba wa mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 30 sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa KV 220.

Kutoka Benaco hadi Kyaka na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kyaka mkoani Kagera.

Mkataba huo umetiwa saini makao makuu ya mfuko huo Mjini Abu Dhabi na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Serikali, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi.

#EastAfricaTV
 
Halafu juzi tu wameandaa sherehe ya kujitukuza wanafanya vizuri, wamefutiwa madeni sasa hivi wanaweza kopa wenyewe.

Ndio tuelewe hiyo annual statement yao imejaa upuuzi mtupu; hakuna la maana wanalofanya pamoja na kufutiwa madeni yote bado kupewa mkopo bila ya government guarantee hesabu zao na matumizi yao ni ya ovyo ovyo tu.

Mambo kama haya ndio busara huyo mama 2025 inatakiwa tumrudishe Kizimkazi au tumjengee hekalu lake analostahili kisheria kwa kushika nafasi ya uraisi popote.

Binafsi napendekeza ajengewe hekalu lake kando ya ziwa Victoria si amekubali kuwa chief wa sukuma tribe huko ndio kunamfaa kwenda kupumzikia, ila hapo Ikulu nchi ataipeleka pabaya sana akiongezewa muda ‘mark my words’ na hawa vijana wasio na uwezo anaowapa sensitive posts.
 
Mwigulu anamiliki timu ya SINGIDA BIG STARS lazima akili yake ipagawe maana wachezaji na timu yote inahitaji Kula Sasa akili za kutatua matatizo ni kukopa Kwa Kasi ili afanyie mambo yake.Usisahau hata kassimu majaliwa anamiliki timu ya namungo Kwa hiyo hawa wapo tayari kuuzwa ,kupapaswa,na Jambo lolote lakini timu zao ,zifanyekazi
 
Back
Top Bottom