Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

unaelewa maana ya wakimbizi na wahamiaji haramu? nyie ndio watoto wa haramu wa Kinyaruanda mlioko hapa nchini,ondokeni rudini kwenu tumeisha beba mizigo yenu vya kutosha= n
The question is why now?
Tatizo la wakimbizi wa Kinyarwanda limekuwepo kwa muda mrefu. Mbona
hatua zimeanza kuchukuliwa baada ya majibishano ya PK na JK halafu
unataka tuamini hakuna uhusiano wowote ?
 
Viscom; Habari haijapotoshwa mkuu, ni dhahiri Mhe.Rais Kikwete ameamuru wahamiaji haramu haswa wa Rwanda na Burundi wafungashe virago.Je, tuamini kwamba Rwanda hakuna Watanzania japo 100 wanaoishi kinyume cha sheria? Basi kama wapo, hata kama ni wachache serikali ya Rwanda imesema haitawafukuza.
 
Tatizo watu mnaleta emotions kwenye masuala yahusuyo sheria.
Hakuna tatizo lolote kwa nchi moja kuwa na raia wa nchi nyingine wanaoishi kihalali (hii ni sheria dunia nzima).
Kinachofanywa na serikali ya Tanzania ni kumalizia kuwarejesha makwao wale wakimbizi waliokuwa wamepitiliza muda wao wa kukaa hapa, na bado wapo (hii haikubaliki na sheria!)........hakuna kitu kibaya kilichofanywa na Tanzania.


Je kunawamalawi, wazambia,wakenya, wahindi, waarabu nk wangapi wanaoishi kinyume na sheria ya uhamiaji? ni hatu zipi zimechukuliwa dhidi yao napia wasomali kibao wanafilisi Tembo wetu?

Nini mtazamo wako katika hili? Jadili ukirejerea kufurushwa kwa wanyarwanda.
 
Yuko sahihi. Hana sababu kuwafukuza watanzania walioingia Rwanda kwa sababu hawakuingia na silaha za kivita, hawafanyi ujambazi, hawauwi wanyarwanda, hawaendi kupora ardhi, hawaendi kuhonga wachaguliwe kuwa viongozi wa vijiji
 
JokaKuu; Hakuna anayetaka wahamiaji haramu waachwe ni vema tukaelewana, kinachoangaliwa mbele ya jumuiya ya kimataifa ni mahusiano baina ya nchi husika. Kwanza, mazingira yaliyopo sasa ni tatanishi ndiyo maana nje ya Rwanda hatujasikia malalamiko ya wahamiaji haramu wa Kenya,Uganda wala Wahindi wanaojificha masokoni na kwenye magorofa yao. Tanzania ni mlezi wa Rwanda kwa namna ya misaada ya ubinadamu na mali ukiachana na kusuluhisha migogoro kupitia mahakama ya iliyokuwa Arusha.Je, mtoto uliyemlea akikutukana utapambana nae kwa nguvu au hekima? Lakini kitu kingine ni mwelekeo wa kuwafukuza wahamiaji haramu, binafsi najua wahamiaji haramu wa kihindi wanavyoishi, Wazungu wanaofanya kazi kinyume cha sheria japokuwa walikuja kwa mgongo wa utalii, bado kwenye viwanda vya samaki lake zone wamejaa wengi tu.Je, ni kweli serikali imejizatiti kuwapukutisha wote? Vipi wasomali wanaoletwa na kushushwa Kibaha kabla ya kutafutiwa kazi?
Makala Jr,

..Hii nchi imekuwa kama haina serikali.

..I am not talking about wahamiaji haramu peke yao.

..watu wanaingia na kutoka Tanzania kama ni choo cha "site."

..kuna mpaka lidege la kijeshi lilitua KIA na kuondoka na wanyama na nyara za serikali.

..nchi imekuwa ni uchochoro wa kusafirisha madawa ya kulevya.

..uwindaji haramu umeshamiri, na tembo, faru, etc wanauwawa hovyo.

..it is about time vyombo vya ulinzi na usalama vianze ku-enforce the laws.

..badala ya kuikatisha tamaa serikali, nawaomba msisitize wayamulike maeneo mengine pia.

cc: Samaritan
 
Last edited by a moderator:
The difference is the same. Why now? And why Ngara? Umesikia wahamiaji haramu wanafukuzwa Arusha au Mtwara?

najua majibu unayo mkuu ila basi tu. Kwanza ulisoma ile ripoti ya Mtikila. Pili itv walishakuwa na kipindi maalum juu ya kadhia ya hawa wanyarwanda. Tatu kila leo kuna utekaji na uporaji huko Ngara vikihusisha silaha nzito nzito. Kaza roho ndio hii ya Kagame na I will hit you! Kwingineko mipakani mbona hatujasikia haya mambo? Hatua kama hii isingechukuliwa yangejirudia ya Amini
 
Viscom; Habari haijapotoshwa mkuu, ni dhahiri Mhe.Rais Kikwete ameamuru wahamiaji haramu haswa wa Rwanda na Burundi wafungashe virago.Je, tuamini kwamba Rwanda hakuna Watanzania japo 100 wanaoishi kinyume cha sheria? Basi kama wapo, hata kama ni wachache serikali ya Rwanda imesema haitawafukuza.

Mkuu
Hapo anapodili na wanyarwanda akiacha wachina, warabu, wahindi nk kibao napata shida sana kuelewa kikwete analenga

nini kama siyo bifu lake na kagame nini. Ni udhaifu kwake kuhindwa kupambana na kagame anakwenda fukuza wanyonge!!!
 
Watanzania waliopo Rwanda siyo illegal immigrant. Ni wasomi waliobobea na wanafundisha kwenye vyuo vikuu rwanda. Wanyarwanda waliopo Tanzania wengine ni malaya wauza miili yao dodoma wakati wa kipindi cha bunge.
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana tunawatetea watu wanaovunja sheria eti tunataka wasamehewe.

Jk alipotangaza kuwasamehe mafisadi wa EPA tulimlaum sana,
Alipotangaza kuwa anamajina ya wauza unga tukamlazimisha kutaja ,ameshindwa kuwataja tunamlaum mpaka na kumwita ni dhaifu.

Huko nyuma tumelaumu kweli kuwa serikali imeshindwa kulinda mipaka hadi wahamiaji wanaishi na kuhatarisha maisha ya Raia.

Leo serikali imeamua kuchukua hatua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi tunailaimu kwa kufanya kitu tulichokipigia kelele siku nyingi.

Ndio maana Jk huwa anasema ni upepo tu utapita sababu anajua akili zetu zinafanya kazi kwa matukio na sio kumbukumbu.!
 
Tanzania is a 'melting pot' of east africa bwana; where all ethics are found and they live amicably; its the only place in east africa where other ethinicities can marry another without any problem.

The world melting point kwa sasa ni USA; u can find all sorts of rubbish co-exist!!

Tatizo la Tanzania ni moja tu, siasa za midebwedo za ccm, ccm ndo tatizo; watz inabidi kufanya juu chini tuwezekuwa ns siasa zitakazotupatia viongozi bora.
 
Je kunawamalawi, wazambia,wakenya, wahindi, waarabu nk wangapi wanaoishi kinyume na sheria ya uhamiaji? ni hatu zipi zimechukuliwa dhidi yao napia wasomali kibao wanafilisi Tembo wetu?

Nini mtazamo wako katika hili? Jadili ukirejerea kufurushwa kwa wanyarwanda.

Wazungu wanasema "two wrongs don't make right"
Ikiwa unajisifia kuwa wewe ni mwizi na kudai "mbona fulani na fulani ni wezi pia?!?, seuze mimi jamani?"..ni tatizo.
Suala ni yeyote aliye nchini kinyume cha sheria ataondolewa...nadhani hili hasa ndilo lilikuwa tamko la mkuu.
 
waafrika tuna laana na siku zote laana hii hudhihirika kwa viongozi kwani hukosa hekima busara na maarifa katka kutamka na kutenda. kagame ni mfano wa hili.
.......aka!!, mi sina laana japokuwa ni Mwafrika.
 
Sasa JokaKuu tunamtazamo sawa, tunatamani na ni nia yetu kuona serikali yetu ina nia ya dhati ya kutafuta NJIA bora na za KUDUMU kpambana na hizi changamoto.

Utatuzi wa mambo usiendeshwe kwa hisia au utashi wa manufaa ya watu wachache, nadhani raisi wetu ana washayri wake, na vilevile ni imani yangu kwamba raisi ni msikivu kusililiza ushauri. Kama washauri wetu ndio wamemshauri aina hii ya kushughulikia wahamiaji haramu kwa hali ilivyo sasa, safari bado ndefu sana na ndio maana ufumbuzi wa mambo mengi huwa haudumu kama sio kushindwa kabisa.

Kama kasi hii itaendelea kupambana na matatizo mengine yanayolikabili taifa, itakua ni ahueni ila ziwe systematic na sustainable. Tuachane na huu ni upepo tu utapita....

Hatuikatishi tamaa mkuu, tunataka iende kwenye njia sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Je kunawamalawi, wazambia,wakenya, wahindi, waarabu nk wangapi wanaoishi kinyume na sheria ya uhamiaji? ni hatu zipi zimechukuliwa dhidi yao napia wasomali kibao wanafilisi Tembo wetu?

Nini mtazamo wako katika hili? Jadili ukirejerea kufurushwa kwa wanyarwanda.


.......Hao Wasomali unamaanisha Kinana, Bashe na Aden Rage? Subiri wale wanaolipwa buku saba saba watakuja kukujibu.
 
Majuro mjukuu, wamekumbuka shuka kumekucha. Imewabidi kutumia lugha ya kupoza, ingawa mwishoni wamesiliba kuwa watawapinga FDRL na wanaowaunga mkono kwa nguvu zote. Nadhani wamemaanisha J.K

Too late, no retreat!
Yeleyale PK alikuwa anatikisa kibiriti aona kama kimejaa,leo ndio wameamua kutumia lugha iliyopoa yaani Membe ebu mjibu huyu mama ukazie kuwa tutaendelea kuwatimua wanyarwanda wahamiaji haramu popote tutakapo wakuta,na unafanyaje mazungumzo yanahusu wahamiaji haramu??? walipoiingia tulikutana tukafanya mazungumzo??hapo ni timua timua tu wakagombee wilaya yao sijui watafanyaje na mifugo mingi namna hiyo???
 
kweleakwelea; Mimi nakupinga ukisema hakuna haja ya majadiliano kuhusu wahamiaji haramu na utaratibu wa kuwarejesha makwao labda hii iwe Tanzania tu. Marekani ni moja kati ya mataifa ambayo wahamiaji haramu haswa kutoka Mexico na hata Afrika wamekuwa sehemu ya mipango,uratibu na mahusiano ya kiraia baina ya Marekani na jumuiya ya kimataifa.Na mara kadhaa Mijadala imeendeshwa kuhusu namna ya kuwapatia uraia au kudhibiti kasi ya ongezeko la wahamiaji haramu. Tofauti yetu na wao ni moja tu yaani umakini mipakani. Wahamiaji haramu si mbuzi ni watu na wanaweza kuingia kwasababu ya kukimbia njaa,vita,magonjwa au kusukumwa na fursa ya biashara na ajira kama wafanyavyo Wahindi,Wasomali na Wachina.Hoja inayokuja ni je, tuna utaratibu mzuri wa kuwatambua wahamiaji haramu maana tetesi zasema wengine ni madiwani tena kupitia CCM ukiachana na sakata la Kinana. Tumejipangaje?
 
Last edited by a moderator:
Yuko sahihi. Hana sababu kuwafukuza watanzania walioingia Rwanda kwa sababu hawakuingia na silaha za kivita, hawafanyi ujambazi, hawauwi wanyarwanda, hawaendi kupora ardhi, hawaendi kuhonga wachaguliwe kuwa viongozi wa vijiji

Kuna watanzania nje kibao wanaishi bila bila vibali na ni majambazi wengine ndio hao wanakamatwa na unga huko
 
Mkuu
siafiki maelezo yako.

Watanzania ni watu wa ajabu sana tunawatetea watu wanaovunja sheria eti tunataka wasamehewe.

Maamuzi yasiyozingatia usawa ni haramu, kwanini iwe kwa wanyarwanda tu na siyo kwa wasomali, wachina, waarabu, wakenya nk. Kama angefanya kwa usawa bila kulenga kundi flani, yesi lakini hapa nadhani ni aibu na udhaifu mkubwa.

Jk alipotangaza kuwasamehe mafisadi wa EPA tulimlaum sana,

Mpaka sasa bado analaumiwa, amechukuwa hatuagani? nakwanini kama nikiongozi jasiri anafukuza wanyonge asiwakamate hao wezi wa mabilioni yetu? sielewi mkuu unalenga nini kwenye hii posti yako.

Alipotangaza kuwa anamajina ya wauza unga tukamlazimisha kutaja ,ameshindwa kuwataja tunamlaum mpaka na kumwita ni dhaifu.

bado ataendela kuwa dhaifu, huoni jinsi Tanzania inavyodhalilika kama moja ya njia kuu za kufanya biashara ya madawa ya kulevya?

Huko nyuma tumelaumu kweli kuwa serikali imeshindwa kulinda mipaka hadi wahamiaji wanaishi na kuhatarisha maisha ya Raia.

Kwahiyo kwa kuwafukuza wanyarwanda na kuwaacha wasomali, warabu na wahindi mipaka na raslimali zetu zipo salama?

Leo serikali imeamua kuchukua hatua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi tunailaimu kwa kufanya kitu tulichokipigia kelele siku nyingi.

Imechukua hatuagani mpaka tuipongeze?

-Wezi wa EPA wako wapi?

-Wezi wa twiga nk ndani ya ndege wako wapi

-Wasafirisha unga na madawa ya kulevya wapo wapi? nk

Ndio maana Jk huwa anasema ni upepo tu utapita sababu anajua akili zetu zinafanya kazi kwa matukio na sio kumbukumbu.

Anasema hivo kwasababu ya udhaifu wake maana hana uwezo wa kukabiliana na mambo makubwa wala hana ujasili wakukamata wezi wakubwa, wafanyabiashara wa dawa za kulevya, wanaotuibia meno ya tembo nk.

Kwahili nawalaumu watanzania mnashindwa kufahamu udhaifu na uzembe wa kikwete katika mambo ya

msingi. Tumebaki watu wa kuishi kwa matumaini na propaganda inatuabisha sana watanzania kimataifa.
 
By artorius
Mimi nahisi kama Rais Kikwete ametumia emotions zaidi katika hili swala,ugomvi wake na Kagame usiwatese wanyarwanda,hao wahamiaji haramu hawakuja baada ya yeye kukwaruzana na Kagame

Ni kweli hatutetei watu kukaa kinyume cha sheria nchini kwetu, lakini ukizingatia hali ya mahusiano kati ya Rwanda na Tanzania ilivyo sasa hivi, utekelezaji wa huu uamuzi huenda ukatafsiriwa na kuchukuliwa kwa muonekano tofauti. Hoja ya kuishirikisha Rwanda kwenye kuwaondoa raia wa nchi yao ingekua na tija zaidi.
Hivi walivokua wanaingia hiyo serikali ya rwanda iliwasiliana na Serikali ya Tanzania? Nyie hao watutsi hawamjui tabia zao. Kwanza kimama si ndio kilianza kumwambia Mh Rais Kikwete maneno ya kashfa? Warudi kwao...kwnn wanganganie nchi ambayo si yao?
 
Waziri huyo anatudanganya tu Watz, kwani huko kwao Rwanda kuna mtanzania anaeishi huko bila kibali? mnafiki huyo, nani aliyewaambia kuwa wanafukuzwa kwa wale wenye vibali nani aliyewafukuza?wakati wanaingia nchini na maefu ya mifugo waliwasiliana na nani?sasa kwa nini wakati wa kuondoka watake wajulishwe kama nani? kwani tunawabembeleza ili iweje kwetu? wao wanayo ardhi ya kuchungia maelfu ya mifugo hao, hana shukrani kabisa.Hta kwa hao waliozaliwa TZ, lakini si wanajua kikwao?jamani mtu kwao warudi., Rais Kikwete tafadhali wala usirudishe moyo wako nyuma kuhusiana na watu makatili hawa.
 
Back
Top Bottom