Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania. Akizungumzia sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k (DW Kiswahili.)
mbona ghafla wamekuwa wapole kulikoni , hii kauli hata mimi inanipa faraja lakini siyo ile ya kagame '''' eti kuna wakati kikwete hatavuka'' wapi?
 
Nilisema cku zote wenye kauli za upole ni wakali kwenye vitendo!!!
 
Huyu waziri she utters non sense! Tanzania haijawafukuza wanyarwanda wanaoishi TZ kwa taratibu ila inawafukuza wanyarwanda ambao wamevamia maeneo yetu kinyume na kujimilikisha..Anasema waTz hawatafukuzwa Rwanda kwan wamevamia na hawana vibali? km wapo wapewe siku 3 waondoke Rwanda! JK usirudi nyuma hakikisha wanyarwanda na wengine wote wanaoishi bila vibali waondoke mara moja asitake tumuonee huruma ili waendelee kuzaliana na baadae waombe uraia...

Rubbish!! Nenda nje uone wabongo wanaoishi bila vibali, South Africa kuna maelfu ya bongo wazamiaji na wengi ndio wahalifu wnauza madawa na wezi. Hata siku moha sikuwahi kusikia serikali ya madiba inapoteza muda kuwasaka wabongo waliozamia. Tuache roho mbaya hii mipaka iliwekwa na wazungu, waafrika wote ni ndugu.
 
Wanapaswa kuelewa kuwa wanaofukuzwa ni wale HARAMU na siyo kinyume chake, wanyaru wanaoishi kihalali hawafukuzwi! Kama kuna Watz wanaoishi Rwanda kiharamu basi wafukuzwe tu ila siyo kawaida ya Watz kufanya hivyo, kwamba waishi nchi za wenzetu hasa hizi jirani bila vibali?[/QUOT]

Mkuu genekai,
Ni sawa, Wahamiaji Haramu wanapaswa Kufukuzwa, Lakini kwanini imekuwa katika Kipindi iki???????????????????

Mkuu Bramo nakubaliana na wewe!

Siungi mkono wahamiaji haramu kuishi nchini lakini mbona waliachwa miaka yote?! Serikali ilikuwa haijui au walikuwa wanaogopa kuchukua hatua wakati uhusiano na Kagame haujaharibika?

Hii "timing" ya kuwatimua wakati JK na PK wako kwenye uhasama inaacha maswali.
 
Last edited by a moderator:
Upotoshwaji wa habari nao ni chanzo cha migogoro mingi mno Duniani,Rais Kikwete hajawafukuza Wanyarwanda na hana nia hiyo ila ni "wahamiaji haramu" wa nchi za Rwanda na Burundi ndiyo waliopewa muda wa wiki mbili kuuza mali zao na kurudi kwao.Tujiulize maana ya wahamiaji haramu na madhara yao ndiyo tutoe hoja zetu,
Rais hajakurupuka na ninamuunga mkono
 
The difference is the same. Why now? And why Ngara? Umesikia wahamiaji haramu wanafukuzwa Arusha au Mtwara?

one has to start somewhere--and why not ngara! any reason why not ngara first?
 
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania. Akizungumzia sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k (DW Kiswahili.)

Janja ya nyani hiyo. Kama kuna Watanzania wapo Rwanda kwa njia ambazo si halali, wafukuzwe tu. Watu wa Rwanda wanaotakiwa kuondoka wameingia Tanzania kinyume cha sheria. Raia wa Rwanda ambaye yupo Tz kihalali hahusiki na zoezi la sasa.

Kama wao wanaondoa waTanzania huko kwao, hilo shauri lao. Msimamo wa Tanzania ubaki kama ulivyo na hili zoezi liwe endelevu kabisa. Ng'ombe wa Rwanda, kuchunga Tanzania, tumekuwa shamba la bibi. Kama kuna maeneo mazuri ya malisho huko, kwa nini ndugu zetu wasukukma na wamasaai wasiende huko na mifugo yao?
 
Mkuu kumbuka kwamba suala la hawa wakimbizi kuwepo sio la leo, na ni dhahiri linafahamika na serikali yetu, ushauri na uamuzi huu kuchukuliwa kwa hali ilivyo sasa ndio tatizo langu.

Ni kweli Kagame ameongea vibaya na hakuonyesha ustaarabu kama ulivyotafri wewe, ikumbukwe kwamba Banda nae alishatishia kuingia vitani na Tanzania na bado usuluhisho unafanywa.

Kama Kagame ameongea vibaya. Kikwete hawezi tafuta suluhu hata kama ni kwa kushirikisha watu kutoka nje? Na kama hawezi kutatua kwa njia ya maelewano, inakuaje aone ni rahisi Kagame kuongea na waasi kama yeye hawezi kusuluhisha hii hali na Kagame?

..umeshadai kwamba tatizo la wahamiaji haramu ni la muda mrefu, sasa ulitaka lishughulikiwe lini? mimi nadhani lishughulikiwe sasa bila kuchelewa zaidi.

..hivi kwanini wa-Tz wanaoishi mipakani waishi kwa hofu ya kuvamiwa na majambazi? imefika mahali mabasi ya abiria inabidi yasindikizwe na askari polisi lakini hiyo haitoshi kwasababu ya silaha nzito zinatumika ktk uhalifu huku Kagera, na Kigoma. sasa wewe ulitaka hali hii ya wasiwasi, na wananchi kuishi as if hakuna serikali, iendelee mpaka lini??

..Binafsi sioni haja ya JK kutafuta suluhu na Kagame. Kama umemsikiliza vizuri JK ktk hotuba yake ya mwisho wa mwezi july, basi utaona hakuna kilichobadilika kwa upande wake, kwa msingi huo hakuna haja ya usuluhishi.

..It is time hao wahamiaji haramu warudi kwao Singapore..oops I meant Rwanda.

cc Jasusi, Nguruvi3,
 
Last edited by a moderator:
Ni Upumbavu kama Serikali ya Nchi X, inawafukuza Raia wahamiaji wa Kutoka Nchini Y , eti Kisa Rais wa Nchi Y amemtukana Rais wa Nchi X.

Mkuu, nadhani hili gari ulilolidandia hujui liendako, hivi unajua 7bu za kufukuzwa kwa wahamiaji haramu? Km hujui uliza mkuu!!!! 4 ur information ugomvi wa PK na Baba riz1 hauna uhusiano na kufukuzwa kwa hawa wahamiaji haramu!!!!!
 
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania. (DW Kiswahili.)

Kama Wanyarwanda wangekuwa wanathamini ushirikiano wa Afrika Mashariki kama Waziri anavyosema, mbona wametutenga kwenye vikao walivyokaa pamoja na Kenya na Uganda?

Maji yamewafika shingoni wanaanza kujikanyaga!
 
Kwa hili waziri wa Rwanda na serikali yake kwa vyovyote vile wanahekima pia wanaheshimu uwepo wa binadamu wengine.

Kikwete hata iwaje ni dhaifu kweli kweli:-

Ameshindwa kupambana na Kagame ananyanyasa raia wasio na kosa lolote eti wahamiaji haramu

-Mbeya, songea, kigoma. mara, geita, mwanza na mtwara tuna wageni wangapi na wanavibali kweli?

-Je Malawi, Zambaia, Kenya, Uganda, kongo nk kunawatanzania wangapi huko na je wako kihalali wote? au nao wafukuzwe?

Ukweli na historia imejiandika ikithibitisha kwamba Rwanda sio adui wa watanzania na wala sio tishio kwa amani yetu

Tishio la amani ya watanzania ni kiongowetu dhaifu Kikwete
ambaye hana hekima japo busara tu ya kawaida ambayo waziri wa Rwanda ameionesha.

Mchawi wa amani ya East Africa ni kikwete kwa sababu binafsi za kujinasibisha na kuutaka umaarufu kimataifa asioustahili.
 
Nilijua kwa ujinga wa CCM watapigwa bao sana km CDM wanavyowapiga bao.Hii ni wazi Rwanda wanaonekana wanajali watu kuliko CCM ambayo hata bongo inaua raia kwa maslahi ya kisiasa.
 
Mkuu kumbuka kwamba suala la hawa wakimbizi kuwepo sio la leo, na ni dhahiri linafahamika na serikali yetu, ushauri na uamuzi huu kuchukuliwa kwa hali ilivyo sasa ndio tatizo langu.

Ni kweli Kagame ameongea vibaya na hakuonyesha ustaarabu kama ulivyotafri wewe, ikumbukwe kwamba Banda nae alishatishia kuingia vitani na Tanzania na bado usuluhisho unafanywa.

Kama Kagame ameongea vibaya. Kikwete hawezi tafuta suluhu hata kama ni kwa kushirikisha watu kutoka nje? Na kama hawezi kutatua kwa njia ya maelewano, inakuaje aone ni rahisi Kagame kuongea na waasi kama yeye hawezi kusuluhisha hii hali na Kagame?

Ndugu yangu hata mimi hilo ndio linanishangaza kila siku.Mtu anayehubiri maelewano na Wauaji kwa njia ya Mazungumzo lakini yeye mwenyewe anaogopa kuzungumza na waliopishana kauli tumweleweje?
 
Watanzania kwa double standard hatujambo ni juzi tu mlikuwa mnalalamika hapa kwamba wahamiaji haramu wamezidi huko Kagera leo wanarudishwa kwao mnaanza kuona Kikwete kakosea!!!

Kama wanataka kuishi hapa nchini wafate taratibu,na kama kuna watz wanaishi huko bila vibali warudishe kongoro zao nyumbani au wafate taratibu za huko,period!
 
Kama Wanyarwanda wangekuwa wanathamini ushirikiano wa Afrika Mashariki kama Waziri anavyosema, mbona wametutenga kwenye vikao walivyokaa pamoja na Kenya na Uganda?

Maji yamewafika shingoni wanaanza kujikanyaga!


Ukijiona unatengwa na wengi fahamu wewe ndiyo tatizo


Malawi kelele mchana na usiku, wakati wote hatuna uhusiano mzuri

Rwanda balaa hatuna uhusiano mzuri

Kenya hatuna uhusiano mzuri

Uganda hatuna uhusiano mzuri

Jiulize kwanini wote hawatutaki? ukipata jibu rejea hapa jukwaani utueleze.
 
Watanzania kwa double standard hatujambo ni juzi tu mlikuwa mnalalamika hapa kwamba wahamiaji haramu wamezidi huko Kagera leo wanarudishwa kwao mnaanza kuona Kikwete kakosea!!!

Kama wanataka kuishi hapa nchini wafate taratibu,na kama kuna watz wanaishi huko bila vibali warudishe kongoro zao nyumbani au wafate taratibu za huko,period!


Kama ndivyo mbona hatuyaoni haya kutendeka katika mipaka ya kenya, zambia na malawi? unafikiri ni kwanini?
 
JokaKuu; Hakuna anayetaka wahamiaji haramu waachwe ni vema tukaelewana, kinachoangaliwa mbele ya jumuiya ya kimataifa ni mahusiano baina ya nchi husika. Kwanza, mazingira yaliyopo sasa ni tatanishi ndiyo maana nje ya Rwanda hatujasikia malalamiko ya wahamiaji haramu wa Kenya,Uganda wala Wahindi wanaojificha masokoni na kwenye magorofa yao. Tanzania ni mlezi wa Rwanda kwa namna ya misaada ya ubinadamu na mali ukiachana na kusuluhisha migogoro kupitia mahakama ya iliyokuwa Arusha.Je, mtoto uliyemlea akikutukana utapambana nae kwa nguvu au hekima? Lakini kitu kingine ni mwelekeo wa kuwafukuza wahamiaji haramu, binafsi najua wahamiaji haramu wa kihindi wanavyoishi, Wazungu wanaofanya kazi kinyume cha sheria japokuwa walikuja kwa mgongo wa utalii, bado kwenye viwanda vya samaki lake zone wamejaa wengi tu.Je, ni kweli serikali imejizatiti kuwapukutisha wote? Vipi wasomali wanaoletwa na kushushwa Kibaha kabla ya kutafutiwa kazi?
 
Last edited by a moderator:
..umeshadai kwamba tatizo la wahamiaji haramu ni la muda mrefu, sasa ulitaka lishughulikiwe lini? mimi nadhani lishughulikiwe sasa bila kuchelewa zaidi.

Hata mimi napenda na nataka lishughulikiwe sasa hivi japo tumechelewa, tunapopishana mimi na wewe mkuu ni jinsi linavyoshughulikiwa.

..hivi kwanini wa-Tz wanaoishi mipakani waishi kwa hofu ya kuvamiwa na majambazi? imefika mahali mabasi ya abiria inabidi yasindikizwe na askari polisi lakini hiyo haitoshi kwasababu ya silaha nzito zinatumika ktk uhalifu huku Kagera, na Kigoma. sasa wewe ulitaka hali hii ya wasiwasi, na wananchi kuishi as if hakuna serikali, iendelee mpaka lini??

Kama hawa wanaowaua watu kwa bodaboda, kumwagia watu tindikali, kuibia watu wote ni wahamiaji haramu, kazi ipo. Na Zanzibar nako wamemwagia watalii tindikali na serikali ipo tu! Suala la uhalifu ni lingine na linahitaji kushughulikiwa ki vyake la sivyo tutafukuza wahamiaji haramu wote na bado uhalifu utaendelea kushamiri

..Binafsi sioni haja ya JK kutafuta suluhu na Kagame. Kama umemsikiliza vizuri JK ktk hotuba yake ya mwisho wa mwezi july, basi utaona hakuna kilichobadilika kwa upande wake, kwa msingi huo hakuna haja ya usuluhishi.

Uko sahihi kuwa na huo mtazamo inategemea hili suala limekuathiri kiasi gani, lakini ikumbukwe kwamba tunaongelea nchi na wananchi wake, kama Kikwete asingekua raisi unadhani nani angejali kama kuna haja ya kutafuta suluhu au la!

..It is time hao wahamiaji haramu warudi kwao Singapore..oops I meant Rwanda.

cc Jasusi, Nguruvi3,

Hata mimi nasema warudi ila kwa utaratibu
 
Rubbish!! Nenda nje uone wabongo wanaoishi bila vibali, South Africa kuna maelfu ya bongo wazamiaji na wengi ndio wahalifu wnauza madawa na wezi. Hata siku moha sikuwahi kusikia serikali ya madiba inapoteza muda kuwasaka wabongo waliozamia. Tuache roho mbaya hii mipaka iliwekwa na wazungu, waafrika wote ni ndugu.

Tanzania hatujawahi kuwa na Roho ya namna hii.Siku zote Tanzania imekuwa ni Nchi Kimbilio la Wanyonge na Wanaoonewa.Hii Roho iliyotuvamia sijui imetoka wapi.
 
Nadhani wewe na wenzio ndo mtaonekana wajinga mwisho wa siku lakini si watanzania wote. Kikwete na serikali yetu hatufukuzi Wanyarwanda wanaoishi kihalali Tanzania kama mjomba wako anavyoishi Rwanda. Wanafukuzwa wahamiaji haramu tu..... Nakushauri kama mjomba wako anaishi Rwanda kiharamu mtake arudi nyumbani haraka.

Tafadhali naomba uelewe maana ya kinachoongelewa kabla ya kuweka ushabiki mbele hasa kwa watu wasomi kama wewe.
Nategemea unayajua matatizo yanayowakumba ndugu zetu wa Kagera, Kigoma na Geita. Kuwa Mzalendo basi
Nimemsikiliza Vizuri sana WASHA TUZIDI POINT MOJA AMBAYO WATANZANIA WENGI HAWATATAMBUA mwisho wa siku tutaonekana sisi ndo wajinga.

Hata mimi uncle wangu doctor huko Rwanda anasema hukuna tatizo wanaendelea na kazi kama kawaida.
 
Back
Top Bottom