Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Ametumia hekima maana mafahari wawili wakigombana ziumiazo nyika. Hapa muathirika mkubwa wa huu mgogoro ni mwananchi wa chini.
 
WAKUU ITAFAHAMIKA TUU MUDA UKIFIKA NANI ANAFANYA KWA AJILI YA NCHI YAKE NA NANI ANAFANYA AWAFURAHISHE WALIOMTUMA.

Hivi hawa wahamiaji wameonekana kipindi hiki tu??

Hivi huku kusini hakuna wahamiaji??

Hivi Tanzania tumepeleka jeshi Kongo kwa maslahi ya nani maanake kabila, kagame, mu7 kuna vitu wanatafuta?
 
Hili zoezi lilitakiwa liwe limefanyika muda mrefu sana, bado kuna wakenya wengi, waganda wengi sana, wahindi ndo wako mamilioni... hii operations isiishie kanda ya ziwa pekee bali ifanyike Tanzania nzima ....Tanzania kwa watanzania...mgeni lazima afuate taratibu zote zinazohitajika ....
 
Hiyo ni adhabu tosha kwa Kikwete na wapambe wake. Watajiona wao ni wakosaji na wana visasi kwa wasio na hatia

wewe ni -------- namba moja duniani,hivi unaona raha jinsi ndugu zetu wanavoteswa na wahamiaji haramu(majambazi)
 
Ni kweli hatutetei watu kukaa kinyume cha sheria nchini kwetu, lakini ukizingatia hali ya mahusiano kati ya Rwanda na Tanzania ilivyo sasa hivi, utekelezaji wa huu uamuzi huenda ukatafsiriwa na kuchukuliwa kwa muonekano tofauti. Hoja ya kuishirikisha Rwanda kwenye kuwaondoa raia wa nchi yao ingekua na tija zaidi.



..sasa serikali ya Rwanda itashirikishwa vipi wakati Raisi Kagame anamtukana Raisi wetu??

..Zaidi, Raisi Kagame amenukuliwa akisema kuwa atamdhuru Raisi Kikwete.

..I dont think we need to worry jinsi Rwanda watakavyotafsiri uamuzi wetu.

..It is up to Rwanda kutafsiri uamuzi huo vyovyote vile watakavyoamua. JK aliwapa ushauri mzuri wao wakautafsiri ndivyo-sivyo na kuanza kurusha matusi, na kutishia kumdhuru.

cc Jasusi, Samaritan, Makala Jr
 
Last edited by a moderator:
Wanyarwanda tunao wengi sana ndani ya serikali yetu, wengine wako mpaka Ikulu.
 
Tatizo mnaolopoka kugusu kuwafukuza wanyarwanda na kushangilia ni watz wa kisalawem lindi,moro au dom ila c wa mbeya kutwambia eti tunafukuza waamiaji haramu tutakushangaa maana hadi hapa sasa nipo malawi na sina kibali na tupo watanzania wengi tu huku na wamalawi wamejazana apo kwetu wilaya za mpakani na hawajui vibali ninini,. Tunaacha kupambana na maadui wetu wa3 tunaanza pambana na majirani wasio na ubaya kwetu

mkuu ndomyana usitake tuvunje sheria za nchi kisa tu wewe unaishi malawi bila kibali,acha ujinga wewe..
 
Last edited by a moderator:
wewe ni -------- namba moja duniani,hivi unaona raha jinsi ndugu zetu wanavoteswa na wahamiaji haramu(majambazi)

Akili imekutuma hapo utapunguza majambazi kikubwa ni kutafuta njia sahihi za kudili na majambazi. Wakiondoka hao wataingia ambao ni watanzania sehemu yenye mali haitaachwa kikubwa itafutwe njia mahususi ya kudili hapo.
 
Nimemsikiliza Vizuri sana WASHA TUZIDI POINT MOJA AMBAYO WATANZANIA WENGI HAWATATAMBUA mwisho wa siku tutaonekana sisi ndo wajinga.

Hata mimi uncle wangu doctor huko Rwanda anasema hukuna tatizo wanaendelea na kazi kama kawaida.
Huyo uncle wako naamini yuko kihalali huko.vile vile naamini na hapa TZ kuna wanyarwanda wailingia kihalali na hawajasumbuliwa kabisa.waliofukuzwa hapa ni wahamiaji haramu na hili halichagui wanyarwanda,warundi,wacongo au waganda ili mradi awe mhamiaji haramu.kwa hili ninaiunga mkono serikali japo nina dukuduku nayo.
 
kwanini iwe kwa wanyarwanda 2 kwani hakuna wengine wanaoishi tz kinyume cha sheria nchi kibao wapo humu hawaafuata sheria je hao hawajaona hili swala lipo kisiasa zaidi so tusipende kuunga mkono bila kufikiri rais angetangaza kwa yeyote anaeishi tz bila kibali bila kutaja nchi hapo tungejua kweli lakini kwa kuitaja rwanda 2 kuna warakini
 
Heshima mbele wakuu,

Hivi tunaweza kujiuliza ni kwa nini kila siku mabasi ya abiria (yawe yanakwenda au yanatoka) maeneo ya Kigoma, Bukoba, Ngara, Biharamulo na Karagwe na yale yaendayo nchi za Burundi, Rwanda na DRC...huwa lazima yapewe eskoti ya askari 2 wenye silaha kwa kila basi!

Mabasi yatokayo Dar kwenda Kigoma/Bukoba na nchi jirani, huwa yakifika eneo la msalabani (jirani ya Runzewe) ni LAZIMA yapewe eskoti ya askari wenye silaha.

JK aliuliza katika ziara yake mkoani Kagera kuwa, iwaje raia wanasafiri ndani ya nchi yao, kwamba hawawezi kusafiri kwa uhuru pasipo vyombo vya usafiri kupewa eskoti ya askari. Kwamba, hakuna usalama katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.

Hali iliyopo huku magharibi mwa Tanzania ni tofauti na Tarime, Namanga, Tunduma na maeneo mengine ya mipaka ya nchi yetu.

Kwa yeyote aliyethubutu kushuhudia uharamia na matukio ya mipaka ya magharibi mwa nchi yetu, naimani angemshukuru JK kwa aliyojionea.

Uharamia katika ardhi ndio kabisaa usiseme, uporaji ndio balaa. Na pia askari wetu huwaua sana maharamia hao na huwa HAITANGAZWI.

Zikumbukwe operesheni zote za misituni za makamanda wa polisi wa Kagera walizozifanya miaka ya karibuni, yote ni kupunguza uharamia.

Binafsi kwa niliyoyashuhudia, naiunga kauli ya JK.
 
artorius; Hiyo siyo sinema mkuu kwani hapo maisha ya watu yanahusika, nimemsikiliza Mtanzania aliyeko Rwanda anasema wanaishi vema na Wanyarwanda na kufanya nao biashara bila kubaguana na wanawapenda sana Watanzania kwani wanawaona ni watu wema.Je, mapendekezo ya Rais wa Rwanda Gen.Paul Kagame kukutana na Rais wa Tanzania Mhe.Dr.Kikwete hayana mashiko kwa ustawi wa nchi mbili na watu wake?

Swala la uhamiaji haramu ni janga kwa usalama wa taifa kwani hata hao waliopo ruanda kama wanaishi kisanii wanaingamiza Rwanda haswa ukizingati nchi yoyote huendesha mambo yake kwa budget inayozingatia idadi ya watu wake ktk kutoa huduma.
 
Akili imekutuma hapo utapunguza majambazi kikubwa ni kutafuta njia sahihi za kudili na majambazi. Wakiondoka hao wataingia ambao ni watanzania sehemu yenye mali haitaachwa kikubwa itafutwe njia mahususi ya kudili hapo.

sijakuelewa,UNACHOTAKA WAHAMIAJI HARAMU WAENDELEE KUBAKI NCHINI AU.?

NA JE HAUJUI KUWA NI RAHISI KU-DEAL NA MAJAMBAZI AMBAO NI RAIA WA TANZANIA KULIKO HAO WA NCHI JIRANI.?
 
..sasa serikali ya Rwanda itashirikishwa vipi wakati Raisi Kagame anamtukana Raisi wetu??

..Zaidi, Raisi Kagame amenukuliwa akisema kuwa atamdhuru Raisi Kikwete.

..I dont think we need to worry jinsi Rwanda watakavyotafsiri uamuzi wetu.

..It is up to Rwanda kutafsiri uamuzi huo vyovyote vile watakavyoamua. JK aliwapa ushauri mzuri wao wakautafsiri ndivyo-sivyo na kuanza kurusha matusi, na kutishia kumdhuru.

cc Jasusi, Samaritan, Makala Jr

Mkuu kumbuka kwamba suala la hawa wakimbizi kuwepo sio la leo, na ni dhahiri linafahamika na serikali yetu, ushauri na uamuzi huu kuchukuliwa kwa hali ilivyo sasa ndio tatizo langu.

Ni kweli Kagame ameongea vibaya na hakuonyesha ustaarabu kama ulivyotafri wewe, ikumbukwe kwamba Banda nae alishatishia kuingia vitani na Tanzania na bado usuluhisho unafanywa.

Kama Kagame ameongea vibaya. Kikwete hawezi tafuta suluhu hata kama ni kwa kushirikisha watu kutoka nje? Na kama hawezi kutatua kwa njia ya maelewano, inakuaje aone ni rahisi Kagame kuongea na waasi kama yeye hawezi kusuluhisha hii hali na Kagame?
 
Kuna namna nyingi ya kuomba radhi-Lakini hiyo haitoshi-Huyo "dada yao" hana ADABU
 
Mkawaida mbona kiswahili chako ni kama unaasili ya unakokutetea?
 
sijakuelewa,UNACHOTAKA WAHAMIAJI HARAMU WAENDELEE KUBAKI NCHINI AU.?

NA JE HAUJUI KUWA NI RAHISI KU-DEAL NA MAJAMBAZI AMBAO NI RAIA WA TANZANIA KULIKO HAO WA NCHI JIRANI.?

Kwamba hao wamewazidi Uwezo askari wetu au??
 
Back
Top Bottom