Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

Serikali ya Rwanda imeapa kutowafukuza Watanzania!

artorius; Hiyo siyo sinema mkuu kwani hapo maisha ya watu yanahusika, nimemsikiliza Mtanzania aliyeko Rwanda anasema wanaishi vema na Wanyarwanda na kufanya nao biashara bila kubaguana na wanawapenda sana Watanzania kwani wanawaona ni watu wema.Je, mapendekezo ya Rais wa Rwanda Gen.Paul Kagame kukutana na Rais wa Tanzania Mhe.Dr.Kikwete hayana mashiko kwa ustawi wa nchi mbili na watu wake?
Mimi nahisi kama Rais Kikwete ametumia emotions zaidi katika hili swala,ugomvi wake na Kagame usiwatese wanyarwanda,hao wahamiaji haramu hawakuja baada ya yeye kukwaruzana na Kagame
 
Last edited by a moderator:
Sikumbuki kama jk aliitaja Rwanda kama nchi, bali aliwataja wahamiaji haramu bila kujali na Warwanda,Warundi au wa nchi yoyote ile ambae anaishi nchini kinyume na sheria.

jiwe limerushwa gizani, liliempata tumesikia sauti yake.!
 
Hiyo ni adhabu tosha kwa Kikwete na wapambe wake. Watajiona wao ni wakosaji na wana visasi kwa wasio na hatia
 
Mimi nahisi kama Rais Kikwete ametumia emotions zaidi katika hili swala,ugomvi wake na Kagame usiwatese wanyarwanda,hao wahamiaji haramu hawakuja baada ya yeye kukwaruzana na Kagame

kwa hiyo mkuu ushauri wako ni upi kwa Serikali dhidi ya wahamiaji haramu.?
 
artorius; Hiyo siyo sinema mkuu kwani hapo maisha ya watu yanahusika, nimemsikiliza Mtanzania aliyeko Rwanda anasema wanaishi vema na Wanyarwanda na kufanya nao biashara bila kubaguana na wanawapenda sana Watanzania kwani wanawaona ni watu wema.Je, mapendekezo ya Rais wa Rwanda Gen.Paul Kagame kukutana na Rais wa Tanzania Mhe.Dr.Kikwete hayana mashiko kwa ustawi wa nchi mbili na watu wake?
Ni siku nyingi sana nilikuwa na pendekezo hili, https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/499266-kikwete-zungumza-na-kagame.html, japo watu wengi walinipinga. Lakini ukweli ni kwamba hakuna namna yoyote nzuri ya kumaliza tofauti zilizopo katika nchi hizi mbili bila ya Kikwete na Kagame kuamua kukaa pamoja na kuombana msamaha.
 
Sikumbuki kama jk aliitaja Rwanda kama nchi, bali aliwataja wahamiaji haramu bila kujali na Warwanda,Warundi au wa nchi yoyote ile ambae anaishi nchini kinyume na sheria.

jiwe limerushwa gizani, liliempata tumesikia sauti yake.!
Utetezi wa enzi za mawe unaleta hizi zama za technology?
 
kiapo chenu ni kazi bure....ila wanyarwanda haramu sisi tunawafukuza
 
Somoche; Majina yao utata mtupu
 
Last edited by a moderator:
waafrika tuna laana na siku zote laana hii hudhihirika kwa viongozi kwani hukosa hekima busara na maarifa katka kutamka na kutenda. kagame ni mfano wa hili.
Hapo ulipoandika Kagame ungebadilisha uweke jina la Kikwete. Mwenye kukosa hekima anajulikana.
 
Mimi nahisi kama Rais Kikwete ametumia emotions zaidi katika hili swala,ugomvi wake na Kagame usiwatese wanyarwanda,hao wahamiaji haramu hawakuja baada ya yeye kukwaruzana na Kagame

Ni kweli hatutetei watu kukaa kinyume cha sheria nchini kwetu, lakini ukizingatia hali ya mahusiano kati ya Rwanda na Tanzania ilivyo sasa hivi, utekelezaji wa huu uamuzi huenda ukatafsiriwa na kuchukuliwa kwa muonekano tofauti. Hoja ya kuishirikisha Rwanda kwenye kuwaondoa raia wa nchi yao ingekua na tija zaidi.
 
Waondoke tu si wahamiaji haramu?! Hawajafukuzwa waliozingatia sheria!
 
Kwani wanaofukuzwa si ni wahamiaji haramu mkuu?, wale walioingia nvhini na kujipa hdahi ya uraia wa Tanzania bila kufuata taratibu......

Anachokifanya huyo Waziri wa Rwanda ni upotoshaji na kujikosha tu ambako hakuna msingi wowote maana kama ni Wanyarwanda wanaoishi kihalali nchini wapo wengi tu na hawajafukuzwa,wanaendelea na shughuli zao kama kawaida....

Hao anaosema hawatawabughudhi ni wale wanaoishi kihalali nchini Rwanda.......

Hata Rwanda kungekuwa na watanzania wanaoishi isivyo halali(wahamiaji haramu) wangepewa hadhi ya PI na kuamuriwa kuondoka kurudi nchini kama sisi tulivyowataka wahamiaji haramu wa Kinyarwanda waondoke na kurudi kwao....
 
Tatizo mnaolopoka kugusu kuwafukuza wanyarwanda na kushangilia ni watz wa kisalawem lindi,moro au dom ila c wa mbeya kutwambia eti tunafukuza waamiaji haramu tutakushangaa maana hadi hapa sasa nipo malawi na sina kibali na tupo watanzania wengi tu huku na wamalawi wamejazana apo kwetu wilaya za mpakani na hawajui vibali ninini,. Tunaacha kupambana na maadui wetu wa3 tunaanza pambana na majirani wasio na ubaya kwetu
 
Kikwete amesema raia wanaoishi kinyume cha sheria waondoke. Hii kwa nchi nyingi tu inafanyika na si ajabu. Mi nashauri pia kwa Rwanda kama kuna mtanzania anaishi kinyume na sheria pia afukuzwe na arudi Tanzania!
 
hapa ni kufukuza wageni wote hata waganda hila kwa waganda wa kiziba ni ngumu mno kwani sura zao kama za watz
 
Kikubwa wafuate taratibu za kuingia nchini siyo kuingia kihuni kama walivyofanya sikioni wanacholalamikia kwetu,wanatakiwa kutambua makosa yao na wajisahihishe.
 
artorius; Hiyo siyo sinema mkuu kwani hapo maisha ya watu yanahusika, nimemsikiliza Mtanzania aliyeko Rwanda anasema wanaishi vema na Wanyarwanda na kufanya nao biashara bila kubaguana na wanawapenda sana Watanzania kwani wanawaona ni watu wema.Je, mapendekezo ya Rais wa Rwanda Gen.Paul Kagame kukutana na Rais wa Tanzania Mhe.Dr.Kikwete hayana mashiko kwa ustawi wa nchi mbili na watu wake?

Watanzania pia wameipokea ile kauli ya rais tofauti maana wengi wao wanaishi mbali na mipaka hivyo hata mahusiano waliyonayo watu wa mipakani hawajui kwani hata kwa upande wetu kuna watu nchi jirani wanaishi vizuri tu bila shida na kuna utaratibu mzuri unaotumika ku-solve matatizo ya hawa watu, tatizo alipotoa ile kauli wanakuja watu wengine kama wakuu wa mikoa na kutoa kauli zingine ambazo zina hatarisha mpaka ndoa za watu. Ukienda maeneo ya Tarime, Serengeti, Kagunga kule Kigoma, Ngara na maeneo ya mipaka mingine kuna utaratibu wao wa ujirani mwema baina ya vijiji vyote vya mipakani na nchi jirani maana serikali zetu zote hazina uwezo wa kuweka department ya uhamiaji kila sehemu.
 
Back
Top Bottom