Nieleze hali ya kiusalama wa raia na mali zao katika mipaka yetu na Zambia,Malawi,Kenya na Msumbiji halafu na mimi nitakueleza hali ya kiusalama mpakani mwa rwanda na burundi. Think outside the box mkuu siyo unaongea tu kama umekatwa kichwa.
Mkuu kama ni hali ya usalama
1. Taifa lolote lazima lijenge himaya bora na salama kwa vizazi vijavyo.
Je usalama wa vizazi vyetu haupo mipakani na katika viwanja vya ndege? Unauhakikagani na ubora wa maisha ya vizazi vinavyokuja kama tumeacha mipaka yote wazi kiasi kwamba
a)
vijana wangapi wanaangamia kwa ubwiaji unga unaopita ovyo? mipakani kote? je huo ni usalama wa mipaka!
b) Tunajivuniaje ulinzi na usalama katika mipaka yetu iwapo tembo, swala pundamilia nk wanauwawa na kutoroshwa mchana kweupe na kwakuwakosa/kuibiwa kwake unaweza eleza watanzania wangapi wanakufa kwa kukosa matibabu au elimu bora ambayo wangeipata kama ujambazi huu ungedhibitiwa?
Kwa taarifa yako wanaoangamia kwa bundunki na ujambazi huko mipakani hususani Kagera, kigoma nk sina utafiti wakina lakini kwa akili ya kawaida huwezi linganisha na wale wanaopoteza uhai na wanaoadhiririka na madawa ya kulevya nchi nzima. Kikwete yupo, mwema yupo, pinda yupo lakini nikama simba wasio na meno hawajui watendalo wala majukumu yao.
Je ni kwanini basi
a) malawi tunazozana nao, na leo asubuhi bbc kama sikosei nilipokuwa nasikiliza Bwana Thabo mbeki na mwenzie wa msubiji wapatanishi wameahilisha kuja TZ bila sababu zinazoeleweka baada ya kutoka malawi ilikuwa waje hapa ..........tafakali
b) museveni ni kama mtoto wa TZ amekulia na kusoma udsm, vipi sasa anaonekna nayeye kujitenga na waliomlea na kumkuza?
c) kenyata huko kenya yaleyale
Swali unadhani wote hao hawana akili? isipokuwa sisi? nini kinaendelea katika siasa zetu anga za kimataifa? hatukuwahi kuyaona haya tangu kipindi cha Nyerere, Mwinyi, mkapa vipi leo....... huoni kunatatizo?