Hivi mkuu mbona sikuelewi? Unataka kusema kwamba changamoto ya wahamiaji haramu isishughulikiwe kwasababu kuna changamoto nyingine zinatukabili hivi hizi ni akili kweli??
Kuhusu wahamiaji haramu kujishughulisha na ujambazi na kupora watu huko Kigoma na Kagera ninao maana nimesikia ushuhuda wa waathirika mara nyingi wakisema kuwa muonekano na rafudhi za majambazi hao si za kitanzania more over wanatumia silaha kali za kivita ambazo it is very difficult kwa raia wa kawaida wa kijijini Nyakahanga kuipata hivyo kwa namna yoyote ile inatokea nchi jirani kwa kuwa wenzetu wamekuwa kwenye vita kwa muda mrefu na silaha zimezagaa kila kona. Pia kuna ushahidi hadi wa baadhi ya majambazi yaliyowahi kukamatwa maeneo hayo kuthibitika kuwa ni raia wa kigeni.
Tatu si kweli kwamba kipindi cha Nyerere tulikuwa na ugomvi na wakoloni tu hata Kenyatta hakuwa kuwa swahiba wa mwalimu kutokana na kupishana kwa ideologies zao ambapo Kenyatta alikuwa ni bepari mwenye kuwalea wazungu huku Nyerere ni Mjamaa asiyepikika na wazungu mpaka alifikia hatua ya kuufungia ubalozi wa Uingereza nchini. Iddi Amin hakuwa mkoloni wala Kamuzu Banda hakuwa Mzungu hivyo acha kuupotosha ukweli. Halafu kuonyesha ulivyomburula unasema kuwa wakati wa Vita ya Uganda Nyerere hakuwafukuza waganda wanaoishi kinyume na sheria nchini, awafukuze vipi ilhali hawakuwa kikwazo kwa usalama wa watanzania waishio mipakani na kwa namna nyingine walikuwa wapo naye pamoja kuhakikisha utawala wa Idd Amin unang'oka Uganda.
Hivi unasema haya ukiwa upo mzima haujaonja hata kidogo kweli? Maana hizi sikukuu may be najibizana na wewe kumbe umelewa.
MWILI NYUMBA
Hayo uliyoyataja juu pia ni moja ya changamoto pia ambazo nchi inazipitia lakini na hili la uhalifu eneo la mipakani ni moja wapo
Changamoto hutatuliwa.
1. Je wale wasafirishaaji na wauza dawa za kulevya ambao kikwete alikiri kuwafahamu zaid ya miaka miwili sasa amechukuwa hatuagani? Hujajibu swali hili
2. Kila mkowa unamateja na waathilika wa madawa ya kulevya kwa maelefu nchin kote, huoni kwamba hili nijanga baya kabisa? Kikwete aanawafahamu wachuuzi amekaa kimya.......kwanini anyamazie watoto wakitanzania wakiteketea nchi nzima? hili janga linaletwa na wanyarwanda au nani na kwanini.............. Hujajibu swali hili
.
Hivyo sidhani kama ni kosa kwa serikali kutatua changamoto hii lakini pia bila kuzisahau hizo nyingine ulizozitaja
.
Lini itatatua wakati ndege zinaendelea kutua na kuchukuwa wanyama na raslimali zetu kila siku mkuu
1. Wagonjwa wangapi wangepona kwa matibabu bora kama tungedhibiti na kufaidi upatikanaji wa madawa na vifaa tiba bora kutoka mapato ya madini na wanyama pori? Hospitali zote za erikali huduma nimbovu kupita kiasi wewe huoni hawa maelfu wanaoteketea na huoni kama hili ni tatizo? Hujajibu swali hili
.Mimi Kagera ni ujombani kwetu na adha wanayoipata wajomba zangu naifahamu kupita kiasi ndiyo maana naliunga mkono hili kwa nguvu zote
Sijasema kagera pasiwekewe ulinzi na hoja kwamba ni ujombani kwenu hii ni sera mfu ya ukabila tunaongele utanzania hapa.
1. Je hiyo ndiyo njia pakee na sahihi ya kulinda mali na usalama wa raia hususani mipakani? kufukuza wasio na vibali vya kuishi nchini? Nasisi wakwetu wafukuzwe huko kenya, malawi, kongo nk? Unauhakika hao ndio wahalifu ? kivipi mkuu Hujajibu swali hili
2. Tanzania imeshakaa na viongozi wa rwanda mara ngapi, kujadili hali tete ya maisha ya watanzania/wanyarwanda na jinsi ya kulitatua tatizo hukompakani unavielelezovyovyote mkuu. Hujajibu swali hili
.Ni upungufu wa kufikiri kusema eti tuache huu upuuzi uendelee kisa twiga wanapandishwa QATAR AIRWAYS na tembo wanauawa kila siku
Upuuzi ni upi
1. Kuacha mamilioni ya watanzania wakifa kwa kukosa tiba na elimu bora kwa kisingizio cha umasikini walowezi wakituibia raslima na utajiri wetu? au Hujajibu swali hili
2. Kushupalia kabila la wanyarwanda ambao idadi yao nadhani haifikii hata wale wa Dar es salaam, na kwa ujinga na ulimbukeni tunashupalia propaganda za kisiasa kwamba Rwanda ni tishio kwa usalama wa Tanzania. Tunauwezo, Jeshi kubwa na bora, tunaraslimali watu nk isitoshe wanyarandwa hatuna uadui nao ni papara tu za kiongozi wako kikwete. Hujajibu swali hili
.Pili uache unafiki mkuu, hakuna kipindi Tanzania ilikuwa na maadau wengi kama Kipindi Nyerere ni Rais, sera ya Tanzania kuwakomboa majirani zake kupata uhuru tulichukiwa kila kona
1. Hapa ndipo unapooneha uwezo kufikiri unapwaya.
-Nyerere hakupigana dhidi ya waafrika wenzie, alisadia nchi hususani kusini mwa afrika Msubiji, Angola, Zimbabwe, Afrika ya kusini nk dhidi ya wareno, wadachi, makaburu nk kupigana kudai na kupata uhuru wakujitawala unamaana kikwete naye anafanya hivyo? Hujajibu swali hili
-Kikwete hapigani vita ila anawachimba viongozi na majirani zake (waafrika wenzake kwenye himaya zao) lengo lake moja tu kujipalilia njia ajulikane kimataifa lakini sio kihalali ila kwa hila, nahapa ndipo mtafaruku na malumbano yanapoanza. Jadili walau mawazo yako
Wakati tunapigana vita na Uganda hatukuwa in good terms na Kenya,South Africa,Zimbabwe etc ambazo zote zilikuwa chini ya wakoloni na hata Hawa Wamalawi unaowataja pia mgogoro wao juu ya Ziwa Nyasa ulikuwepo palepale.
-Nyerere hakupenda ukoloni, lakini Mwalimu aliingia vitani akiungwa mkono na watanzania wote wazee, vijana wake kwa waume kumtwanga IDD AMIN DADA kwasababu hakukurupuka, na watanzania tulivamiwa hatukuvamia wala hatukuwafukuza waganda. jadili hoja usipotoshe kama ulivotaka ufanya hapo juu
-Nyerere hakujishebedua eti autafute umaarufu kimataifa ili akistaafu aitwe UN akapewe madaraka. Mwalimu alijitoshereleza alikuwa na hekima na aliona mbali. huwezi mlinganisha mwalimu na mtu kama kikwete ambaye ameshindwa kila kitu. Unasemaje na nini mtazamo wako?
Hebu fuatilia historia ya nchi yako (kama wewe ni Mtanzania) maana sina uhakika kama ni Mtanzania.
Historia ya nchi yangu kifupi
1. Tumekuwa tukijulikana kimataifa popote dunia kama kisiwa cha amani na kila mtanzania alipokutana na mwenzake tuliitana ndugu.
SWALI
Je hii falsafa bado inaendelea? kama ndiyo jadili kivipi nakama haipo jadili kwanini imetoweka na nani alaumumiwe wanyarwanda au kikwete na mawaziri wake?
Hujajibu swali hili