Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Ingawa hapo nyuma ndani ya thread hii nimeonyesha mafanikio ya JK, Lakini hili la kupanda kwa gharama za umeme mheshimiwa amechemsha , tena amechamsha mno, jitihada zake za kuinua kiwango cha maisha zinakwamishwa na kupanda kwa gharama za umeme, Just imagine kuna mtu kanunua umeme wa shilingi 7000 kapewa 0.7 Units, eti service charge, service charge ni upuuzi gani ati!. Ni sawa sawa na kwenda sokoni kununua bidhaa halafu mfanyabiashara akukate hela ya kukuhudumia on top ya hela ya bidhaa yenyewe!
 
Nikweli kuna mazuri mengi ameyafanya na mabaya mengi yamefanyika chini ya uongozi wake. Mimi ningependa tu kuuliza kweli kweli Rais na serekali yake na wapelelezi wote waliopo hapa Tanzania kweli hii nchi imeshindwa kuzuia uingizwaji wa madawa ya kulevya?? Vijana wengi wa kitanzania wameharibika kwa kutumia madawa ya kulevya. Nina hakika hawa tunao wasikia wanakamatwa kila siku ni watu wadongo sana katika mtandao wa watu wanaoingiza madawa ya kulevya. Je hii serekali na huyu kiongozi tulienae kweli wameshindwa kuzuia kabisa hii biashara chafu ya kuharibu vijana wa kitanzania???
 
Endelea kujipa moyo wakati wazee wako huko kijijini hawajui wanakula mara ngapi kwa siku
 
Hayo yanaweza kufanyika hata chini ya uongozi wa kijeshi, acha kudanganya watanganyika
 
pia amefanikiwa kumfunga Babu Seya na kuwashauri wana ccm wasiwe wanyonge
 
Sisi walimu hatutamsahau kwa kututelekeza,Mishahara duni pamoja na malimbikizo ya walimu tangu mwisho mwa awamu yake ya kwanza hadi leo hii hakuna dalili ya malipo,hii ni dharau ya hali ya juu kwa walimu huku pesa nyingi za nchi ikiliwa na chama chenye wanasiasa wengi serikalini(CCM). Cha kusikitisha wizara nyeti kama ya fedha kushikwa na mwendawazimu kama MWIGULU NCHEMBA yaonyesha ni jinsi gani tusivyo serious na uchumi wa nchi hii. Go Kikwete go,walimu tubaki tunajipanga upya!
 
Amejenga chuo kikuu UDOM, ameongeza freedom of speech, amejenga barabara kama utitiri, ameboresha mishahara kwa wa2mish wa umma. Ametoa mwanya kwa vijana wauze unga na kujizoleo utajiri wa muda mfupi.
 
Amejenga chuo kikuu UDOM, ameongeza freedom of speech, amejenga barabara kama utitiri, ameboresha mishahara kwa wa2mish wa umma. Ametoa mwanya kwa vijana wauze unga na kujizoleo utajiri wa muda mfupi.

mishahara ipi aliyopandsha labda ya mawazri...kikwete hajafanya la maana zaidi ya kuwasaliti waliombeba kama akna lowasa...kikwete hajafanya kitu anasimamia kumalizia miradi ya mkapa...
 
Sisi walimu hatutamsahau kwa kututelekeza,Mishahara duni pamoja na malimbikizo ya walimu tangu mwisho mwa awamu yake ya kwanza hadi leo hii hakuna dalili ya malipo,hii ni dharau ya hali ya juu kwa walimu huku pesa nyingi za nchi ikiliwa na chama chenye wanasiasa wengi serikalini(CCM).
Sema wafanyakazi mzee sio walimu peke yenu!
 
Akitaka tumkumbuke aondoe service charge ya umeme kwanza haiingii akilini. yaani unanunua bidhaa halafu unalipia na ghalama za kuhudumiwa? wakati huo ndo wajibu wa muhudumu....hii haikubaliki hata kidogo. yaani unanunua bia moja kisha unalipia na huduma? ama kweli huu ni wizi kabisa. na mbona haipo hivyo kwa mashirika mengine ya umma ama biashara nyingine? ACHENI UHUNI TANESCO!!
 
Mkuu kwa nini una-quote bandiko langu halafu unatukana? Inakuwa kama unanitukana mimi vile wakati na mimi nayashangaa haya ma-Zombie ya CCM yanayotudanganya na maendeleo ya mikopo!!Naomba unitake radhi mkuu!!

Hata bajeti za vyama vya upinzani vingini pesa za serikali, tena za walalahoi ambao wengine sio wanachama wa chama chochote cha siasa lakini zinatumika kuendesha shughuliza vyama, JK simamisha hizi ruzuku kwa vyama kila chama ikiwemo ccm kijitegemee kwisha ...
 

watanzania ujinga tutaacha lini...........................picha ikiwekwa ya richomond utachelea kwasababu mnachotaka kuona ni output ya project na sio input ya project

lete mkataba ya project tukuone wa maana picha(architectural picture ) kama hizi watu wanozao nyingi kwenye mafaili yao, watanzania wanafaidika nini na hizo project let us go deep of this project Tanzania
 
Back
Top Bottom