Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

Serikali ya Kikwete Imefanya nini 2005-2015...

CHADEMA wakiona hivi wanachanganyikiwa kabisa, ndio maana kwenye majukwaa yao ya kisiasa hawana jipya zaidi kuanzisha fujo ili wapate la kuongea. Hongera sana JK.
 
Jamani angeboresha na hospital maana hakuna huduma pia vifaaaa hayo mabarara na majengo ndio maisha boraa wakati watu wanakufa kwa kukosa hudumaa wao wanaenda kutibiwaa India na Marekaniiiii
 
images.jpeg images2.jpeg ALeqM5igBPNg3rlinxPt9M9Y6t6V0dZZGA?size=m.jpeg

chini ya uongozi wa amiri jeshi mkuu jk, tanzania imeendelea kutoa mchango unaohitajika kijeshi kwa ndugu zetu waliokuwa katika zahama na hivyo kuliletea heshima taifa letu, hapa wanajeshi wa tanzania wakiwa katika uwanja wa mapambano kumuondoa muasi kanali bacar wa Comoro
 
Mkuu Annael endelea kuwawekea Picha! Mbona umeacha! Maandiko matakatifu yanasema usichoke kutenda mema, kwani utavuna kwa wakati.
 
Kama hujaridhika na haya uliyaona pichani, huna tabia ya kuridhika na kuaprishieti, hata yakifanywa hayo uliyoyataja hapo juu hutaridhika pia.

aliochofanya ni wajibu wake kufanya sio hisani na alitakiwa afanye zaidi ya hicho, mtu kujisifu kuhudumia familia yake ni ujinga kwa kuwa ni wajibu wake.
 
Nimendawazimu tu atakaekubali kuindosha Serikali ya CCM kwa vile Rais Kikwete amesawazisha makosa yote ya nyuma
- Amejenga mabarabara mara mbili ya idadi ya kilomita alizozikuta
- Amejenga madaraja makubwa sana 3 kati ya 5 aliyoyaahidi Nyerere
- Ameleta vyuo vikuu zaidi ya 44 ? mara 4 zaidi ya waliowakuta
- Amewezesha wanafunzi 160,000 wa vyuo vikuu mara 4 zaidi ya aliowakuta
- Amejenga chuo kikubwa kuliko vyote EAC.
- Ameejenga chuo kikubwa cha sayari kwenye ukanda huu cha Nelson Mandera
- Amepeleka sekondari hadi kwenye kata
- Amezalisha umeme wa mega wait 1500 mara mbili zaidi ya alioukuta
- Ameanzisha umradi wa kupeleka umeme vijijini?
- Anajenga bomba la gesi kubwa toka Mtwara hadi DAR
- Anajenga barabara ya mabasi yaendayo haraka.
- Anayekubalika na viongozi wote wakubwa wa Dunia hii
- Aliyeanzisha hospital ya tiba ya moyo nchini
- Aliyesogeza huduma za afya karibu na wananchi
- Aliyejenga miundombinu ya afya
- Aliyeboresha huduma ya maji nchini
- Aliyeongeza ajira nchini
Jamani acheni mzaha si tutachekwa tukiiondosha CCM na kuwaweka vichaa?
Kweli ni kichaa tu ambaye haoni mafanikio ya JK
 
Mi sio mzungumzaji wa siasa kivile, ila nataka fahamu jambo bila unafki wala kuhusisha vyama vya siasa! Raisi wetu JK lazima kuna mazuri kafanya. Embu tuambiane hapa! Msisitizo: Mambo mazuri tu aliyoyafanya na anayoyafanya Mh Raisi. Bila chuki wala kebehi. Kama inavyokuaga kwa wasifu wa marehemu, sasa Mkuu bado yu hai tuzitaje sifa zake nzuri tu.
 
Mi sio mzungumzaji wa siasa kivile, ila nataka fahamu jambo bila unafki wala kuhusisha vyama vya siasa! Raisi wetu JK lazima kuna mazuri kafanya. Embu tuambiane hapa! Msisitizo: Mambo mazuri tu aliyoyafanya na anayoyafanya Mh Raisi. Bila chuki wala kebehi. Kama inavyokuaga kwa wasifu wa marehemu, sasa Mkuu bado yu hai tuzitaje sifa zake nzuri tu.

Kuna mambo ya msingi sana ya kuzungumza zaidi ya 'kumtafutia' sifa Raisi Kikwete, lakini kwa kawaida kipimo cha mafanikio ya mtu hutegemea vitu mojawapo ni uwezo wa utekelezaji wa mipango yake.

Mfano, mtoto mdogo awapo anakua humpatia sifa kwa kuona anatekeleza yale yanayo paswa kutekelezwa kwa watoto wa umri wake huo, ila iwapo mtoto tufanye wa miaka 7 anakojoa kitandani, au wa miaka 4 hajajua kuongea, hata kama anakipaji, uwezo fulani wa kuperform bado kuna walakini mkubwa kwake, hata kuhitaji uchunguzi zaidi kujua ni nini hasa kinaweza kuwa na uwalakini pia.

Hivyo basi, kama ulivyosema .."wewe si mzungumziaji wa siasa kivile"..Ningekushauri, ili tujue mafanikio/sifa zake tungejua ;
1. Ni nini anapaswa/alipaswa kufanya katika utawala wake?
2. Nini kimefanyika hadi sasa kwa ukamilifu?
3. Nini hakijakamilika? Kama bado, makusudio au mipango ni ipi?
4. Ni nini hakikuwa katika mipango, lakini kimefanywa pengine kwa ukamilifu?

Hapo ndipo tunaweza tukajua tumpime namna gani, na anastahili sifa gani, vinginevyo ni 'kumpamba kama maiti zinavyopambwa kwa sifa katika misiba' hata kama wakati wa uhai wake hakuwa kama sifa zake. (No offence Mr. President)
 
anahudhuria sana misiba ya wasanii.
ametembea dunia nzima.
 

IMEFANYA HAYA: ANGALIA HIZI PICHA HAPA CHINI SIO MNAKAA NA KUSHOBOKEA SHOBOKEA UPUZI

images
images
9k=
images


Hapa sijakuonyesha bado wodi ya majeruhi pale Muhimbili (MOI) na hospitali nyingine. 53 yrs ccm watu wanaishi maisha magumu kiasi hiki pamoja nautajiri mkubwa wa rasilimali (madini, mbuga za wanyama, kodi lukuki wanazokusanya TRA kwa ubabe na kuwanyonya watz) halafu na kikofia chako cha kijani unatuambia habari za mafanikio. HATUDANGANYIKI NG'O!!!
 
Amejenga na kusimamia ujenzi na ukamilishaji wa mtandao wa barabara za lami nchi nzima
 
Chini ya utawala wake amefanikiwa kujenga Vyuo vikuu zaidi ya kumi vya umma na vya binafsi pamoja na taasisi za kidini
 
Amejenga hospitali za rufaa kila mkoa na kuiboresha hospitali ya rufaa ya muhimbili. Aidha hopsitali za wilaya zimeboreshwa kwa kupelekewa madaktari bingwa mmoja mmoja...pia vituo vya afya na zahanati kwenye kata na vijiji zimejengwa nchi nzima
 
Back
Top Bottom