Serikali ya JK Mufilisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK Mufilisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Mar 30, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Waziri Magufuli hoi

  NA MWANDISHI WETU

  30th March 2012

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo


  Imebainika kuwa chanzo cha miradi mingi ya barabara nchini kukwama kumalizika kwa kipindi kilichopangwa inatokana na madeni inayodaiwa Wizara ya Ujenzi, Sh. bilioni 331 kutoka kwa makandarasi hadi Februari, 2012.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema mwisho wa mwaka 2009-2010 Wizara ya Ujenzi ilikuwa na madeni ya Sh. bilioni 44 na hadi kufikia Juni 30,2011 madeni yaliongezeka mpaka Sh. bilioni 420.
  Aliongeza kuwa kufikia Februari 30, 2012 Wizara ya Ujenzi ilipokea Sh. bilioni bilioni 384 kutoka Hazina ambayo ni pungufu ya madeni inayodaiwa.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango, alisema wizara hiyo haipati fedha katika muda mwafaka kutoka Serikalini, ila wamehaidiwa kupewa Sh. bilioni 317 na Serikali kulipa madeni hayo.

  Akitaja miradi ambayo imesitishwa kuendelea kutokana na wakandarasi kuidai Wizara ya Ujenzi, Cheyo ni barabara kutoka Bariadi kwenda Lamadi, Ndundu kwenda Somanga yenye urefu wa kilomita 60, iliyogharimu Sh. bilioni 58.8 na Wizara imeshalipa Sh. bilioni 46 na kudaiwa Sh. bilioni 12  CHANZO: NIPASHE
   
 2. maziwa ya mgando

  maziwa ya mgando Senior Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmh, hadi kumrudisha huyo mtu kulikuwa na uwalakini.
  Walijua wameshachemka parefu.

  Si ujenzi tu, angalia sasa hivi upatikanaji wa mafuta kwa magari ya serikali umekuwa wa kibaba
  Hakuna sehemu yenye pesa kabisa.

  Yaani mbele kua kiza kwa kweli.
   
 3. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio hilo tu,

  Serekali imesema kuwa wao ndio watapeleka 20% ya mishahara ya wafanyakazi wake kwenye mifuko kama PPF, NSSF, LAPF nk. Lakini kuanzia mwaka jana mwezi wa saba hakuna kilichopelekwa. Angalia website ya PPF uone kama kuna kitu kimepelekwa huko.

  Serekali kupitia HESLB wamebadilisha mkataba ili waliokopeshwa walipe haraka badala ya mkataba wa mwanzo wa miaka kumi. Ina maana serekali haina hela, wanataka wachukue hela ya mfanyakazi wake.

  Lakini nenda uongee na wakurungenzi wa taasisi za serekali, utaogopa. Kuna mkurugenzi ameomba OC ya milioni tano analetewa nusu milioni ambayo ina uwezo tu wa kununulia dawa za kusafishia vyoo, haiwezi hata kulipia umeme, maji nk. Sasa usishangae serekali inadaiwa sana na taasisi kama TANESCO, DAWASCO nk.

  Bado kuuza watu wake ndio imebakia
   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  serikali ipi ya TZ haikuwa muflisi?
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,087
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  Hata tbc imefilisika nn kitapona. wao wanaruka anga kwa anga tu.
   
 6. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fifty years of independence,and stil economically dependant!and no ways to let ourselves out of it,what a country.
   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,171
  Likes Received: 1,174
  Trophy Points: 280
  Wananchi watauzwa kwa mara ya pili?
   
 8. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Ngoja niangalie pochi langu.....ahaaa bado zipi Mhe Mkullo naomba unitafute niwape japo heal ya chai mpate changamoto za kuanza kazi
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mbona tittle haiendani na content au ni usingizi wa mleta mada
   
 10. G

  Galaticos Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  After 50 years: Tumeweza, tumethubutu na tunasonga mbele....
   
 11. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  We kilaza huoni kuwa inashindwa kulipa madeni yake ya ndani achilia mbali ya nje. Soma michango ya wenzako hapo juu ili uweze kuelewa.

  Au wewe ni magamba unaona lakini huangalii!
   
 12. k

  ksalama0 Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Magamba kweli ni tatizo hata kama nyumba inaungua atatetea tu eti moto ni mdogo watazima, hebu wana magamba kabla hamjaongea jaribuni kufikiri sana. maana wengi imani imetoweka juu yenu.

   
 13. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kutoka billion 44 hadi billion 420 hapa katikati tulipita uchaguzi
   
 14. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Serikali punguza wafanyakazi kwa asilimia 40%.

  Acha kununua magari, wakopeshe wafanyakazi wanunue magari yao wenyewe.

  Chukua vijana wenye nguvu kutoka vyuo vikuu wape kazi uone mambo yatakavyoenda fasta na expenses zitakavyopungua.

  Ziba mianya ya kodi. Punguza kodi kwa kufuta kodi zisizo la lazima na kupunguza zile ambazo zinaumiza wafanyabiashara hawa wadogo. Tanua tax base watu wengi walipe , sio mnatubana sisi tu wafanya kazi.

  Ongeza usimamizi kwa kuweka systems nzuri TRA (wawezeshe)

  Ongeza penalty kwa wanaokwepa kodi ili watu wasifikirie kukwepa kodi.

  Wawezesheni wakulima wa kati na wakubwa muwawekee na utaratibu wa kuchangia japo kidogo
   
 15. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nchi hii imeshauzwa na hela zooote zimeliwa na ****** na jamaa zake, hatuna tunachozalisha hatimae hatuexport kitu, kazi yetu ni kuiport tu, ni sawa na omba omba ambae anategemea ufadhili wa wapita njia.CCM imetufikisha hapa jamani kwani licha ya kutumia hela vibaya ana kuto tafuta vyanzo vya fedha pia wameacha soko huria kila mtu aweke bei ya bidhaa anavyotaka, mi sielewi kwa nini watz tuko home bado kwa nini hatuingii barabarani kushinikiza raisi ajiuzuru? Pale lybia walikuwa wanamaisha bora lakini wakamchoka gadaffi, kwa nini sisi na maisha magumu hivi tumeridhikatu, kwa hio sisi na viongozi wetu tunamatatizo ya kimaamuzi.
   
 16. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Haya yote yasingekuwepo kama WAANOSTAHILI KULIPA kodi wangekuwa wanalipa kodi.
  Waanchi wamebanwa weee hadi kupumua hawapumui, jamaa wanapeta tu
   
 17. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndio matokeo ya Tanzania badala ya kugundua jinsi ya kuukomboa uchumi wetu tuliishia kugundua 'nazi'.....'viongozi vichwa nazi! Hi nyema tuamini ni kwanini hata wa-Kenya wanatupuuza kila siku kwa viongozi kukosa fikra na utawala finyu! Kenya majuzi waligundua na uchimbaji mafuta kwa mabilioni ya mapipa! Sisi je! Blaaaaaaaaaa, blaaaa, blaaaaa na viongozi kulalalaaaaa, na kusingizia kila sababu! Vichwa nazi!

  JK na Uongozi wa nchi....Madaraka aliyopewa ni kama mtoto kavalishwa kanzu ya babu yake...hata mwenyewe alishakiri toka awali...na bado hiyajatufika! Bado miaka mingine minne....!
  Dr Slaa alishasema toka awali kuwa 'kuichangua CCM ni maafa kwa taifa....' Huyu jamaa habahatishi ktk kauli zake....! Haya maafa bado hayajatufika...ndio yanaanza kuja!

  My Take: Hawa Viongozi na kina magamba wenzie, na wenzake...watakapoanza kujua muda wa kukaa madarakani umebaki mwaka mmoja au miezi, ndio mtajua jinsi nchi inavyofilisiwa....! Napo ndipo tutayakumbuka maneno ya Dr Slaa na kulia mara-3 kabla ya jogoo hajawika!
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Na bado wanajitahidi kufanya kila wawezalo ili waendelee kuwa madarakani. Nawapongeza wanajeshi wa nchi ya MALI
   
 19. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ukiwaambia magamba nchi imefilisika watakuambia sera ya CCM ni kudumisha amani, umoja na mshikamano. Wanashau Amani ni zaidi ya kuwepo vita; mtu anayelala njaa hana amani, watu wakiishi maisha duni hakuna mshikamano. Nchi hii imefilisiwa na serikali ya awamu ya nne kwani kila kiongozi na mtumishi wa umma aliyepo nafasi ya juu amajilimbikizia mali. Watoto wetu wanasoma shule za kata zisizo na sifa wao wanasoma saint Mary, St. Patrick n.k Sisi tunakosa huduma za afya katika hospitali zetu wao wanatibiwa India au katika hospitali binafsi ambapo mlalahoi hawezi. SERIKALI IMEFILISIKA
   
 20. moto ya mbongo

  moto ya mbongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 336
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Asante Ileje kwa mada moto moto
   
Loading...