Serikali ya JK Mufilisi

Wataalamu wa Kichina na Kivietinam wanashangaa jinsi uduni wa Mtanzania unavyozidi kila siku! Wanadai hata uwekezaji wa wageni ukiongezeka hakutakuwa na unafuu wo wote kwa kuwa mishahara itakayotolewa haitatosha kumudu gharama za maisha. Hakuna juhudi za kutosha kudhibiti kuporomoka kwa thamani ya shilingi!

Hivyo serikali inashauriwa kuwasaidia wakulima wadogo wapate ardhi yenye rutuba na ipunguze gharama za pembejeo ili uzalishaji wa mazao ya kilimo na hasa chakula uongezeke. Kwa kufanya hivyo bei ya chakula itashuka na angalau mishahara ya watumishi katika sekta ya umma na binafsi itakidhi mahitaji muhimu ya familia.
 
Serikali punguza wafanyakazi kwa asilimia 40%.

Acha kununua magari, wakopeshe wafanyakazi wanunue magari yao wenyewe.

Chukua vijana wenye nguvu kutoka vyuo vikuu wape kazi uone mambo yatakavyoenda fasta na expenses zitakavyopungua.

Ziba mianya ya kodi. Punguza kodi kwa kufuta kodi zisizo la lazima na kupunguza zile ambazo zinaumiza wafanyabiashara hawa wadogo. Tanua tax base watu wengi walipe , sio mnatubana sisi tu wafanya kazi.

Ongeza usimamizi kwa kuweka systems nzuri TRA (wawezeshe)

Ongeza penalty kwa wanaokwepa kodi ili watu wasifikirie kukwepa kodi.

Wawezesheni wakulima wa kati na wakubwa muwawekee na utaratibu wa kuchangia japo kidogo
Umeacha mojaa muhimu. wauze ATC na TRL maana hayana tija.
 
Umeacha mojaa muhimu. wauze ATC na TRL maana hayana tija.

ATC na TRL ni vizuri yakaimarishwa kwa kuwa ni nyenzo muhimu kwa kukuza uchumi wa nchi! Hivyo kuyauza ni janga la kiuchumi
 
Back
Top Bottom