Kwa mara nyingine serikali ya CCM imechanwa laivu. Haina aibu, huruma wala utu. Ajabu na kweli yenyewe inaona sawa tu.
Inamwakilisha nani kwenye minajili hii? Labda walamba asali, wahuni au wale vijana wa hovyo?
Yamejiri laivu kwenye mkutano wa wafanya biashara Kariakoo na Waziri Majaliwa. Kwamba polisi, TRA, wizara ya fedha ni majizi, dhulumati, wanyanyasaji nk?
"Kwamba vitendo vya rushwa, manyanyaso kutoka kwa watumishi wa TRA, Jeshi la Polisi pamoja na kodi ya stoo vilikuwa miongoni mwa shtuma zilizotolewa huku Waziri Mkuu akivitaka vyombo, TRA na Jeshi la Polisi kujitafakari kutokana na kile kilichoelezwa na wafanyabiashara."
Kwamba uchafu huu ukiendelea serikali ipo na imekuwa imetulia tu? Sana sana ikiwataka watuhumiwa kujitafakari tu?
Serikali ya walamba asali au wahuni inapojiitisha kujitafakari ndani ya uponzani ulio usingizini, labda tusubirie maajabu ya Mussa.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao baina yake na vigogo wa wizara wa Fedha na Mipango, Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mawaziri, Dk Mwigulu Nchemba wa fedha na mipango, Dk Ashatu Kijaji wa viwanda, biashara na uwekezaji, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata pamoja na watendaji wao wameshiriki kikao hicho. Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka.
Kikao hicho kimefanyika leo Alhamisi, Mei 17 Ikulu ya Dar es Salaaam ikiwa ni siku moja kupita tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuumaliza mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo uliokuwa umedumu kwa siku tatu kuanzia Jumatatu ya Mei 15 hadi 17, 2023.
Katika kikao hicho, mawaziri wa fedha, Dk Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Ashatu Kijaji, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kijaji waliokuwapo walishtumiwa kwa na wafanyabiashara hao kushindwa kuwawekea mazingira mazuri ya biashara.
Vitendo vya rushwa, manyanyaso kutoka kwa watumishi wa TRA, Jeshi la Polisi pamoja na kodi ya stoo vilikuwa miongoni mwa shtuma zilizotolewa huku Waziri Mkuu akivitaka vyombo, TRA na Jeshi la Polisi kujitafakari kutokana na kile kilichoelezwa na wafanyabiashara.
Mbali na Dk Mwigulu, Dk Kijaji, wengine waliokuwapo kwenye kikao hicho cha Majaliwa kilichofanyikiwa Viwanja vya Mnazi Mmoja ni mawaziri, Angellah Kairuki wa Tamisemi, Hamad Masauni wa Mambo ya Ndani pamoja na Katibu Mkuu-Ikulu, Mululi Majula Mahendeka.
Majaliwa aliunda kamati ya watu 14 ukijumuisha maofisa wa Serikali na wale miongoni mwa wafanyabiashara kwenda kupitia changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na kuona jinsi ya kuishughulikia.