Waziri Ashatu aagiza taasisi za serikali kuacha kufungia biashara

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amezitaka taasisi zote za serikali zinazohusika na ukaguzi na udhibiti kuacha kufungia biashara na viwanda, kwani kufanya hivyo ni kusimamisha uchumi wa nchi.

Kijaji alisema katika maonesho ya wafanyabiashara yaliyoandaliwa na
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) jijini Dar es Salaam.

“Naomba nisisitize kwa mamlaka zote za serikali za udhibiti ziendelee kuruhusu biashara zifanye kazi hata kama kuna jambo hatukubaliani kati yetu wakati tunashughulikia jambo lile hatuna sababu ya kusitisha kusimamisha shughuli za biashara, ni kusimamisha uchumi wa nchi.

“Kwa hiyo ni muhimu sana tunapoelekea kuhitimisha utekelezaji wetu wa dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025 tusisitishe shughuli yoyote ya kiuchumi kwa jambo lolote lile, kwani mazungumzo ni msingi wa sisi kuwa na uchumi imara, " alisema
 
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amezitaka taasisi zote za serikali zinazohusika na ukaguzi na udhibiti kuacha kufungia biashara na viwanda, kwani kufanya hivyo ni kusimamisha uchumi wa nchi...
Wenye mamlaka hudui hayo ni maneno ya wanasiasana na hayana nguvu yoyoyte ya kisheria
 
Back
Top Bottom