Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 4,181
- 6,214
Nasema hivi kupitia sababu zifuatazo
- Katiba hii ya mwaka 1977 ilitengenezwa na mwalimu julius Nyerere, ila cha ajabu miaka ya mbeleni kwa nyakati tofauti Nyerere amekuwa akionyesha mapungufu ya hii katiba ila hakujaribu kuibadilisha sanasana aliiendelea kuifanyia amendment mpaka anafariki
- Wakati wa utawala wa mwinyi katiba ilifanyiwa Marekebisho sababu tulia-adopt capitalism na vyama vyingi kwa katiba ile ambayo ilikuwa inalalamikiwa instead ya kubadilishwa tuliendelea kuifanyia Marekebisho swali kwanini ilikuwa ni ngumu kuibadilisha jumla???
- Wakati wa utawala wa mkapa nayeye kwa nyakati tofauti aliifanyia amendment swali la kujiuliza kwanini hakutaka kuibadilisha jumla
- Wakati wa kikwete alimteua warioba ili akusanye maoni ya wananchi na atengeneneze rasimu ya katiba alikamilisha ila mchakato ulifanyiwa zengwe again tukafeli hatukupata katiba mpya
- Wakati wa utawala wa magufuli yeye mwenyewe alisema hakuahidi katiba mpya means hakukua na mchakato wowote wa katiba mpya ndo habari ikaishia hapo
- Mwaka huu 2025 tumeahidiwa katiba mpya je watafanikiwa au watafeli kama wengine wa nyuma waliofeli
- Ccm hawawezi kutupa katiba mpya prove nimeonyesha hapo juu
- Hata wakitupa katiba mpya basi itakuwa mbovu kuliko hii
- Spika wa bunge anatakiwa achaguliwe na wananchi na asiwe affiliated na chama chochote wote ni mashahidi wa spika wa bunge wa miaka ya karibuni sina haja ya kuwaongelea sana
- Jaji mkuu anatakiwa achaguliwe na wananchi
- Majaji wa mahakama kuu wanatakiwa wachaguliwe na mahakama yenyewe
- Mkuu wa Takukuru anatakiwa achaguliwe na wananchi
- DPP anatakiwa achaguliwe na wananchi na DCI anatakiwa awe kwenye ofisi ya DPP na sio chini ya polisi
- Mbunge anatakiwa achukue majukumu ya Mkurugenzi sio sawa mbunge anachaguliwa alafu anaenda kuishi dar jimboni kwake anarudi kama mtalii sio sawa anatakiwa awe ana-sign kwenye mashine ya biometric kama wafanyakazi wengine hii tutapata watu genuine wanaopigania wananchi
- Waziri asiwe mbunge kwa sababu majimbo mengi ya mawaziri yamepwaya
- Anayeshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi awe mkuu wa kambi ya upinzani bungeni
- Mkuu wa mkoa achaguliwe na wananchi
- Msajili wa vyama vya siasa, mkuu wa tume ya uchaguzi na wajumbe wa tume ya uchaguzi hawataki kuchaguliwa na Rais bali kupitia mchakato utakaofanywa na vyama vya siasa.
- Vita vya kagera- hivi havikuwa tu vita bali vilikuwa vinaisimika katiba ya mwaka 1977 ndo maana hata Nyerere mwenyewe aliishia kuiponda katiba lakini hakuweza kuindoa
- Hali ngumu ya uchumi ya kuanzia 1980 mpaka 1984- hii nayo ilikuwa inasimika hii katiba fahamu mabadiliko yadumuyo yamefungwa kwenye ubaya