Uko na chick vision chief, samahani kwa hilo. Unaona usawa wa pua yako tu. Huko vijijini kwenu kuna barabara nzuri za kufanya hayo magari yaweze kupita huko kwa muda wote wa mwaka? Kuna uhakika wa huduma nyinginezo jumuishi za kusaidia huo usafiri kuwa madhubuti na kupunguza mzigo badala ya kuongeza mzigo?
Nguvu kubwa ya manunuzi iko vijijini au mjini? Hizo IST unataka zishuke bei ili zikafanyie nini huko vijijini? Gari zikishuka bei automatically mjini kutajaa misongamano maana ndio kwenye purchasing power kubwa than vijijini. Halafu hizo fuso, pick ups, tractors zina utaratibu wake na kodi rafiki tu.. Usafiri binafsi bado kwa nchi yetu ni anasa. Na ni kwasababu usafiri wa umma haujakaa vizuri namiundombinu nayo sio rafiki sana haijaendelea kiwango chakuridhisha. Ili tupate miundombinu bora na usafiri bora, salama na wa uhakika ni lazima watu walipe kodi tu hakuna namna nyingine. Ndio nashangaa jamaa anakuja na hoja nyepesi hapa eti kodi za magari zishuke ili vijijini wanunue magari. Vijiji gani hivyo ambavyo hata maji ya bomba ni shida, vituo vya afya, barabara na madaraja hakuna.. Umeme etc sasa hao ndio anatetea washushiwe kodi ili wanunue magari.. Kula yenyewe tabu hayo magari wataweka maji humo? Kujua vipaumbele vya nchi ni muhimu. Sio matakwa binafsi ya mtu yanachukuliwa kama ndio mahitaji ya jamii nzima.