Serikali Sasa Irekebishe Ushuru Wa Magari

Serikali Sasa Irekebishe Ushuru Wa Magari

Hivi Mimi sielewi naona kama serikali rais na makamu wake wanapishana

Makamu anataka makusanyo ya tr 2 kwa mwezi lakini hakumbuki makusanyo ya tr 1.5 chini ya hayati magufuli ilivotuhenyesha watanzania pamoja na bidhaa nyingi kupanda bei

makusanyo yalipatikana sio kwa njia halali inawezekana bado hatukuwa na uwezo huo wakukusanya pesa hizo hivyo ata hiyo miradi ya kimkakati hatukupaswa kuifanya
Mpango kitu anachojua ni kuongeza kodi na sio kitu kingine
 
Mtu mwovu hakupenda Watanzania tumiliki magari. Unapopandisha ushuru wa IST kwa milioni mbili, gari ya kimasikini, je unakuwa unamtakia nini mtu wa chini ambaye wewe unawadanganya watu kuwa unawatetea?
Hiii nchi imeharibika sana aisee yan kuireform it takes time kwa kweli
 
Yan ist kuagiza imefika mpk 13m nimechukia sana miaka miwil nikua nakusanya nitembelee matako af unakuta mambo yamepanda ivo
Mim mpango siumkubali uwezo wa kutengeneza mazingira ya kukua kwa tax base Hana, yeye akilala akiamka anamfikiria kuongeza kodi ndo anachojua
 
Hayo ni magari ya nchi nyingine wanaenda kulipa huko
Samahani mkuu, kodi inayolipwa na haya magari ya IT(In Transit) huwa ni kwa ajili ya kutumia bandari yetu au ni pamoja na kutumia barabara zetu mana mengi yanapita yanatembea yenyewe.
 
Nyie nao hoja nyepes sana uko vijijn hakuna watumish tunaojiweza kutaka ist hakuna wakulima hakuna wafanyabiashara ?Yan vijijin hakuna uhitaj wa magar sio
Jumping conclusions

Sijasema vijijini hakuna uhitaji wa magari. Jaribu kuangalia ratio ya vipato kwa watu wa mjini na vijijini ndio utaelewa point ilipo. Kama huko vijijini kuna wafanyakazi na wafanyabiashara wenye uwezo wa kumudu kununua hayo magari ni sahihi kabisa. Wanunue tu maana uwezo wanao.

Ila majority huko vijijini wanahitaji huduma bora kwanza za msingi na miundombinu sahihi. Kuna changamoto nyingi sana za kuzitatua kuliko kuwaza kununua magari. Swala la kupunguza kodi sawa liangaliwe ila sio kutumia kichaka cha wakijijini nao waweze kununua.

Huko mjini ndio kutajazana hayo magari tu. Vibarabara finyu, usafiri wa umma mbovu.. Kila mtu atataka kupanda gari yake, parking finyu mijini humo... Ni kujiongezea changamoto tu.
 
Hayo magari yakipungua Kodi Sana kwa hizo asilimia unazotaka mtaziendeshea kwenye barabara zipi?
Kazi ya kutengeneza barabara ipo kwenye Road License ambayo imeweka kwenye kila Lita unayoinunua kwa matumizi ya gari. Kumbuka pia ipo kodi ya kujenga reli iliyojumuishwa kwenye gari inayoingizwa nchini. Yaani ni utitiri wa kodi kwenda mbele.
 
Hayo magari yakipungua Kodi Sana kwa hizo asilimia unazotaka mtaziendeshea kwenye barabara zipi?
Ulaya,Japan,Asia gari sio issue karibu kila nyumba ina gari tena nyingine zaidi ya gari moja,nenda Muscat tu hapo utajionea,sasa mbona wao wanatumia gari bila shida na kwao gari si ghali?
Tatizo la watanzania wengi ni exposure....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kama ishu ni kodi, watapata kwenye ongezeko la matumizi ya mafuta na vipuri. Pia wenhi wakiagiza kodi inaweza hata isiathirike. Kodi za magari nchi hii ni kandamizi na kijinga.
+1
Road toll yenyewe watapata zaidi kama magari yanaongezeka barabarani , na hii ni kodi ya kila siku kwa maisha yote gari litakapokuwa barabarani,
Nashangaa wanakomalia import duty wakati hata ingekuwa zero rated bado serikali ingekusanya kodi kwa uwepo wa gari hilo barabarani
 
Nilishangaa sana bilionea Laizer alipopata zile bilioni 7 serikali ilichukua kodi ndogo mno,kitu kama milioni mia mbili au tatu ...tu.....
Nikasema kama Laizer angeleta gari la thamani ya bilioni saba basi angetakiwa alipie ushuru bilioni 12 !
Hapo ndio unapoona hii kodi kwa magari ni kukomoana tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Rwanda,Burundi nasikia ushuru wa gari ni chini sana,ndio maana hata magari watu wengi wananunua na kuyapitisha hapa kwetu It

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kama sikosei serikali iliamua kupandisha kodi za magari used, (yaliuotumika) kama njia ya kujikinga kuwa dampo la kutupiwa magari na kipunguza athari za uchafuzi wa hali ya hewa.

Ila kwa magari mapya sijajua, wajuvi wa haya watusaidie hili. Tulielewe.
hii HOJA ni nyepesi mno maana hata wakipandisha hiyo kodi bado watu hawatoweza kumudu kununua gari ambalo halijatumika, na hiyo kodi pia wanayochaji kubwa kiasi hicho inasaidia vipi kukinga uharibifu na uchafuzi wa mazingira wa moja kwa moja kama siyo uonevu tu kwa watu wa kipato cha chini.

Kama magari used yanachafua mazingira basi wayazuie kabisa tujue moja na siyo kugeuza kichochoro cha kukusanya pesa
 
Ushuru upunguzwe kwa ma landcruiser ford ranger na magari mengine ya juu.ila kwa hivi vi passo,ist na vibugs vingine uongezwe maradufu,wanaoendesha hivi vidubwana sijui huwa wanajionaje barabarani,wanaendesha wanavyojisikia wenyewe,mpo highway mtu anaendesha speed 30kmh!!mpaka mtu unaweza kujikuta unafanya overtaking eneo la hatari kwa upuuzi wa kiji IST kimoja.NASEMAA USHURU UONGEZWE[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hehehehe, mzee unaonekana mbabe sana.
 
Akili ya kipumbavu kabisa. Hapa utakuta hata pkpk hauna kenge we.
 
Ulaya,Japan,Asia gari sio issue karibu kila nyumba ina gari tena nyingine zaidi ya gari moja,nenda Muscat tu hapo utajionea,sasa mbona wao wanatumia gari bila shida na kwao gari si ghali?
Tatizo la watanzania wengi ni exposure....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Sasa mkuu kweli kwa hiyo exposure yako ndio unataka ufananishe huku na Japan au Ulaya kwa wingi wa magari? Hivi miundombinu inafanana kweli? Purchasing power inalingana kwa raia wake? Hizo gari wenye vipato wakiongezeka sana na miundombinu ikiwa bora na usafiri wa umma ukiborekaa ndio utaona gari zitashuka bei na zitakosa thamani automatically.

Yani kama mnavyopishana na kukatiza kkoo ndio magari nayo yapite hivyo hivyo! Kuwa serious chief. Lazima miundombinu ijengwa sasa labda mshauri kodi ya magari ipunguzwe ila makusanyo yaelekezwe kwenye kitu kingine. Bila kodi mambo hayawezi kwenda
 
Rwanda,Burundi nasikia ushuru wa gari ni chini sana,ndio maana hata magari watu wengi wananunua na kuyapitisha hapa kwetu It

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hahaha wewe jamaa bhana, kwa hiyo wanapitisha gari zao hapa kwa sababu kwao ushuru ni mdogo? Kwani kwao huko import duty ni asilimia ngapi na uchakavu ni asilimia ngapi ya FOB?

Fanyeni tafiti ya haya mambo kabla ya kukurupuka tu. Kwa hapa E. A ni Tanzania ndio kuna kodi nzuri ya magari. Haswa haya mtumba. Kama ni kubishana njoo na facts hapa sio siasa
 
Wale hawana bandari lazima zipite hapa,ulizia mtu aliyeko Burundi jinsi gani,Uganda jinsi wanavyolipa

Hapa Zanzibar tu ukilipitishia gari kule halafu uululete huku bara lazima wanakubana ulipie tena tofauti ya ushuru

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Uko na chick vision chief, samahani kwa hilo. Unaona usawa wa pua yako tu. Huko vijijini kwenu kuna barabara nzuri za kufanya hayo magari yaweze kupita huko kwa muda wote wa mwaka? Kuna uhakika wa huduma nyinginezo jumuishi za kusaidia huo usafiri kuwa madhubuti na kupunguza mzigo badala ya kuongeza mzigo?

Nguvu kubwa ya manunuzi iko vijijini au mjini? Hizo IST unataka zishuke bei ili zikafanyie nini huko vijijini? Gari zikishuka bei automatically mjini kutajaa misongamano maana ndio kwenye purchasing power kubwa than vijijini. Halafu hizo fuso, pick ups, tractors zina utaratibu wake na kodi rafiki tu.. Usafiri binafsi bado kwa nchi yetu ni anasa. Na ni kwasababu usafiri wa umma haujakaa vizuri namiundombinu nayo sio rafiki sana haijaendelea kiwango chakuridhisha. Ili tupate miundombinu bora na usafiri bora, salama na wa uhakika ni lazima watu walipe kodi tu hakuna namna nyingine. Ndio nashangaa jamaa anakuja na hoja nyepesi hapa eti kodi za magari zishuke ili vijijini wanunue magari. Vijiji gani hivyo ambavyo hata maji ya bomba ni shida, vituo vya afya, barabara na madaraja hakuna.. Umeme etc sasa hao ndio anatetea washushiwe kodi ili wanunue magari.. Kula yenyewe tabu hayo magari wataweka maji humo? Kujua vipaumbele vya nchi ni muhimu. Sio matakwa binafsi ya mtu yanachukuliwa kama ndio mahitaji ya jamii nzima.
Kichwa chako ni kufugia nywele tu hakina kazi nyimgine inaonekana, kwani hayo magari yananunuliwa na serikali au mwanachi eti kisa kijijini watu wanashida ndo kupandisha kodi za magari we jamaa nenda haraka milembe ufungue file
Unashindwa kuelewa watu wakiagiza magari wengi ndo serikali itapata kodi hata ya kutengeneza miundo mbinu ambayo unasema haipo ,angalia nchi za jirani ambao tuna uchumi tunaokaribiana nao wanatax vipi magari
Haiingii akilini Japan watengeneze magari kwa malighafi zao technologia zao, viwanda vyao alafu waamue kuuza magari yao kwa Tanzania kodi izidi hadi bei ya gari lenyewe. Imagine eti Railway levy unaagiza gari kwani limapita kwenye mataruma??
 
Back
Top Bottom