Serikali Rasmisha KAZI za wajasariamali wote KWA kugawa vitambulisho kama zamani Ili mkusanye mapato Mengi zaidi KWA mwaka.

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Sep 10, 2022
1,282
2,508
Tozo pekee sio suluhisho la uchumi wetu .

Rudisha vitambulisho KWA wajasiria mali,vitambulisho viwe na gredi kutokana na mtaji wa muhusika,yaani ;-


Gredi A

Wajasiria mali wenye mitaji ya kuanzia milion 100 na kuendelea hao walipe hata laki tatu KWA mwaka!TRA watamuandalia kanuni mpya ya kodi punguzo Baada ya kulipia kitambulisho cha "Rasmisha KAZI yako jenga uchumi wa nchi"

Mnaweza kuboresha hapo ikakaa vizuri zaidi KWA maslahi mapana ya serikali na mjasiria mali!
Upelelezi wa kina kuhusu historia ya transaction ya mjasiria mali itatumika ku gredi kitambulisho chake.

Gredi B

Wenye mitaji ya milion 50 hadi 100,Hawa walipe walau laki Mbili KWA mwaka kurasmisha kazi yao,ufuatiliaji wa kina kuhusu transaction zao utumike kurasmisha KAZI zao!

Gredi c

Hawa wenye mitaji milion 50 Hadi 10 milion Hawa watalipa kama laki moia na nusu KILA mwaka na vitambulisho hivi vitaandikwa majina take matatu,mwaka husika Ili asikwepe Mwakani KWA kuwa na kitambulisho kile kile!

Gredi D

Wenye mitaji ya sh milion 10 Hadi Milion5 walipie laki Moja kama KILA mwaka!

Gredi E

Wenye mitaji kuanzia milion 5 hadi milion 1 hao walipe 50,000 KWA mwaka TRA wataandaa kanuni kuwa favor kutokana na mitaji yao Ili wapate punguzo la kodi lisiwe kubwa Baada ya kulipia kitambulisho cha "Rasmisha kazi yako jenga nchi yako"

Gredi F

Wenye mitaji ya laki Tisa Hadi Laki tano hao walipe sh 30000/= KWA mwaka kodi wapunguziwe katika kanuni za TRA Ili kuutambua mchango wao wa kurasmisha KAZI zao na kujenga nchi yao!

Gredi G

Kuanzia laki Moja Hadi Laki nne walipe 20000/=
Kodi wapunguziwe kutokana na mchango wao!

Gredi H

Wenye mitaji ya chini ya laki Moja Hadi 20000/= hao walipe 5000/= hao wasilipe kodi kabisa TRA walee mitaji yao Hadi wakue!!

Mnaweza boresha zaidi KWA wachoma mkaa,Mama ntilie,machinga,wenye nyumba za kupangisha na mengineyo!

Mtakusanya fedha NYINGI ZAIDI kuliko Tozo pekee,itafikia hatua mtaona Tozo HAINA maana tena kwani fedha za kurasmisha KAZI na punguzo la kodi zinatosha zaidi kuliko Tozo!

Jinsi ya utelezaji


TRA ianze ku gredi mitaji ya watu kutokana na data base yao,KWA wale ambao hawapo chini ya mfumo wa TRA mabalozi,watendaji vijiji watatumika kuwatambua KAZI zao wanazo fanya Ili wapatiwe vitambulisho vyao.

TRA wanapoanza kufuatilia kodi hatua ya kwanza ni kumuuliza mhusika kuonyesha kitambulisho cha "Rasmisha KAZI yako jenga nchi yako" kabla ya yote !kama hana hatua za kinidhamu zinafuatwa!kukamatwa na kulipa faini na kupigiwa kanuni za kawaida za juu,ikiwezekana wasio na vitambulisho wajulikane kama wahujumu uchumi na kesi zao ziwe kufilisiwa mali zao kufidia MAPATO waliyoyakwepa!!!

Kaeni ,mfikirie muone kama inafaa ikifaa fanyieni KAZI!
KWA mawasiliano zaidi kuboresha mfumo huu,wadau mni pm Ili kuona Namna bora ya kuwezesha hilo!


Mungu ibariki TANZANIA
 
Neno sahihi ni 'wajasiri amali' na siyo wajasiria mali

"Jasiri"
"Amali"

Mjasiri-amali
Wajasiri-amali
Ujasiri-amali

Ingawaje linakosewa sana neno hili kuandikwa na watu wengi.


Lakini una 'point' kwenda mada
 
Mtaji wa mil. 100 alipe tozo/kodi ya laki tatu?! Halitekelezeki hilo.
 
Back
Top Bottom