Serikali ni chanzo cha masomo ya ziada kwa watoto

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,602
Shule zinashindana kwenye ufaulu wa watoto kwa kushirikiana na wazazi wa watoto. Wanafanya hivyo kwa mbinu tofauti ikiwemo ya watoto kusoma masaa mengi hata weekend na long vacation, kuwakaririsha maswali ya mitihani na hata kuiiba mitihani yenyewe.

Serikali Ina mchango mkubwa sana kwenye hili sakata kutokana na yafuatayo:

1. Serikali kutenga shule za wenye ufaulu mzuri na zisizo za ufaulu. Hivyo kila mzazi ataka mwanawe aende kwenye hizo shule pambe.

2. Idadi kubwa mno ya wanafunzi madarasani wwsiofundishika kwa muda wa kawaida.

3. Upungufu wa walimu na miundombinu kama madarasa na madawati na vitabu.

4. Mishahara midogo ya walimu, walimu wanalazimika kufundisha tuition kupata nauli, Kodi ya nyumba, maji, umeme, ada ya watoto wao na kufidia makato makubwa ya mikopo ya benki. Walimu wanakopa sana jamani.

5. Shule na walimu wenye ufaulu mdogo kubezwa na serikali na kupewa adhabu.

6. Upungufu wa vyuo vya serikali na ada kubwa vyuo binafsi. Hii inasababisha wenye ufaulu mkubwa tu wachukuliwe vyuo vya serikali vyenye ada ndogo na wenye ufaulu mdogo kuambulia vyuo binafsi vyenye ada kubwa.

7. Shule nzuri za private kuchukua watoto wenye ufaulu mkubwa TU. Ili kuchaguliwa kwenye shule binafsi nzuri mwanao lazima apite mtihani wa kujiunga.

8. Mikopo ilikuwa kwa wanafunzi wenye ufaulu mkubwa tu.

Haya yanasababisha walimu na wazazi wakubaliane kuwatesa watoto kwa kusoma muda mrefu sana kinyume na kanuni za kufundisha na kujifunza zinavyotaka.

Serikali isitenge shule zake kwa misingi ya ufaulu mzuri na hafifu. Badala yake kuwe na madarasa/streams A, B, C, D, E,..... ndani ya kila shule kutokana na ufaulu. Mfano stream A wapande wenye ufaulu mkubwa
 
Back
Top Bottom