Habari!
Nitatoa mifano angalau 3 kuthibitisha hoja katika title ya Uzi wangu.
Mfano # 1
Diwani analipwa pesa ndogo, ilikuwa chini ya laki 4 labda kama mabadiliko yafanyike majuzi.
Huyo diwani anazidiwa mshahara na watumishi karibu wote katika kata yake. Atakuwa na uzalendo kweli?
Huyo diwani ndiye wananchi wanamwona mkombozi wao, akiingia mitaani wananchi wenye maisha magumu wananza kumlilia shida.
Mfano # 2
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa /kijiji analipwa posho ya sh 50000.
Huyu mwenyekiti ndiye yuko kwenye kamati ya maendeleo ya mtaa au kijiji.
Zamani nasikia miaka ya 70 walikuwa wanalipwa pesa ambayo inatosha kununua mahitaji muhimu yote ya familia. Sasa 50000 si kiroba Cha unga na dagaa kilo 2 tu biashara imeisha.
Mfano #3
Watumishi wanaolipwa kima cha chini kama wahudumu wa ofisi, walinzi, wapishi n.k
Hivi 370000 ukiikata NHIF, kodi na 5% ya mfuko wa uhifadhi kinabaki nini?
Huyu mtumishi anatumwa akalitafute file la mteja. Hatajifanya yuko bize au halioni ili apewe ya maziwa?