Serikali ndiyo inayowafundisha watumishi wake kula rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,480
35,372
Habari,

Nitatoa mifano angalau 3 kuthibitisha hoja katika title ya uzi wangu.

Mfano # 1
Diwani analipwa pesa ndogo, ilikuwa chini ya laki 4 labda kama mabadiliko yamefanyika majuzi. Huyo diwani anazidiwa mshahara na watumishi karibu wote katika kata yake, atakuwa na uzalendo kweli? Huyo diwani ndiye wananchi wanamwona mkombozi wao, akiingia mitaani wananchi wenye maisha magumu wananza kumlilia shida.

Mfano # 2
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa/kijiji analipwa posho ya sh 50,000/-. Huyu mwenyekiti ndiye yuko kwenye kamati ya maendeleo ya mtaa au kijiji. Zamani nasikia miaka ya 70 walikuwa wanalipwa pesa ambayo inatosha kununua mahitaji muhimu yote ya familia lakini sasa 50,000/- si kiroba Cha unga na dagaa kilo 2 tu biashara imeisha?!

Mfano #3
Watumishi wanaolipwa kima cha chini kama wahudumu wa ofisi, walinzi, wapishi n.k. Hivi 370,000/- ukiikata NHIF, kodi na 5% ya mfuko wa uhifadhi kinabaki nini? Huyu mtumishi anatumwa akalitafute file la mteja. Hatajifanya yuko bize au halioni ili apewe ya maziwa?​
 
Ingekua pesa ndio inapunguza rushwa basi hakuna waziri au kiongozi mkubwa angechukua rushwa.

Kadri pesa inavyopanda na ndio hamasa ya rushwa kubwa inapoongezeka
 
Habari!

Nitatoa mifano angalau 3 kuthibitisha hoja katika title ya Uzi wangu.

Mfano # 1
Diwani analipwa pesa ndogo, ilikuwa chini ya laki 4 labda kama mabadiliko yafanyike majuzi.

Huyo diwani anazidiwa mshahara na watumishi karibu wote katika kata yake. Atakuwa na uzalendo kweli?

Huyo diwani ndiye wananchi wanamwona mkombozi wao, akiingia mitaani wananchi wenye maisha magumu wananza kumlilia shida.

Mfano # 2
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa /kijiji analipwa posho ya sh 50000.

Huyu mwenyekiti ndiye yuko kwenye kamati ya maendeleo ya mtaa au kijiji.

Zamani nasikia miaka ya 70 walikuwa wanalipwa pesa ambayo inatosha kununua mahitaji muhimu yote ya familia. Sasa 50000 si kiroba Cha unga na dagaa kilo 2 tu biashara imeisha.

Mfano #3
Watumishi wanaolipwa kima cha chini kama wahudumu wa ofisi, walinzi, wapishi n.k
Hivi 370000 ukiikata NHIF, kodi na 5% ya mfuko wa uhifadhi kinabaki nini?

Huyu mtumishi anatumwa akalitafute file la mteja. Hatajifanya yuko bize au halioni ili apewe ya maziwa?
Upo sahihi kabisa,

Ndio maana diwani wetu hapa ameamua kabisa kwa makusudi ikifika jioni tu barabara zote za ndanda na Muheza kupitia Narun'gombe, Masasi na Aggrey na Magila zinafungwa na malori yanachukua nafasi kupakia mizigo utafikiri tupo bandarini,

Sawa kabisa kila mtu ale ofisini kwake
 
Chama chenyewe kimejaa wezi unategemea wafuasi wake waweje mkuu?

Kama mkuu wa nchi anaongea bila aibu kabisa kwamba "watu wale kwa urefu wa kamba"unategemea nini hapo?
 
Kwanza naomba nikwambie kuwa na mshahara mkubwa au mdogo Hakuna uhusiano na kupokea Rushwa, Ndio maana unaona Kuna watu Wana mamishahara makubwa lakini unawakuta kwenye skendo za Rushwa,

Pili, Serikali ya mh Rais mama Samia suluhu Hassani inaendelea kufanya jitihada za kuboresha maslahi ya watumishi wa umma hasa wa kipato Cha chini Kama ilivyo fanya majuzi kwa kuwaongezea 23% ili kuendana na Hali ya maisha ya wakati huu

Pia kwa wenyeviti nako Kuna jitihada zinafanyika ambako wao wanalipwa kutokanaa na uwezo wa halmashauri kimapato,

Vivyo hivyo kwa madiwani serikali inaendelea kuboresha maisha yao, majuzi tu iliwaongezea kiasi Kama motisha kwa kutambua ukubwa na umuhimu wao ,kwani wao ndio wasimamizi wa pesa za serikali zinazokwenda halmashauri,

Kikubwa Tuwe wazalendo kwa wale wanaokuwa wameaminiwa katika nafasi fulani, sisi vijana huku mitaani tunawategemea ili mtutumikie na kutusaidia
 
Bila Rushwa unadhani nchi hii kuna kitu hakitakufa, Mashule, Hotel, Mabar, Magari na chain yake yote
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom