Serikali na mikakati ya kuwezesha wasomi kuajiriwa, vingenevyo tunakoelekea elimu itakosa thamani hapa Tanzania

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kukwama kwenye sekta ya ajira kamekuja katabia ka watu kuwabeza wasomi waliorundikana mitaani kwa kukosa ajira, kwamba wameshindwa kutumia elimu waliyoipata ama kujiajiri au kuwa wabunifu ili waweze kujikwamua.

Kiuharisia suala la msomi kujiajiri baada ya kuhitimu masomo huwa linapewa second chance kwa wasomi wengi kutokana na Hali halisi, mojawapo ikiwa ni upatikanaji wa mtaji hasa kwa mtu aliyetoka chuo na alikuwa akisoma kwa msaada HESLB.

Lakini pia tuongee katika uhalisia, mtu ametumia miaka 17 Hadi 20 shuleni Mpaka kupata shahada yake ya kwanza na baada ya kuhitimu masomo yake anapoingia mtaani anaambiwa ajira hakuna inabidi ajiajiri kuuza nyanya, mboga mboga, matunda, mitumba, dereva bajaji, bodaboda, kuchimba mitaro, n.k.

Hizi Ni kazi ambazo zinaweza kufanywa na mtu yeyote na Wala hazihitaji degree Wala dipoloma. Kama tunatamani watu wajiajiri Ni Bora ikiaanzishwa kampeni ya kuwashauri watu wasitumie muda mwingi kukaa shuleni ilihali akimaliza miaka 12 shuleni atarudi kufanya kazi ileile ambayo anaifanya yule waliyemaliza wote shule ya msingi miaka 10 au 12 iliyopita na Tena huyu wa darasa la 7 ndo atamfundisha kazi graduate maana yeye tayari ana uzoefu wa kazi kwa miaka mingi.

Point yangu Ni kwamba, tunakolekea hamasa ya watu kusoma au kusomesha watoto hasa elimu za juu itapungua kwa kasi Kwani watu hawaoni umhimu wa kutumia muda mwingi shule harafu baadae urudi mtaani kuwa boda boda tena baada ya miaka 10 wakati hiyo kazi angeweza kuianza pindi anapomaliza darasa la Saba.

Tutengeneze mazingira ya wasomi kuajiriwa ili kuipa thamani elimu hapa nchini.
 
Awamu iliyoshindwa.
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.

So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.

Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.

Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.

Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili. Chagua ccm chagua maendeleo chagua mitano tena ikiisha mitano tena jiandae kwa kumi tena.
 
Kusomeshwa watu namba lengo kuu lilikuwa ni kuliongeza zaidi tatizo la ukosefu wa ajira nchin
 
Tatizo watu wengi Hawjui kuwa kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwa kingereza ni investing in yourself

Unatakiwa kujiuliza hiki ninschosoma au ku invest in myself kina soko na future? Ili gharama nilizotumia kwenye hii investment irudI?

Wengi wanasoma ili mradi ajaze mivyeti tu

Sasa ukijua ulikosea investment yako kwa kusomea litakataka lisilo na ajira unafanyaje? Unaangalia ufanye kingine nini iwe kuuza genge nk au urudi kusoma usomee kingine chenye soko

Ukigundua ulikosea usikae tu unabweka ohh ajira hamna utakufa njaa kubali uliinvest vibaya muda na pesa za kusomea reinvest eneo lingine chap chap tafuta hata kibarua cha kumwaga nzege au konda wa daladala au dereva wa Lori nk
 
Point yangu Ni kwamba, tunakolekea hamasa ya watu kusoma au kusomesha watoto hasa elimu za juu itapungua kwa kasi Kwani watu hawaoni umhimu wa kutumia muda mwingi shule harafu baadae urudi mtaani kuwa boda boda tena baada ya miaka 10 wakati hiyo kazi angeweza kuianza pindi anapomaliza darasa la Saba.
Tutengeneze mazingira ya wasomi kuajiriwa ili kuipa thamani elimu hapa nchini.
Kwa kiasi fulani una point lakini kusoma ni kuelimika,japo hili halisemwi na hatulisikii mara nyingi masikioni.
Ni sawa na watoto wa shule nyingi za msingi na sekondari,wanapofundishwa namna ya kujibu mitihani ili wafauru
kwa mtizamo wangu hali hii haimsaidii mwanafunzi kwani hata akishafaulu mtihani anajikuta bado mjinga
maana kwenda shule lengo ni kuelimika na siyo kufaulu.

Tatizo ninaloliona katika vyuo vyetu vingi ni wakufunzi, hawatoi elimu ya viwango,unamkuta mwalimu anakufundisha
kwa kuonyesha ugumu wa elimu,badala ya kuirahisisha ili uelewe anachokufundisha.Ni jambo la kawaida mwalimu kuingia darasani
akasema watu hawa ni wengi inabidi wapungue,na misemo mingi ya namna hiyo inayoongeza woga kwa wanafunzi.

Kwa waliobahatika kufundishwa na waalimu wa mataifa ya ulaya,urusi,marekani n.k. wataelewa ninachokisema,usipomuelewa mwalimu unamuona akiumia moyoni ni kwa nini huelewi,kitu ambacho sijakiona kwa waalimu wengi wa kwetu hapa,Hali hii umewafanya wanavyuo kukimbizana na kufaulu badala ya kuelimika.

chukua mfano mdogo wa kutoelimika: fani unayosemea mfano: kama wewe ni injinia wa umeme,je una uwezo wa kutatua matatizo ya umeme nyumbani kwenu? Nimeshuhudia wengi wakisema hii ni kazi ya mtaani tafuteni kishoka,kwa nini,kwa sababu ulisoma kufaulu umeme na siyo kufanya kazi ya umeme.

Ninayasema haya kwa ujasiri ili tuangalie tulipojikwaa na siyo tulipoangukia.

Nini kifanyike:
* Wakufunzi wa vyuo,wafundishe wanavyuo,wahakikishe wameiva na siyo kuwaonyesha ugumu wa elimu wanazosomea
hapa namaanisha waondoe vitisho wajikite kuwanoa watu waive kitaaluma.
  • Wasomi ,mnapoenda mafunzo ya vitendo(field) acheni usharobaro,huko ndo tulijifunzia kazi,acheni kudanganyana kwamba injinia hatakiwi kuchafuka,hiyo ilikuwa zamani kabla mainjinia hawajawa wengi enzi za mwalimu ambapo walikuwa watawala.
  • Tujenge moyo wa kujitolea kwenye taasisi zinazotoa huduma tulizosomea,hapa wazazi wajitoleekuendelea kuwapa watoto wao
nauli za kwenda kujitolea,nimeshuhudia watu wakiajiliwa kupitia mfumo huo japokuwa unatakiwa ujitume hasa ili mwajili aone umuhimu wako.
 
Elimu katika Dunia ya leo si kwa ajili ya kuajiriwa bali ni kupanua uelewa wako katika kupambana na mazingira yako.
Fanya utafiti wako vizuri, Dreva Bajaji mwenye degree ana tofauti kubwa sana na Dreva Bajaji wa darasa la saba.
 
mi wavyo sema mkajiajili.huwa naelewa kwamba wanamanisha tukajiajili kupitia elimu tuliyo ipata shuleni.na siyo kwenda kufanya kitu kingine tofauti na carie yakk
 
Tatizo watu wengi Hawjui kuwa kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwa kingereza ni investing in yourself

Unatakiwa kujiuliza hiki ninschosoma au ku invest in myself kina soko na future? Ili gharama nilizotumia kwenye hii investment irudI?

Wengi wanasoma ili mradi ajaze mivyeti tu

Sasa ukijua ulikosea investment yako kwa kusomea litakataka lisilo na ajira unafanyaje? Unaangalia ufanye kingine nini iwe kuuza genge nk au urudi kusoma usomee kingine chenye soko

Ukigundua ulikosea usikae tu unabweka ohh ajira hamna utakufa njaa kubali uliinvest vibaya muda na pesa za kusomea reinvest eneo lingine chap chap tafuta hata kibarua cha kumwaga nzege au konda wa daladala au dereva wa Lori nk
Ndugu tukubali tu Serikali ya awamu hii inawajibika kwa kila kitu kuhusu ajira. Mfano Ni sekta ya afya na ualimu. Hawa Hizi ndo sekta pekee ambazo upatikanaji wa ajira ilikuwa Ni uhakika 100% Sasa na zenyewe imekuwa shida na wote Hawa nao wamerundikana mtaani. Watu wasome Nini Sasa ili wajiweke ktk mazingira mazuri ya kuajiriwa.
 
Elimu katika Dunia ya leo si kwa ajili ya kuajiriwa bali ni kupanua uelewa wako katika kupambana na mazingira yako.
Fanya utafiti wako vizuri, Dreva Bajaji mwenye degree ana tofauti kubwa sana na Dreva Bajaji wa darasa la saba.
Tofauti gan unamaanisha mkuu mbayo Ina tija ya kumshawishi abiria amuongezee kipato au nauli dereva. Abiria anaposimamisha daladala au bajaji mjini Hana MDA wa kuchunguza kwamba hii daladala au bajaji Ni ya mtu wa degree au darasa la Saba😀😀😀😀😀
 
Baada ya Serikali ya awamu ya tano kukwama kwenye sekta ya ajira kamekuja katabia ka watu kuwabeza wasomi waliorundikana mitaani kwa kukosa ajira, kwamba wameshindwa kutumia elimu waliyoipata ama kujiajiri au kuwa wabunifu ili waweze kujikwamua.
Kiuharisia suala la msomi kujiajiri baada ya kuhitimu masomo huwa linapewa second chance kwa wasomi wengi kutokana na Hali halisi, mojawapo ikiwa ni upatikanaji wa mtaji hasa kwa mtu aliyetoka chuo na alikuwa akisoma kwa msaada HESLB.

Lakini pia tuongee katika uhalisia, mtu ametumia miaka 17 Hadi 20 shuleni Mpaka kupata shahada yake ya kwanza na baada ya kuhitimu masomo yake anapoingia mtaani anaambiwa ajira hakuna inabidi ajiajiri kuuza nyanya, mboga mboga, matunda, mitumba, dereva bajaji, bodaboda, kuchimba mitaro, n.k.

Hizi Ni kazi ambazo zinaweza kufanywa na mtu yeyote na Wala hazihitaji degree Wala dipoloma. Kama tunatamani watu wajiajiri Ni Bora ikiaanzishwa kampeni ya kuwashauri watu wasitumie muda mwingi kukaa shuleni ilihali akimaliza miaka 12 shuleni atarudi kufanya kazi ileile ambayo anaifanya yule waliyemaliza wote shule ya msingi miaka 10 au 12 iliyopita na Tena huyu wa darasa la 7 ndo atamfundisha kazi graduate maana yeye tayari ana uzoefu wa kazi kwa miaka mingi.

Point yangu Ni kwamba, tunakolekea hamasa ya watu kusoma au kusomesha watoto hasa elimu za juu itapungua kwa kasi Kwani watu hawaoni umhimu wa kutumia muda mwingi shule harafu baadae urudi mtaani kuwa boda boda tena baada ya miaka 10 wakati hiyo kazi angeweza kuianza pindi anapomaliza darasa la Saba.
Tutengeneze mazingira ya wasomi kuajiriwa ili kuipa thamani elimu hapa nchini.
Hii ni serikali ya wanyonge ina wanyonga haswa
 
Kwa kiasi fulani una point lakini kusoma ni kuelimika,japo hili halisemwi na hatulisikii mara nyingi masikioni.
Ni sawa na watoto wa shule nyingi za msingi na sekondari,wanapofundishwa namna ya kujibu mitihani ili wafauru
kwa mtizamo wangu hali hii haimsaidii mwanafunzi kwani hata akishafaulu mtihani anajikuta bado mjinga
maana kwenda shule lengo ni kuelimika na siyo kufaulu.
Tatizo ninaloliona katika vyuo vyetu vingi ni wakufunzi,hawatoi elimu ya viwango,unamkuta mwalimu anakufundisha
kwa kuonyesha ugumu wa elimu,badala ya kuirahisisha ili uelewe anachokufundisha.Ni jambo la kawaida mwalimu kuingia darasani
akasema watu hawa ni wengi inabidi wapungue,na misemo mingi ya namna hiyo inayoongeza woga kwa wanafunzi.

Kwa waliobahatika kufundishwa na waalimu wa mataifa ya ulaya,urusi,marekani n.k
wataelewa ninachokisema,usipomuelewa mwalimu unamuona akiumia moyoni ni kwa nini huelewi,kitu ambacho sijakiona kwa waalimu wengi
wa kwetu hapa,Hali hii umewafanya wanavyuo kukimbizana na kufaulu badala ya kuelimika.
chukua mfano mdogo wa kutoelimika: fani unayosemea mfano: kama wewe ni injinia wa umeme,je una uwezo wa kutatua matatizo ya umeme nyumbani kwenu? Nimeshuhudia wengi wakisema hii ni kazi ya mtaani tafuteni kishoka,kwa nini,kwa sababu ulisoma kufaulu umeme na siyo kufanya kazi ya umeme.
Ninayasema haya kwa ujasiri ili tuangalie tulipojikwaa na siyo tulipoangukia.

Nini kifanyike:
* Wakufunzi wa vyuo,wafundishe wanavyuo,wahakikishe wameiva na siyo kuwaonyesha ugumu wa elimu wanazosomea
hapa namaanisha waondoe vitisho wajikite kuwanoa watu waive kitaaluma.
  • Wasomi ,mnapoenda mafunzo ya vitendo(field) acheni usharobaro,huko ndo tulijifunzia kazi,acheni kudanganyana kwamba injinia hatakiwi kuchafuka,hiyo ilikuwa zamani kabla mainjinia hawajawa wengi enzi za mwalimu ambapo walikuwa watawala.
  • Tujenge moyo wa kujitolea kwenye taasisi zinazotoa huduma tulizosomea,hapa wazazi wajitoleekuendelea kuwapa watoto wao
nauli za kwenda kujitolea,nimeshuhudia watu wakiajiliwa kupitia mfumo huo japokuwa unatakiwa ujitume hasa ili mwajili aone umuhimu wako.

yess

yaani kwa sasa kielelezo cha mtu kuwa na elimu ni awe amefaulu mitihani na kupewa cheti.

hili jambo limegeuzwa.nia ya walioanzisha ilikuwa kupima uelewa wa yale waliyokuwa wanafundisha.lakini tumefanya iwe hatma na kielelezo pekee kwamba huyu mtu ameelimika kweli kweli.

ndio maana wanafunzi mpaka wanamaliza vyuo hawajui hata nini lengo la yeye kufika alipo,anawaza ajira tu.
 
Elimu katika Dunia ya leo si kwa ajili ya kuajiriwa bali ni kupanua uelewa wako katika kupambana na mazingira yako.
Fanya utafiti wako vizuri, Dreva Bajaji mwenye degree ana tofauti kubwa sana na Dreva Bajaji wa darasa la saba.
Utofauti wa kuendesha bajaj au kufanya nini
 
Na mikopo yao ya Helsb hailipiki maana watu hawaajariwa dogo naona naona imeshuti mpk 18 wkt alisoma biashara.
 
Tatizo watu wengi Hawjui kuwa kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwa kingereza ni investing in yourself

Unatakiwa kujiuliza hiki ninschosoma au ku invest in myself kina soko na future? Ili gharama nilizotumia kwenye hii investment irudI?

Wengi wanasoma ili mradi ajaze mivyeti tu

Sasa ukijua ulikosea investment yako kwa kusomea litakataka lisilo na ajira unafanyaje? Unaangalia ufanye kingine nini iwe kuuza genge nk au urudi kusoma usomee kingine chenye soko

Ukigundua ulikosea usikae tu unabweka ohh ajira hamna utakufa njaa kubali uliinvest vibaya muda na pesa za kusomea reinvest eneo lingine chap chap tafuta hata kibarua cha kumwaga nzege au konda wa daladala au dereva wa Lori nk
Vile viwanda 100@mkoa vya Tanzania ya viwanda viko wapi ili vijana wapate ajira? Au ni hizi propaganda mfu za awamu ya 5?
 
Tatizo watu wengi Hawjui kuwa kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwa kingereza ni investing in yourself

Unatakiwa kujiuliza hiki ninschosoma au ku invest in myself kina soko na future? Ili gharama nilizotumia kwenye hii investment irudI?

Wengi wanasoma ili mradi ajaze mivyeti tu

Sasa ukijua ulikosea investment yako kwa kusomea litakataka lisilo na ajira unafanyaje? Unaangalia ufanye kingine nini iwe kuuza genge nk au urudi kusoma usomee kingine chenye soko

Ukigundua ulikosea usikae tu unabweka ohh ajira hamna utakufa njaa kubali uliinvest vibaya muda na pesa za kusomea reinvest eneo lingine chap chap tafuta hata kibarua cha kumwaga nzege au konda wa daladala au dereva wa Lori nk

mkuu kitu gani ukisoma bongo kina soko ? mkuu usiwabeze wasio na kazi madogo wanasota mkuu
 
Sio ktk malengo yake elimu ya darasani/vyuoni kukujenga wewe ujiajiri. Na hili si kwa mfumo wa elimu wa Tz pekee bali ni mifumo ya elimu za madarasani kote duniani hadi huko US.

Lengo la elimu za darasani ni kutoa waajiriwa (watumishi) bora, wenye uwezo wa kufata miongozo na kanuni za waajiri wao.

Ukitaka elimu ya kujiajiri soma vitabu vya watu waliojiajiri/wafanyabiasha, waulize wamefanyaje ili nawe ujifunze kwao.
 
Awamu iliyoshindwa.
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili. Chagua ccm chagua maendeleo chagua mitano tena ikiisha mitano tena jiandae kwa kumi tena.
Hii comment inabidi iongezwe kama ubeti katika wimbo wa taifa ili watoto na kizazi kijacho waukute na wajue kuwa kulikuwa na babu zao tulikuwa tunawapigania na tulikuwa na akili nyingi sana ila tu kuna wapuuzi wachache walikuwa wanatulazimisha kufuata upuuzi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watu wengi Hawjui kuwa kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine kwa kingereza ni investing in yourself

Unatakiwa kujiuliza hiki ninschosoma au ku invest in myself kina soko na future? Ili gharama nilizotumia kwenye hii investment irudI?

Wengi wanasoma ili mradi ajaze mivyeti tu

Sasa ukijua ulikosea investment yako kwa kusomea litakataka lisilo na ajira unafanyaje? Unaangalia ufanye kingine nini iwe kuuza genge nk au urudi kusoma usomee kingine chenye soko

Ukigundua ulikosea usikae tu unabweka ohh ajira hamna utakufa njaa kubali uliinvest vibaya muda na pesa za kusomea reinvest eneo lingine chap chap tafuta hata kibarua cha kumwaga nzege au konda wa daladala au dereva wa Lori nk
Kwa maneno mengine ni kwamba unasema kinachotokea sasa cha ukosefu wa ajira sio kosa la serikali hata kidogo ni sisi wasomi ndio tunazembea sio?! Au nimekuelewa vibaya mkuu?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom