Baada ya Serikali ya awamu ya tano kukwama kwenye sekta ya ajira kamekuja katabia ka watu kuwabeza wasomi waliorundikana mitaani kwa kukosa ajira, kwamba wameshindwa kutumia elimu waliyoipata ama kujiajiri au kuwa wabunifu ili waweze kujikwamua.
Kiuharisia suala la msomi kujiajiri baada ya kuhitimu masomo huwa linapewa second chance kwa wasomi wengi kutokana na Hali halisi, mojawapo ikiwa ni upatikanaji wa mtaji hasa kwa mtu aliyetoka chuo na alikuwa akisoma kwa msaada HESLB.
Lakini pia tuongee katika uhalisia, mtu ametumia miaka 17 Hadi 20 shuleni Mpaka kupata shahada yake ya kwanza na baada ya kuhitimu masomo yake anapoingia mtaani anaambiwa ajira hakuna inabidi ajiajiri kuuza nyanya, mboga mboga, matunda, mitumba, dereva bajaji, bodaboda, kuchimba mitaro, n.k.
Hizi Ni kazi ambazo zinaweza kufanywa na mtu yeyote na Wala hazihitaji degree Wala dipoloma. Kama tunatamani watu wajiajiri Ni Bora ikiaanzishwa kampeni ya kuwashauri watu wasitumie muda mwingi kukaa shuleni ilihali akimaliza miaka 12 shuleni atarudi kufanya kazi ileile ambayo anaifanya yule waliyemaliza wote shule ya msingi miaka 10 au 12 iliyopita na Tena huyu wa darasa la 7 ndo atamfundisha kazi graduate maana yeye tayari ana uzoefu wa kazi kwa miaka mingi.
Point yangu Ni kwamba, tunakolekea hamasa ya watu kusoma au kusomesha watoto hasa elimu za juu itapungua kwa kasi Kwani watu hawaoni umhimu wa kutumia muda mwingi shule harafu baadae urudi mtaani kuwa boda boda tena baada ya miaka 10 wakati hiyo kazi angeweza kuianza pindi anapomaliza darasa la Saba.
Tutengeneze mazingira ya wasomi kuajiriwa ili kuipa thamani elimu hapa nchini.