DOKEZO Serikali mulikeni kiwanda cha pombe cha Kingdom kilichopo Kalobe Mbeya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu uzi una watu wajinga sana. Hamuoni janga la magonjwa ya figo ,cancer etc. Nyie mnachojali maslahi ya mwenye kiwanda undezi mtupu
 
Whistle blower kama hawa hawazingatiwi ila kina kigogo wa kupost vitu ambavyo havimuathiri mwananchi moja kwa moja wanapewa kipaumbele kwasababu wanapost umbea, na wabongo na umbea ni chupi na tako.
 
Mnaomshambulia mtoa maada mmemuelewa point yake lakini?

Hicho kiwanda kama kingekuwa kinawalipa vizuri wafanyakazi(kulipa vizuri sio mshahara mkubwa maana yake yale makato ya nssf wapewe mkononi) ,Ingekuwa manyanyaso hakuna , kiwanda kingefuata utaratibu sahihi wa uzalishaji, vitendea kazi vingekuwepo

Asingeripoti hayo
 
TRA Tanzania Hiki kiwanda kipo kata ya Kalobe Mbeya mjini. Kiwanda kina waajiriwa wengi na kinauza bidhaa zake sana. Cha ajabu baadhi ya bidhaa hazilipiwi stika ya TRA. Wafanyakazi tunalipiwa mishahara mkononi hamna payee kwa serikali.

-Anakata NSSF kwa wafanyakazi lakini hawasilishi michango.
-Unyanyasaji kwa wafanyakazi.
-Halipi WCF mfanyakazi akiumia kazini ni juu yake.
-Pombe zinatengenezwa kwenye mazingira mabovu( Hamna vitendea kazi kwa wafanyakazi)

Serikali naomba mlimulike hili.
Kwanza kabisa tunakushukuru kwa taarifa hii na kukupongeza kwa kuonyesha uzalendo na kuthamini ulipaji wa kodi.TRA tumechukua taarifa hii kwa uzito wa kipekee na tunaenda fanyia kazi mara moja.Ni kosa kisheria kutowasilisha makato ya kodi katika mshahara na pia kuwa na vileo visivyokuwa na stika za TRA yaani ETS (Electronic Tax Stamp)
 
Back
Top Bottom