Polisi Kilimanjaro wakamata kiwanda cha pombe kali kilichokuwa kinajiendesha bila kusajiliwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata kiwanda cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.

Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara wanatafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.

Hali hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha Pombe kali .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.

Zoezi la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi vikiwa katika wilaya ya Rombo

1.jpg

2.jpg

3.jpg
 
Kwa nini kila inapotawala chadema kuna matatizo makubwa ya ukwepaji kodi na madawa ya kulevya?
 
wanywaji tuwe makini na vinywaji tunywavo........na utakuta bei yake chee,,,,,so vijana mumo humo....gongo imetokomezwa kwa asilimia 60% pande hizo....ila sasa inatengenezwa kitaalamu zaidi....ukiangalia hiyo plant ilivyo inaendana na ule mfumo wa zile plant za kienyeji za gongo....nchi ya viwanda.
 
Ngoma kitoko hiyo na bei yake ni2500 mtu anayumba fresh tu. What's wrong kamanda? Ati kiwanda fake ingekua kiwanda feki kingetengeneza mvinyo boomba?
 
wanywaji tuwe makini na vinywaji tunywavo........na utakuta bei yake chee,,,,,so vijana mumo humo....gongo imetokomezwa kwa asilimia 60% pande hizo....ila sasa inatengenezwa kitaalamu zaidi....ukiangalia hiyo plant ilivyo inaendana na ule mfumo wa zile plant za kienyeji za gongo....nchi ya viwanda.

Kheri wakifungie kabisa! Nawafahamu vijana wawili tumewazika miezi miwili iliyopita kisa "Babylon" "Shing'waa" "Bee"! Hizo spirits haziko produced professionally kuna kiungo kinazidi wao wanafurahia ganzi ya haraka inayowapata kwa kunywa kichupa kimoja lakini madhara yake ni makubwa sana!

Halafu hivi inawezekana kweli spirits kali kiasi hicho zikawa stored poa tu kwenye plastic bottles na kusiwe na any chemical reaction kati ya spirit na plastic?
 
Hawa wanajuana hawa... Hilo mbona bonge la investment.

Wamepishana mahala...
 
urasimu ulioko serikalini na procedures zisizoeleweka ndo chanzo cha yote hayo.
hao wameitikia wito wa tz ya viwanda kwa vitendo. wanapaswa wasaidiwe na siyo kukamatwa.
procedures ni bureaucracy tu, issue ni kuleta hiyo mitambo na kuanza kuzalisha
 
Kheri wakifungie kabisa! Nawafahamu vijana wawili tumewazika miezi miwili iliyopita kisa "Babylon" "Shing'waa" "Bee"! Hizo spirits haziko produced professionally kuna kiungo kinazidi wao wanafurahia ganzi ya haraka inayowapata kwa kunywa kichupa kimoja lakini madhara yake ni makubwa sana!

Halafu hivi inawezekana kweli spirits kali kiasi hicho zikawa stored poa tu kwenye plastic bottles na kusiwe na any chemical reaction kati ya spirit na plastic?
Katika vitu ambavyo vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kutungiwa sheria kali ni utengenezaji na uuzaji wa pombe. Hili eneo watengenezaji wengi wenye viwanda vya hali ya chini kabisa wamelivamia. Matokeo yake wanatengeneza sumu na si pombe.
 
Kwa nini kila inapotawala chadema kuna matatizo makubwa ya ukwepaji kodi na madawa ya kulevya?
Wewe jiandae kujiunga na musiba korokoroni hivi punde! Yaani hujui hata maana ya kutawala na kuongoza! Aibu sana hii. Natamani nijue unaishi mji gani ili nikusaidie kutawaliwa!
 
Jamaa ameinvest vizuri ata mitambo yake ni. Mizuri.. Ilipaswa asaidiwe na si kufilisiwa.. Kiwanda feki maana yake nn..
 
Kheri wakifungie kabisa! Nawafahamu vijana wawili tumewazika miezi miwili iliyopita kisa "Babylon" "Shing'waa" "Bee"! Hizo spirits haziko produced professionally kuna kiungo kinazidi wao wanafurahia ganzi ya haraka inayowapata kwa kunywa kichupa kimoja lakini madhara yake ni makubwa sana!

Halafu hivi inawezekana kweli spirits kali kiasi hicho zikawa stored poa tu kwenye plastic bottles na kusiwe na any chemical reaction kati ya spirit na plastic?
zina madhara kibao.....hakuna maabara pale......ila unafikiria hao polisi hawajui....kuna mahali wamepishana lugha tuu.
 
Back
Top Bottom