Elia Wilinasi: Watanzania kwa Pamoja tutumie nishati safi ya Gesi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Bwana Elia Wilinasi amesema misitu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwakua huhifadhi vyanzo vya maji, kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji madawa, malisho ya mifugo, kuboresha shughuli za kilimo na kuboresha
mandhari ya nchi yetu mijini na vijijini.

Ni kutokana na umuhimu huo wa Misitu ndio maana Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) akapewa jukumu la kusimamia misitu na rasilimali zake kwa niaba ya Serikali Kuu ili iweze kuwanufaisha watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo kupitia matumizi endelevu.

Iko wazi kuwa kuna utegemezi mkubwa wa misitu kama chanzo rahisi na kikuu cha nishati nchini, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika Nchini inatokana na miti. Uvunaji mkubwa wa mkaa umeathiri sana ubora wa misitu. Kuni zinatumika zaidi vijijini na mkaa unatumika zaidi mijini.

Matumizi ya nishati mbadala yanatajwa kama moja ya suluhisho la tatizo hilo, Katika kukabiliana na tatizo la uharibifu wa Misitu Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) inafanya ushirikiano na wadau wa sekta mbalimbali hasa Wizara ya Nishati na madini na jamii kwa ujumla ili kupunguza utegemezi wa misitu kama chanzo kikuu cha nishati.

Matumizi ya nishati mbadala hususani gesi asilia katika matumizi ya kupikia ni rahisi zaidi na ina faida nyingi kuliko matumizi ya mkaa wa miti.

"Kuna siku nilipata kuzungumza na mkazi wa Kata Mwinjuma Wilaya ya Kinondoni, alinieleza yeye na familia yake ya watu watano hutumia nishati ya gesi kupikia na wamegundua faida nyingi za kiuchumi kwakuwa hutumia kiasi kidogo cha fedha katika nishati hiyo kuliko walivyokuwa wakitumia nishati ya mkaa hapo awali" alisema Bwana Elia.

“Nilikuwa natumia karibu 4,000 kila siku kununua mkaa wa reja reja, kwa wiki mbili ilinigharimu shilingi 60,000. Kwa sasa natumia nishati ya gesi kupikia ambapo kwa wiki mbili natumia mtungi wa gesi wa kilo sita ambao kuujaza hunigharimu shilingi 18,000 tu, hiyo ni faida kubwa” alisema mkazi huyo.

"Alisema kwa sasa ameacha kabisa matumizi ya mkaa kwa kuwa hayana faida kiuchumi na athari zake kimazingira ni kubwa ukilinganisha na gesi ambayo matumizi yake ni rahisi na hupika kwa haraka zaidi" aliendelea kusema mkazi huyo.

Bwana Elia amesema tatizo lililopo kwa baadhi ya wananchin ni uoga wa kuingia kwenye matumizi ya gesi wakiamini kuwa nishati hiyo ni ghali zaidi kuliko matumizi ya mkaa ambayo wameyazoea jambo ambalo sio la kweli.

Kwasasa bei ya kununua mtungi na gesi ya kilo 15 ni shiingi 85,000 na bei ya kujaza mtungi mtupu ni shilingi 45,000. Kwa upande wa mtungi wa kilo 6 alisema
unauzwa shilingi 70,000 pamoja na jiko lake na hujazwa kwa shilingi 18,000.

Ukipiga mahesabu ya matumizi ya kawaida, mtungi wa kilo 15 huweza kutosha familia ya watu watano kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kiwango cha mkaa kwa mwezi kwa ukubwa wa familia kama hiyo hata kama wanatumia
kiwango cha chini kabisa cha 2,000 kwa siku, kwa mwezi itakua shilingi 60,000 matumizi ambayo ni ghali zaidi ukilinganisha na bei ya kujaza mtungi wa kilo 15 ambao ni shilingi 45,000 na bado matumizi yake huweza kuzidi mwezi mmoja.

Elia amesema kinachotakiwa ni watanzania kwa pamoja kuacha uoga na kuwa na mtaji kidogo wa kuweza kumiliki mtungi wa gesi na jiko lake kwa wale watakaotumia mitungi mikubwa kuanzia kilo 15 kwenda juu na kuanza mara moja matumizi ya nishati ya gesi ambapo wataona faida zake kiuchumi na kimazingira.
 
Mje Muwaambie WASUKUMA waache kukata kata miti ovyo badala yake watumie gesi.

Wasukuma ni kabila ambalo linakata miti kupita kiasi pia kwao kutumia gesi ni anasa kwa kuwa kuna kuni za bure.

Hawa jamaa hata waliosoma hawajaelimika kabisa.
Ni kweli kama nishati ya gesi ipo haina haja ya kutumia kuni na mkaa.
 
Back
Top Bottom