Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Msemaji wa Serikali, Dkt. Abbasi amewataka wahariri na waandishi nchini kuenzi misingi ya weledi na uzalendo katika kazi zao ikiwemo kufanya utafiti kwanza kuliko "kufakamia" mawazo na maoni ya watu wasioitakia nchi mema.
"Baadhi ya waandishi hawafanyi utafiti wala kutaka kujua mambo kwa kina na huishi wakifakamia tu kila kinachosemwa na mabeberu kupinga maendeleo yetu.
We mwandishi gani sisi ndio Serikali na ndio wenye hela na ndio wenye mradi tunakwambia tunakwenda kujenga mradi Rufiji, anatokea wakala wa mabeberu mmoja kashiba mivyakula ya kwenye kopo huko anakofadhiliwa kuishi anakwambia huo mradi hautajengwa, hawana hela hao, mwandishi unatoka unamwamini wakala wa beberu unaandika na kusambaza uongo, we vipi mbona hatukuelewi na wewe ni wa moto au wa baridi?"
Dkt. Abbasi akisisitiza tangu utekelezaji wa mradi wa Umeme JNHPP Rufiji uanze hakuna malipo ambayo Serikali imechelewesha au kushindwa kuwalipa wakandarasi.
ZanziNews