Serikali: Kuna Wanahabari wanafakamia kila kinachosemwa na mabeberu ili kupinga maendeleo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,533
2,000
Msemaji wa Serikali, Dkt. Abbasi amewataka wahariri na waandishi nchini kuenzi misingi ya weledi na uzalendo katika kazi zao ikiwemo kufanya utafiti kwanza kuliko "kufakamia" mawazo na maoni ya watu wasioitakia nchi mema.

"Baadhi ya waandishi hawafanyi utafiti wala kutaka kujua mambo kwa kina na huishi wakifakamia tu kila kinachosemwa na mabeberu kupinga maendeleo yetu.

We mwandishi gani sisi ndio Serikali na ndio wenye hela na ndio wenye mradi tunakwambia tunakwenda kujenga mradi Rufiji, anatokea wakala wa mabeberu mmoja kashiba mivyakula ya kwenye kopo huko anakofadhiliwa kuishi anakwambia huo mradi hautajengwa, hawana hela hao, mwandishi unatoka unamwamini wakala wa beberu unaandika na kusambaza uongo, we vipi mbona hatukuelewi na wewe ni wa moto au wa baridi?"

Dkt. Abbasi akisisitiza tangu utekelezaji wa mradi wa Umeme JNHPP Rufiji uanze hakuna malipo ambayo Serikali imechelewesha au kushindwa kuwalipa wakandarasi.

ZanziNews
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
30,735
2,000

Serikali ya awamu hii ni waoga wa kupigwa spana kuliko serikali yoyote ile ambayo iliwahi kuwepo hapa Tanzania. Spana ni lazima kwa sababu bila spana hizi serekali za maruhani huwa haziwajibiki!

61551.jpg
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
6,574
2,000
Tunachoangalia ni mpango kazi wa mradi, maendeleo ya ujenzi na maneno ya beberu je vinaendana? Kama mradi uko nyuma ya mpango tunamwamini beberu kuwa mnachelewesha malipo!
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,139
2,000
Mbona kaongea kama wale akina mama, zamani waliokuwa wakiitwa mashambenga?

Tanzania sijui tuna watu wa namna gani! Maana akiongea anayejiita dokta msomi, kuna wakati unaona ni afadhali aongee Musukuma wa darasa la saba, ataongea kitu cha maana.

Huyu abasi kwa maneno yake haya unaona kabisa ni wale wanaoitwa madokta kwa sababu ya kukaa darasani miaka mingi, lakini siyo kwa sababu ya maarifa au kile kilichomo kichwani.
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
4,179
2,000
Yaani katika watu huwa wanafanya mikutano na waandishi wa habari kwa mtindo wa kuudhi ni huyu jamaa. Ni bora awe anatoa press release ya kuandika ila kuongea huwa anaongea hovyo sana kama sio Professional wa tasnia ya habari kabisa.

Au sijui ndo kujitoa ufahamu tu.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,125
2,000
Formal media zote ni za kwako na zinaimba sufa zako saa 24/7.

TBC1, TBC FM, TBC TAIFA, CHANNEL TEN, MAGIC FM, RADIO UHURU, GAZETI MZALENDO, TV, GAZETI UHURU, HABARI LEO, DAILY NEWS, SUNDAY NEWS, TANZANITE ONLINE TV, TANZANITE GAZETI, JIJI, GLOBAL MEDIA, WASAFI MEDIA, CLOUDS TV, RADIO FREE AFRICA, ABOOD FM n.m

Lakini bado mnateseka na kuumia na vi-social media accounts vya Kigogo2014, Maria Sarungi na Fatma Karume.

Jamani CCM tendeni haki mpate Amani, hicho ndicho kitu cha msingi. Mmekuwa na tamaa ya kupindukia
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,125
2,000
Yaani katika watu huwa wanafanya mikutano na waandishi wa habari kwa mtindo wa kuudhi ni huyu jamaa. Ni bora awe anatoa press release ya kuandika ila kuongea huwa anaongea hovyo sana kama sio Professional wa tasnia ya habari kabisa


Au sijui ndo kujitoa ufahamu tu
Imagine huyo bumunda kwenye nchi ya watu million 60 amepewa vyeo viwili.


1. Katibu Mkuu wizara ya habari

2. Msemaji wa Serikali

Hii nchi ni Mungu tu anajua
 

Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,125
2,000
Formal media zote ni za kwako na zinaimba sufa zako saa 24/7.

TBC1, TBC FM, TBC TAIFA, CHANNEL TEN, MAGIC FM, RADIO UHURU, GAZETI MZALENDO, TV, GAZETI UHURU, HABARI LEO, DAILY NEWS, SUNDAY NEWS, TANZANITE ONLINE TV, TANZANITE GAZETI, JIJI, GLOBAL MEDIA, WASAFI MEDIA, CLOUDS TV, RADIO FREE AFRICA, ABOOD FM n.m

Lakini bado mnateseka na kuumia na vi-social media accounts vya Kigogo2014, Maria Sarungi na Fatma Karume.

Jamani CCM tendeni haki mpate Amani, hicho ndicho kitu cha msingi. Mmekuwa na tamaa ya kupindukia
Wanataka watende Dhambi na wawe na amani. Imeandikwa hakuna amani Kwa mabaya.
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,086
2,000
Hivi kwanini kila wakisemwa kdg tu wanakuwa wakali sana?
Ukweli hawautaki! uongo ndio dira yao!
Kwanini msiache jamii iwakosoe ili muwajibu kwa matendo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom