Serikali Kujenga Kituo cha Afya Kata ya Mtunda, Kibiti

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,685
1,235

SERIKALI KUJENGA KITUO CHA AFYA KATA YA MTUNDA, KIBITI

"Kata ya Mtunda ni Kata ya kimkakati katika Jimbo la Kibiti ambayo ilikumbwa na mafuriko kipindi kilichopita. Je, nini kauli ya Serikali katika kujenga kituo cha Afya kwa wananchi ambao wamesubiri kwa muda mrefu sana?" - Mhe. Twaha Mpembenwe, Mbunge wa Jimbo la Kibiti

"Kata zote za kimkakati ambazo Halmashauri zilikubaliana na kuwasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI tumeziwekea Mpango wa Utekelezaji wa kupitia Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Mpango wa kupitia fedha Serikali Kuu" - Naibu Waziri TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange

"Naomba nimuhakikishie Mhe. Mpembenwe, amefuatilia mara kadhaa Kuhusu kituo cha Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI tumeweka kipaumbele kuhakikisha wananchi wa Kata Mtunda wanapata kituo cha Afya ili waweze kupata huduma bora"
 

Attachments

  • D1vG8fPw_400x400.jpg
    D1vG8fPw_400x400.jpg
    25.2 KB · Views: 2
Back
Top Bottom