Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kuanzia sasa Serikali itaanza kuzitazama ajira za vyuo vikuu badala ya kuangalia ubora wa ufaulu yaani GPA pekee sasa waajiriwe kwa kupimwa uwezo wao kwa kufanya usaili.

Kuangalia ufaulu pekee wa wanafunzi haitoshi kuboresha elimu badala yake ni muhimu kuongeza vigezo hivyo katika mapitio ya sera na mabadili ya mitaala jambo hilo litatazamwa kwa weledi mkubwa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2022 mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania iliyofanyika Kinondoni Jijini Dar es Salam.

Amesema wakati serikali inaongeza udahili wa wanafunzi haitakuwa tayari kuona ubora unapungua hivyo serikali inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha ubora wa elimu hususani katika vyuo vikuu unaimarika.

"Zamani ilikuwa rahisi kuwa Profesa ukiandika tu kwenye magazeti unakuwa Profesa lakini kwa sasa vigezo vya kuwa Profesa vimezidi kuwa vigumu kwa sababu tunataka maprofesa wetu wawe sawa na wale wa nchi zingine," amekaririwa Prof Mkenda.

Amesema katika mageuzi ya elimu yanayokuja ambapo wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika mapitio ya sera na mitaala miongoni mwa mambo yatakayofanyiwa kazi itakuwa ni pamoja na kuhakikisha wanaoajiriwa ni wanafunzi wenye sifa zinazotakiwa.

Pia, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali kwa sasa inaendelea na Ujenzi wa Kampasi mpya za Vyuo Vikuu katika mikoa 14 Tanzania pamoja na upande wa Zanzibar (Unguja na Pemba) katika maeneo ambayo hayana vyuo vikuu ukiacha vyuo huria.

Mikoa hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na kampasi za vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini ni pamoja na Tabora, Katavi, Kigoma, Kagera, Singida, Manyara, Lindi, Rukwa, Mwanza, Simiyu, Tanga, Ruvuma, Shinyanga na Dodoma.
 
Kweli nchi inaenda kubaya sana. Kwa hiyo wakifanyiwa usaili ndio elimu inakuwa bora. 😀😀😀😀😀.
Mtu mwenye GPA kubwa kwa vyuo kama SUA, MZUMBE na UDSM huyo anauwezo mkubwa, haina haja ya kujiuliza mara mbili.

Nenda uendako, kwenye usaili watu wanakalili na kufaulu baada ya hapo wanasahau. Ila mwenye GPA kubwa ni mtu mwenye uwezo.

Haiwezekani mtu kidato cha Nne abamize one ya saba, kidato cha sita one ya nne na chuo GPA ya 4.6. Useme hana uwezo badala yake utegemee kumpima kwenye usaili Ili kupima uwezo wake.

Tuwekeze kwenye practical zaidi
 
Siku hizi binti akiwa pisi kali anaruka na lecturers tu analamba GPA kali, kijana akiwa yupo kwenye circle ya huyo binti (wanafanya discussion pamoja ya mapepa anayovujishiwa) nae anakula GPA kali. Wakienda kwenye practical makazini wanaanza upya. Ufanisi hauendani na GPA.

Wale wenzangu na mie shule za kuunga unga msuli tembo marks sisimizi, wakikaza zaidi wanakula 4.0 kushuka chini.

Nimekumbuka mwaka wa pili chuoni kuna lecturer pisi kali haswa tuliletewa kala GPA 4.7 aje atufundishe parasitology, cha ajabu hata kudadavua lifecycle za Plasmodium na Wuchereria bancrofti ilikua changamoto.

Kwahiyo naunga mkono hoja, suala la kuangalia GPA katika kuajili hawa T.A na Lecturers vyuoni lisipewe mkazo sana bali wawe strict na usaili ili wapate cream iliyo bora kuwafundisha vijana wetu huko vyuoni.
 
D42CC97B-6976-402F-94AA-7661A56A803F.jpeg
Professor soma hii
 
Back
Top Bottom