Serikali kuja na pedi za kike za kurudia

Ubunifu gani utakaofanyika hapo zaidi ya kuiga tu au kukopi kwa wenzetu hizo pedi za kutumia zaid ya mara moja zipo muda tu.
b5ab8ad8c731a93edf3152ac4eda8ff5.jpg
Shirika ninaliofanyia kazi pia tumeanza kitambo kuzitoa. Mwanzoni tulikuwa tunatoa kenya shirika la Huru international. Badae tukahamishia ujuzi kwenye vikundi vya kina Mama wajasiriamali, wanatengeneza na wanauza kwa walengwa. Ni nzuri sana na zinasaidia mno.
Sema changamoto kubwa, watoto wetu wengi wa vijijini ht pichu in ishu.
 
Hapa ni uokoe pesa au afya....
Serikali haishindwi kuongeza ruzuku na kuwapatia watoto wa kike pedi ,hata kama ni kuwachangisha wazazi na wadau wa elimu..
 
Blaa!! Blaa!! nyingi.

Serikali imesema inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kunauwezekano wa kupata taulo za hedhi ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Kigwangalla2.JPG

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla kwenye mahojianio na EATV kuhusu jitihada za serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa ya kuambukizwa.

shigoli1.JPG


Jenifer Shigoli

Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja Bi. Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
 
Maskini pua zangu! Sijui kama tutavumiliana kwenye mabasi ya ferry! Shombo la samaki huku smell za papuchi!
 
Back
Top Bottom