Serikali kuja na pedi za kike za kurudia

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,201
2,000
Serikali imesema inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kunauwezekano wa kupata taulo za hedhi ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla kwenye mahojianio na EATV kuhusu jitihada za serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa ya kuambukizwa.Jenifer Shigoli

Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja Bi. Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom