Serikali kuja na pedi za kike za kurudia

Serikali imesema inafanya tafiti mbalimbali ili kubaini na kuona kama kunauwezekano wa kupata taulo za hedhi ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.

Kigwangalla2.JPG

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla kwenye mahojianio na EATV kuhusu jitihada za serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha utoro mashuleni kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.

Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa ya kuambukizwa.

shigoli1.JPG

Jenifer Shigoli

Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja Bi. Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
Tujiandae kurudi kwenye enzi za kuvaa magome ya miti
 
Tafiti wapi, waache ujanja. Hizi pedi zipo muda mrefu sana huko kasulu maana wakimbizi wa kambi ya nyarugusu wanagawiwa bure maboksi kwa maboksi na wanaziuza mjini. Sasa huo utafiti gani wanaufanya. Waache kudanganya bwana
 
Mhhh kufua?? Hope za buku3 bado zitaendelea kuwepo
 
Huyu Nassoro Bagaile, a.k.a hamisi kigwangala nae ana mambo!, sasa WakinaDinazarde wamemwambia kuwa wanataka kurudia pedi!? That' s a political stunt!!!
 
Serikali itoe ruzuku, pedi ziuzwe sawa na bure kila mwanamke aweze kupata
Hii ya kufua ni mtihani,
 
wapeleke vijijini Kyle pedi zao no vitambaa vya khanga
 
Duuu Hakuna kitu hapo zaidi ya kutaka kunyimana raha katika matendo ya ndoa harufu itatunyima raha
 
Kingwala huo ni uchafu wenzetu wanatengeneza za kubadili masaa machache tuu wewe umekaa kufikiri kutunza uchafu mwezi mzima..punguzeni ukiritimba viwanda vidogo viwepo hapo mbona huku ni hao hao watanzania wana hivyo viwanda vya Tissue,ped,petrolium jel na vingine viingi tuu..
 
Back
Top Bottom