Serikali kuhamia Dodoma: Serikali imefanya makosa kuruhusu taasisi zake kujenga ofisi katikakati ya mji

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Manispaa ya Dodoma ilipima viwanja vingi tu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma hasa baada ya Makao Makuu ya Nchi kuhamishiwa Dodoma. Sio Manispaa tu, bali hata makampuni binafsi yamepima na kuuza viwanja vingi tu.

Maeneo hayo ni pamoja na Mtumba, Nata, Ihumwa, Nzuguni, Michese, Mapinduzi, Nong'ona, n.k. Katika maeneo haya, mbali na viwanja kwa ajili ya makazi, lakini pia kulikuwa na viwanja vikubwa kwa ajili ya ujenzi wa taasisi mbalimbali, mashule, nyumba za Ibada, n.k .

Kwa mtazamo wangu, nilitarajia serikali ingezitaka taasisi zake zinazohamia Dodoma kujenga ofisi zake katika maeneo haya mapya yaliyopimwa ili kuendeleza na kupanua mji, lakini kinachoendelea kwa sasa ni kinyume chake kwanini taasisi nyingi zinatafuta viwanja katika ya mji na kujenga ofisi zao (Headquarter).

Kwa mfano, kwa sasa kuna eneo moja hapa Dodoma ndio taasisi kibao za serikali zinaonekana kujenga ofisi zao. Kwa wanaoijua Dodoma, eneo hili ndio uliop ukumbi wa CCM wa Jakaya Kikwete, Ofisi za Hazina, Bima ya Afya, CAG na nyinginezo huku magorofa mengine yakiendelea kujengwa katika eneo hili liilko katika barabara ya kuelekea Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Binafsi naamini, taasisi za serikali zinazohamia Dodoma, zingejenga katika maeneo haya mapya, hata huduma za maji na umeme zingefika katika maeneo haya kwa haraka zaidi na hii ingechochea wananchi walionunua viwanja katika maeneo haya mapya kujenga nyumba za makazi na hata za kibiashara kwanini huduma za maji na umeme zingekuwa zinapatikana.

Hata hivyo, serikali bado haijachelewa sana kuingilia kati na kurekebisha hali hii, vinginevyo yale ya Dar ambapo ofisi nyingi zilirundikana Posta yatajirudia hapa Dodoma.

Kama mji wa serikali umejengengwa Mtumba, kwanini taasisi zake nazo sisijengwa nje ya mji wakati mnajenga barabara ya kuunganisha mji mzima(ring road)?

Msiseme hatukuwashauri.
 
Maeneo ya Taasisi za Serikali Kwa Dodoma ni 2 yaani Medeli na Mtumba ndiko Serikali inajenga taasisi zake..

Mimi sioni shida Kwa sababu sio busara Sana Serikali kujitenga moja kwa moja na Wananchi kwa kukaa peke yao kule Mtumba.

Hii itafanya huduma Bora kuwa sehemu moja na kuleta matabaka.
 
Maeneo ya Taasisi za Serikali Kwa Dodoma ni 2 yaani Medeli na Mtumba ndiko Serikali inajenga taasisi zake..

Mimi sioni shida Kwa sababu sio busara Sana Serikali kujitenga moja kwa moja na Wananchi kwa kukaa peke yao kule Mtumba..

Hii itafanya huduma Bora kuwa sehemu moja na kuleta matabaka.
Sijui kama umesoma na kuelewa vizuri nilichoandika.
 
Soma haya maandishi!! WIZARA ZOTE ZIHAMIE HUKO MAMBO YA BIASHARA YAACHWE DAR ES SALAAM TATIZO NI HILI TENGANISHA BIASHARA,CCM, NA SERIKALI yaani mtu mmoja yupo Kwa biashara CCM NA SERIKALI that is wrong ,Kenya wana bandari Mombasa mbona activity zinaenda!
 
Siku hizi umepoa sana au na wewe upo kwenye basi moja la wanalambishwa asali?
 
Back
Top Bottom