Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu

Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu

Ni vizuri sana kuwalipa ,kama wasingewalipa Serikali ya UKAWA ingewavuta ukosi wale wote waliohusika na malipo na kuwahoji.

CCM ijitahidi kulipa kila kitu kabla ya kuondolewa madarakani hapo 25 ,tunaelewa kifo cha CCM kimekaribia Wasije wakafa na madeni

Kabisa!
 
walimu wa tanganyika sielewi kwa nni wananyanyaswa sana,mara wakopwe mara wachapwe viboko,yaani nivululu tu.
 
Kama hakuna mwalimu anayedai hicho wanachotaka kuwalipa ni nini?

SERIKALI imesema kwamba imeshalipa madeni ya walimu ya kiasi cha Sh. bilioni 5.7 ambayo yaligungulika kihalali kati ya Sh. bilioni 19.6 zilizokuwa zinadaiwa kudaiwa, hivyo kwa sasa hakuna malalamiko mwalimu ambaye hajalipwa.

Aidha Serikali imependekeza kwamba halimashauri zilizowasilisha madeni ambayo si halali, yenye shaka, au watumishi wasio na madai, madai ya watumishi wasio na madai, madai ya watumishi waliokwishalipwa na waliowasilisha madai ya mishahara kama madai yasiyo ya mishahara wawajibishwe.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Likwelile alisema hayo wakati akitoa taarifa ya uhakiki wa madeni ya walimu wa shule za msingi, sekondari na Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Alisema awali wizara yake ilipokea madai ya walimu kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) na watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(WEMU)yenye jumla ya Sh. bilioni 19.6 ikiwa Sh. bilioni 17.4 kutoka TAMISEMI na Sh. bilioni 2.1 kutoka WEMU.

"Madeni ambayo hajalipwa ni kwa sababu hakuna kielelezo juu ya madai hayo," alisema Dkt. Likwelile .
Aliongeza kwamba wizara yake kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali, ilifanya uchambuzi wa awali kwa lengo la kujiridhisha na takwimu zilizowasilishwa na TAMISEMI kwa kila halimashauri na kwa watumishi wa WEMU, ambao umeonesha kuwa na shaka na baadhi ya madai.

"Baada ya uchambuzi wa awali idara iliandaa hadidu za rejea kwa lengo la kufanya uhakiki wa madai yaliyowasilishwa. Uhakiki huo ulifanywa na wakaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na timu ya wakaguzi wa ndani chini ya usimamizi wa idara hiyo.

"Matokeo ya uchambuzi wa awali yalipelekea madai ya walimu na watumishi yasiyo ya mishahara kupungua kutoka Sh. 19.6 hadi kufikia Sh. bilioni 16.2.," alisema.

Alifafanua kwamba madai hayo yaliyohakikiwa yalihusisha walimu 16,315 kutoka halimashauri 147 na watumishi, 1,152 kutoka WEMU. Madai yasiyohakikiwa ni Sh. bilioni 3.3 yakihusisha walimu 1,448 ambao hawakuwa na cheki namba na walimu 1,834 ambao cheki namba hazikuonekana kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya utumishi wa Serikali.

Dkt.Likwelile alisema kazi ya uhakiki katika halimashauri na WEMU ilifanyika kuanzia Machi 12, mwaka huu hadi Aprili 11, mwaka huu.

Aliongeza kwamba matokeo ya uhakiki yameonesha kiasi cha Sh. 5.7 kimekubaliwa na kiasi kilichokataliwa ni Sh.bilioni 10.5.

"Zoezi hili la uhakiki wa madai limeiwezeshha Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na iwapo malipo yangefanyika bila kufanya uhakiki," alisisitiza.

Alizitaja baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni kuendelea kuwepo kwa madi ya muda mrefu kwenye halimashauri, baadhi ya madai kuwasilishwa kama madai ya mshahara, kutokuwepo kwa kumbukumbu za madai kwenye majalada ya watumishi, majalada ya walimu kutopatikana na hivyo baadhi ya madai kutohakikiwa.

Changamoto nyingine ni baadhi ya madai yaliyokwisha kulipwa kuwasilishwa kama madai mapya na baadhi ya madai kuwasilishwa zaidi ya mara moja kwa madai yanayofanana.

Akitolea mfano wa madai hayo Mkaguzi wa mifumo ya kompyuta kutoka wizra hiyo alisema yupo mwalimu aliyekuwa akidai Sh. milioni 500, wakati deni sahihi ni Sh. laki tano.
 
Ni vizuri sana kuwalipa ,kama wasingewalipa Serikali ya UKAWA ingewavuta ukosi wale wote waliohusika na malipo na kuwahoji.

CCM ijitahidi kulipa kila kitu kabla ya kuondolewa madarakani hapo 25 ,tunaelewa kifo cha CCM kimekaribia Wasije wakafa na madeni

CCM iko mita chache sana kutoka kaburini.Si zaidi ya MITA 17.
 
Kuanzia wiki ijayo serikali itaanza kulipa madai ya walimu ambayo yanafikia bilion 32.wakuu nauliza hii sio kampeni chafu ya chama cha mapinduzi. Walikuwa wapi siku zote wasiwalipe hadi waje wawalipe wiki ijayo ilhali tayari kuna walimu wengine walishakufa wakiwa njiani kufuatilia madai yao. CCM acheni kampeni za kizamani

Na umeme nao je wataanza kushughulikia lini.. hii serikal kila kona siasa tu..
@# HAPA GIZA TU.
 
Wanipe nipate za kuhimiza mabadiliko.maana kuna makamanda wanaojituma ila kipato ni kidogo.nitawasaidia.
 
Kuanzia wiki ijayo serikali itaanza kulipa madai ya walimu ambayo yanafikia bilion 32.wakuu nauliza hii sio kampeni chafu ya chama cha mapinduzi. Walikuwa wapi siku zote wasiwalipe hadi waje wawalipe wiki ijayo ilhali tayari kuna walimu wengine walishakufa wakiwa njiani kufuatilia madai yao. CCM acheni kampeni za kizamani
kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya hivi majuzi some of them wametokea chama cha walimu, lengo ilikua kuwashika akili wale wajuu, wafanye wanavyoweza wawatulize walimu ili kuokoa chama!
 
Kuanzia wiki ijayo serikali itaanza kulipa madai ya walimu ambayo yanafikia bilion 32.wakuu nauliza hii sio kampeni chafu ya chama cha mapinduzi. Walikuwa wapi siku zote wasiwalipe hadi waje wawalipe wiki ijayo ilhali tayari kuna walimu wengine walishakufa wakiwa njiani kufuatilia madai yao. CCM acheni kampeni za kizamani
Mkuu wa idara zingine kama kilimo, afya na nyengine tunao idai selekali hatulipwi?
 
Mwalimu mmoja anafundisha shule la kwanza hadi la saba, (uhaba wa walimu) anashindwa kufundisha, mwanafunzi anafundishwa na walimu saba, asipoelewa KOSA! Imekaaje hii?
 
Hapa kuna dhuluma imefanyika kwa namna moja au nyingine. Ni kwanini wasingewaita walimu wanaodai ili kudhibitisha madai yao na vielelezo vyao kama ni vya kweli na vinakidhi? Jambo kama hili liliwahi fanyika mwaka 2010 na lilisaidia sana japo wachache hawakulipwa nikiwa mmoja wao. Nasema hivi kwasababu watendaji wa ofisi za halmashauri huwa na tabia ya kujilipa madai ya walimu kwa kuchomoa vielelezo vya madai kwenye mafaili ya walimu ili waati wa ukaguzi visionekane na huenda mchezo huu unaendelea. Binafsi sijawahi lipwa likizo kwakipindi chote cha utumishi wa miaka 22 na ukihoji ni kwanini unapata jibu la serikali haina pesa. Isitoshe hata nilipojiendeleza sikuwahi kupewa hata nauli na ada kama watendewavyo watumishi wengine kwa jibu la kuwa sikuwekwa kwenye mpango wa halmashauri na juzi nilibahatika kuliona faili langu likiwa limenyofolewa hadi barua ya ajira haipo. Huu ni unyanyasaji kwa kweli.
 
asikudanganye mtu kuwa wanaweza kulipa wiki ijayo,kwani nimemsikia madai mengi ni malimbikizo ya mshahara, haya yanalipwa pamoja na mshahara ,la kama mshahara utatoka wiki ijayo sawa
Sikugusi
 
Asiyeona kuwa hizi ni campaign chafu ni mjinga.Lete pesa yetu tule.Ila tarehe 25 tutamchinja Magufuli kwa kuwa chama na serikali yao imetu cheleweshea haki yetu.
Kuanzia wiki ijayo serikali itaanza kulipa madai ya walimu ambayo yanafikia bilion 32.wakuu nauliza hii sio kampeni chafu ya chama cha mapinduzi. Walikuwa wapi siku zote wasiwalipe hadi waje wawalipe wiki ijayo ilhali tayari kuna walimu wengine walishakufa wakiwa njiani kufuatilia madai yao. CCM acheni kampeni za kizamani
 
Kuanzia wiki ijayo serikali itaanza kulipa madai ya walimu ambayo yanafikia bilion 32.wakuu nauliza hii sio kampeni chafu ya chama cha mapinduzi. Walikuwa wapi siku zote wasiwalipe hadi waje wawalipe wiki ijayo ilhali tayari kuna walimu wengine walishakufa wakiwa njiani kufuatilia madai yao. CCM acheni kampeni za kizamani
Si haki yao hao wewe unataka walipwe lini?
 
Hizo ni rushwa,kipindi chote mlikuwa wapi mafisadi nyie
Kumlipa mtu haki yake ni rushwa? Kwa hiyo hata wafanyakazi wa serikalini wasilipwe mishahara yao sasa hivi itakuwa rushwa?
 
Yaani hata sie tunaodai likizo na nyongeza stahiki ya madaraka tutapata?
 
Back
Top Bottom