Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Kuna watu wana mawazo ya ajabu sana.. Usishangae gawa wanakuja kuwa na post kubwa serikalini
 
Kuna hoja ya msingi, ingawa najua itapingwa hapa kwa hoja nyepesi. Hakuna sababu ya mtu kuja Dar halafu analala kwenye vibaraza vya maduka kwa kutandika na kujifunika mabox, halafu mtu anasema tutabanana hapa hapa!

attachment.php
 
Watu wenyewe wa Dar ya tangu enzi za Shomvi anatoka Barawa, tangu enzi za Sayyidina Said Majid, tangu enzi za Dr. Seward na Pazi Mazungera, tangu enzi za Jumbe Tambaza huwezi kutusikia tunaongea maneno mbofumbofu.

Ni hawa wa kuja juzi na mbio za Mwenge hata ukiwauliza Odeon iko wapi, City Drive imeanzia wapi na kuishia wapi na kwa nini imebadilishwa jina? Kitchwele ni wapi? Mwembetogwa pako wapi? Mchafukoge inaanzia wapi na kuishia wapi?

Mtu hajui Aga Khan kauziwa na nani uwanja wa kujenga shule, au kwa nini Salender Bridge linaitwa Salender Bridge.

Mtu hajui Tangi Bovu liko wapi, na kwa nini kwa Sykes kunaitwa kwa Sykes.

Hamjui Mwanamboka alianzia wapi, Mengi alijaza wino kwenye peni nyumbani kwake wapi, wala kiosk cha kwanza cha Bakhressa kilikuwa wapi.

Mtu hajui Saigoni iko wapi, na chapati kwa mchuzi inaliwaje.

Hamjui Sykes wala Mwinyijuma, Chamgui wala Rupia.

Hana historia ya familia Misheni kota wala Gerezani.

Watoto hawajui hata historia ya Jumbe Tambaza alivyomtilia ngumu Carl Peters kuuza vijiji vya Mzi Mzima kwa rupia 15 kila kijiji.

Leo wanataka kukuambia Dar es salaam kwao wanakataza wengine wasije.

By Tambaza na mimi nikirudi naweza kuitwa mgeni wakati babu wa Bibi yangu kajenga Azania Front mpaka kulimaliza 1903 !

Sasa kama.wenye mji wenyewe hatuwezi kukataza wagenu, mshihiri gani wa kutoka wapu anaweza kujipakazia yeye Dar ndio kwao?

Kiranga salute sana mkuu,
Unanikumbusha enzi za kula ice cream kwa bakhresa hapa livingstone au kwa chalinze lumumba nikitaka pamba kijiti nashuka malapa inn!!!!!
Fete fair ya wagiriki (mabembea) mnazi mmoja!!!!
Kulaboda Mchikichi,gerezani to keko! !!!!!
Mix kwa Kenge!!!!!!
Nakimbia na pila (used tyre) Livingstone yote!!!!!
Ukonga ndo kwa babu ukiambiwa safari ya huko maembe yanatetemeka,na narudi na pepeta za kutosha!!!!!!

Dar was Dar kaka sasa mtu kama huyu ukimuuliza pepeta ni nini atatoa macho hapa!!!!!

Wapumzike kwa amani wazee wenye mji wao!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wakazi wote wa Dar tupewe vitambulisho special.., hakuna kuingia Dar kama huna hicho kitambulisho.., unless uwe umepata kazi huku au unamwaliko maalumu kutoka kwa mwana Dar.., na hiyo shughuli iliyokuleta ikiisha unarudi ulikotoka.., TUMEJAAA...!!

Mzee wa kazi wewe unaweza jikuta huna sababu ya kuwapo kama tunaongelea wenye kwao, ni vipi kama ukipewa work permit tu???!!!!
Kumbuka ajira sio sababu ya mtu kuwa mwenyeji wa sehemu husika!!!!!
 
Unaogopa watakuibia power window za lile landcruiser mpya uliyonunua juzi!!
 
bora iwe hivyo mkuu hawa watu wa bara wamekuwa wengi mno au wawe wanaingia kwa passport na visa

watu tunafika na mishe zetu kisha tunasepa coz dar kwenyew wanaoishi mbona wachache? isije ikawa ni miongoni mwa wanaoishi kweny vidimbwi
 
Mwenzio amewaza kwa kichwa sio makalio kama wewe! pambaf!


Acha matusi jenga hoja unamtukana mwenzio ili iweje au nawewe Dar ya baba yako

Use common sense
 
Kisiwani ka zenji vile...vunjeni daraja la Mzinga pale Kongowe na Kivuko cha Kigamboni kipigeni Boom na vunjeni daraja la Ruvu...kwisha. Mtabaki wenyewe tu hapo daslam.
Kikubwa tafuteni njia mbadala mtu akitoka Mtwara anaenda Tanga basi asipite hapo Jiji la Joto na Kero zilizokithiri.
 
Kuna watu wana mawazo ya ajabu sana.. Usishangae gawa wanakuja kuwa na post kubwa serikalini

Ukute hata aliyezuia bodaboda na vibajaji alianza kama huyu mwehu...yaani bila sababu za msingi unakurupuka tu.
 
ushukuru lile lori la pilipili lililokupa lift kuja hapa dar, nakumbuka mjomba ako alitutuma tuje tukupokekee kidongo chekundu ukiwa unapiga chafya sana.! na toka ufike hap umeanza kuchambua makosa hap na pale wakat hata miaka 10 hujamaliza, je tukikupa na kaudiwani itakuwaJE...
 
Kwani hiyo Dar ni ya baba yakoooo!!!!!!!!!! We ndio uhamee ukaishi kijijiin au utengeneze mji wako watu wasijee
 
Hapo sasa utashitakiwa....kila mtu anaota kuja DSM hata kama siyo kuishi. Mimi nilikuwa naota sana kwenda New York City (NYC) hadi nilipofika ndiyo kiu yangu ikatulia
 
Back
Top Bottom