Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Halafu anamsaidia dada yake huko kwa shemeji kuosha vyombo na kwenda gengeni. Ndio anajiona mjanja huko anakokaa Tandale Kwamtogole kwa Tumbo!

Habari za kukataza watu kuja Dar hawakuweza kina Nyerere na Sokoine siku za chama kimoja.

Hakuna atakayeweza leo kwa sababu watu wana uhuru wa kuhoji zaidi.

Hii habari nzima inavunja ibara ya 17 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inayoongelea Freedom of Movement kwa Watanzania.

This prospective restriction is unconstitutional.

Soma hapa pp. 18-19

17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

(2) Kitendochochote cha halali au sheria yoyote yenye madhumuni ya -

(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako na kumweka chini ya ulinzi au kifungoni;
au

(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wa mtu kwenda anakotaka ili-
(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;
au
(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibu wowote anaotakiwa na sheria nyingine
kuutimiza; au
(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumla au kuhifadhi maslahi fulani mahususi au maslahi ya sehemu fulani ya umma,
kitendo hicho hakitahesabiwa au sheria hiyo haitahesabiwa kuwa ni haramu au ni kinyume cha ibara hii.

Cc : EMT
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nafikiri wakati umefika sasa kwa Serikali ianze kuzuia watu kutoka Mikoani kuja Dar, tumetosha sasa! ikiwezekana Waruhusiwe wale tu ambao wamepata kazi au walioitwa kwenye usahili... Hali inatisha sana ukienda Ubungo Mabasi yanakuja yamejaa na yanaondoka tupu, kwa nini hamkai huko Mikoani mbona mnatutambia kuna kuna Hali ya Hewa nzuri, sasa ni nini kinawaleta Dar?

Ivi wakati unaandika hii thread ulikua na ulevi gani kichwani mwako?
Au ni akili yako ndio imekutuma uandike hivyo?

tuanzie hapo, ukinijibu nitakwambia nini sababu ya kukuuliza maswali hayo!
 
Itakayemshinda dar ahame yeye, wanaoiweza wabaki. By october nitakuwa mkazi wa jiji la tanga, burudaaani pasi na bugudha!
 
Itakayemshinda dar ahame yeye, wanaoiweza wabaki. By october nitakuwa mkazi wa jiji la tanga, burudaaani pasi na bugudha!

Tanga bomba kichizi, ina mji uliopangwa vizuri, bandari, haina msongamano, sio mbali sana na Dar etc.

People are sleeping on Tanga.

Kulikuwa na haja ya ku decentralize na kuipa miji kama Tanga, Mwanza na Mbeya kipaumbele.

Then utaona msongamano wa kila mtu kulundikana Dar unapungua naturally.
 
Nafikiri wakati umefika sasa kwa Serikali ianze kuzuia watu kutoka Mikoani kuja Dar, tumetosha sasa! ikiwezekana Waruhusiwe wale tu ambao wamepata kazi au walioitwa kwenye usahili... Hali inatisha sana ukienda Ubungo Mabasi yanakuja yamejaa na yanaondoka tupu, kwa nini hamkai huko Mikoani mbona mnatutambia kuna kuna Hali ya Hewa nzuri, sasa ni nini kinawaleta Dar?
kodi zote ziache kuja dar ili tujipangie maendeleo yetu wenyewe, gess,dhahabu na mengineyo yanufaishe kule yanako toka
 
Back
Top Bottom