Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

watu kuja dar watakuja sana,labd kungekua na kifungu chochot kile ktk ktiba yet hapo ndo ningesem wametosh,ss wew hilo wazo umelitoa wap,badilish usemi wako,dar watu wakuja kwa mambo mbalimbal,zikiwem matibabu,vyuo,shule hata utaftaji wa kimaisha
 
Kuna hoja ya msingi, ingawa najua itapingwa hapa kwa hoja nyepesi. Hakuna sababu ya mtu kuja Dar halafu analala kwenye vibaraza vya maduka kwa kutandika na kujifunika mabox, halafu mtu anasema tutabanana hapa hapa!

attachment.php

I see unconstitutionality in this.

Let me break it down as a true Dar debonair with much regard for the rule of law, human rights and international morality.

Hoja yoyote ya msingi itakayoletwa hapa itaondoka uhalali kwa kukiuka uhalali wa kikatiba wa Watanzania kwenda popote ndani ya nchi yao.

Kama kuna tatizo la watu kulala kwenye vibaraza, jiji lina sheria zake, wekeni sheria kukataza kulala vibarazani hata maMwinyi wa Muhonda wasiweze kulala mabarazani mwao wakizidiwa na joto ndani.

Tukianza habari za kuombana visa za kuja Dar -this is what it will come down to- what's to stop the same logic from saying "wapiga kura wengi hawajui wanachopigia kura, inabidi wapasi mtihani kabla ya kuweza kupiga kura".

There is a reason the constitution is the constitution.

Nenda kasome ibara ya 17 ya katiba "The Right To Freedom of Movement".

attachment.php
17.-(1) Every citizen of the United Republic has the right to freedom of movement in the United Republic and the right to live in any part of the United Republic, to leave and enter the country, and the right not to be forced to leave or be expelled from the United Republic.

(2) Any lawful act or any law which is intended to -
(a) curtail a person's freedom of movement and to restrain or imprison him; or
(b) limit a person from exercising his freedom of movement so as to -
(i) execute a judgment or court order; or
(ii) compel a person first to comply with any obligations arising under another law; or
(iii) protect public interest in general or preserve certain special interest or interests of a certain section of the
public,

such act or law shall not be construed or be held to be repugnant to or inconsistent with the provisions of this Article.

attachment.php
 
Tunashukuru hatutakuja Dar! Kwanza tunaambiwa chips zinakaangwa kwa mafuta ya transfoma; juisi ni ya ukwaju; samaki mpaka uende feri ukanunue waliokaangwa kwa mafungu. Huku mikoani mambo ni mswano!
 
Wewe masai! Una work permit ya kulinda usiku na kusuka nywele mchana?

Ha ha haaaa maasai long kitambo down town mamii,chotara wa kinubi mzawa wa muhimbili makuzi mchikichi, wakariakoo wanajua ngoma ya kilua nikitoroka kucheza anatoglo! !!!!!!!!

Sitaki kuoga karoni mpaka hela ya koni kwa bakhresa mamake!!!!!
Mdundiko unatokea gerezani unakatiza livingstone ole wako utie miguu yako, by then unachapwa na chelewa tu miguuni au bibi (RIP) akufinye mpaka ukojoe ndo anajua umeelewa!!!!!!

Ila bado mashuka yangu ninayo m keepin it real,na bush nazuka saaana tu kwa boma!!!!!!
Na huwezi taja madiwani wa kariakoo bila kukuta damu yangu humo!!!!!
 
Nafikiri wakati umefika sasa kwa Serikali ianze kuzuia watu kutoka Mikoani kuja Dar, tumetosha sasa! ikiwezekana Waruhusiwe wale tu ambao wamepata kazi au walioitwa kwenye usahili... Hali inatisha sana ukienda Ubungo Mabasi yanakuja yamejaa na yanaondoka tupu, kwa nini hamkai huko Mikoani mbona mnatutambia kuna kuna Hali ya Hewa nzuri, sasa ni nini kinawaleta Dar?

Ubinafsi siyo mzuri!
 
hata magar yanayoingia dar kuleta vyakula yaje kwa rimote. vyakula mlime wenyewe huko huko dar kwenu.
 
Kiranga salute sana mkuu,
Unanikumbusha enzi za kula ice cream kwa bakhresa hapa livingstone au kwa chalinze lumumba nikitaka pamba kijiti nashuka malapa inn!!!!!
Fete fair ya wagiriki (mabembea) mnazi mmoja!!!!
Kulaboda Mchikichi,gerezani to keko! !!!!!
Mix kwa Kenge!!!!!!
Nakimbia na pila (used tyre) Livingstone yote!!!!!
Ukonga ndo kwa babu ukiambiwa safari ya huko maembe yanatetemeka,na narudi na pepeta za kutosha!!!!!!

Dar was Dar kaka sasa mtu kama huyu ukimuuliza pepeta ni nini atatoa macho hapa!!!!!

Wapumzike kwa amani wazee wenye mji wao!!!!!!

Duh, umenikumbusha pepeta mwana.

Kwa Bakhressa watu tumeenda kuangalia "Commando John" huku unapata world class chocolate ice cream.

Baadaye Kidogo unaenda kumuangalia Jabali la Muziki Marijani Rajab au Gurumo na madaktari, bure, courtesy of Prof. Sarungi and crew.

Watu wamekuja mjini baada ya side streets kuwekwa lami halafu leo wanataka kujifanya mji wao?
 
Last edited by a moderator:

Aaaargh kama mpaka pepeta umepiga basi kaka siongezi tena Kiranga!!!!
Kuna mtu hapo kaongelea kulala kibarzani ndo kaonesha ugeni wake dhahir shahir wenyewe nyumba zetu za udongo na miti joto sana mpaka zipoe hiyo saa tano muda wote tulale wapi sasa!!!!????
 
Ndiyo mimi nikamwambia watunge sheria kuwazuia mamwinyi wasilale vibarazani tuone.

Hizo pepeta alikuwapo bibi mpenzi, shamba lake likiwa hapa Tangi Bovu, ukikaa shambani unaliona tangi hili, liko upande wa pili tu wa barabara, lina kutu kichizi.

Basi kabla ya kuvuna mpunga lazima upatiwe pepeta kwanza.

Leo wanakuja Wakavirondo hata Tangi Bovu hawajawahi kuliona, wanataka kusema Dar mji wao.

Nikirudi mimi nikiyeona Sozigwa anachukia imla kutoka kwa mchonga live nisemeje?
 
Acha babu umenikumbusha bibi zangu walale pema waliko!!!!!!!!
Ha ha ha haaaaa umemtaja mzee Sozigwa umenikumbusha mtemi mmoja marehemu Sykes Alli huyu alinunua Land Rover 110 mpyaaaaa by then wanazo serikalini tu akatua airport afuatwe na hiyo mashine then mtundu mmoja pale katoka nayo.........anyways!!!!!!!
Watu wanawasikia watu redioni leo wanataka kufukuza wengine ati wao wamekuwa wenyeji!!!!!!

Mkuu Kiranga hope huyo nani sijui mtoa mada atakuwa kajitafakari sasa na kajua kama Dar ni dambwe tu kama mengine kila uchao channel zinaamka na kufa in a Darwinian fashion!!!!!
 
Mtu anakwambia Dar kwao hata Mzee Amri Abeid hamjui.
 
hahahahahaaa ...unaogopa watachukua ajira yako? tulia waje. mi nimeingia jana na ndo kwanza natafuta kazi..
 
Kuna hoja ya msingi, ingawa najua itapingwa hapa kwa hoja nyepesi. Hakuna sababu ya mtu kuja Dar halafu analala kwenye vibaraza vya maduka kwa kutandika na kujifunika mabox, halafu mtu anasema tutabanana hapa hapa!

attachment.php

wengine wanalala stoo!
 
hahahahahaaa ...unaogopa watachukua ajira yako? tulia waje. mi nimeingia jana na ndo kwanza natafuta kazi..

Marekani ingekataa immigrants isingekuwa hapa ilipo.

Naongea hivyo kama immigrant wa kutoka Dar/ Tanzania, kuishia kuishi Marekani.

Dar needs some new blood.

What we have now is obviously not working.

Nimekuja likizo nimekuta mabanda machafuchafu kibao, rushwa unaanza kuwa initiated tangu unakanyaga chini airport.

Dar ain't what it used to be.

And for that alone, one cannoit claim to protect what one stands for.

Nakumbuka kwenda kona ya Azikiwe na City Dr, bumping into a classmate serendipitously.

Now if I bump into anybody I would most likely bump into a bank robber after retrieving my cash from an ATM.

Now who wants that?\

Could Kipi have had a semblance of a recue on this "City"?

Or will the fate be death by a thousand commitees?
 
Watu milioni 4, population density watu 100,000 kwa eneo la mraba. Kwa stahili hii mji hauwezi kua safi wala kero kuisha. Miundo mbinu haikuandaliwa kwaajili ya ongezeko hilo la watu.
 
Mbona unajishaua hivo kwani Dar ya babaako?
 
Wewe na hiyo Dar yako unalalamika hivyo je wenzetu wa New York ambapo biashara ya kimataifa inafanyikia pale nao wasemeje?
wakuja utawaona tu,, kukaa dar miaka 4-5 wanajiona ndo wenyeji...wenyemji tupo kimyaa na hadi tumehamia pembezoni mwa mji kwa jinsi karaha za mji zilivyotuchosha.
 
Hewaaaaa,.nilikuwa sijaiona hii mada,mwaka juzi nilianzisha mada kama hii mukanitukana kweli,mods nao inaonekana ni wakuja maana waliificha chit chat,kama kununa munune,kuanzia members hadi mods nasema hivi,kama wewe ni wakuja basi RUUUDI KWEENUUU,huyu anasema wapya wasije,mimi nasema wakuja wote muondoke murudi kweenu mutuachie Dar yetu inapumulia mashine jamani.Mutuache tuliozaliwa huku,na wale waliokuja miaka ya tisini,kama wewe umekuja kuanzia 2000 na kuendelea nasema ruudi kweenu,hamna pahala pa kujenga "pasipoti" tena,hadi jangwani imejaa,muruudi kweenu,december mukiendaga kwenu kamji ketu kanapoaga na kurudia "umalaika" wake,wezi wanapungua,matapeli wanapotea,gari za kuzimika kwenye madimbwi ya maji huwa hazionekani,Ubungo na buguruni panapitika bila vikumbo,vikwapa kwenye daladala hamna,matusi mitandaoni yanapungua,maji mabombani hutoka,transifoma za Ubungo hazilipuki kwa kuzidiwa "lodi",yaani kamji ketu kanarudi enzi zilee za "ochestre sambulumaa"!tena mukiendaga huko na haya maredio yenu sijui kilaudiz,mejiki muwe munafungia stoo,tumechoka kusikiliza ujinga,mufunge mutuachie RTD yetu na nyimbo zake za ngapulila na baba jeni.Muende kwenu eeh,mumesikia watoto wazuri eeh,mubaki huko huko,tutawaletea yote ya Dar huko!kama munataka mabomba bila maji tutaleta,umeme wa mgao tutaleta,tutaleta magari mengi ili na barabara zenu ziwe na foleni,mumesikia eh?musijali na mafuriko ya jangwani tutaleta,kifua kikuu,malaria,mishikaki,chips,tutaajiri vijana waje wapike huko,betting tutaleta,wapiga debe wa kuchangamsha miji yenu tutaleta,yaani kila kitu mutaletewa,hata bahari tutajenga muogelee ila mkioga muogelee usawa wa huko huko..no stowaway kuja Dar Please please.,tumeenea,tumetosha,tuacheni tupumuweee,nyie murudi kwenu,na hapa nazungumzia wakuja wote,wabara na wapem..mh huku ngoja niache nisionekane "serikali tatu" bure!muruudi kwenu,tumechoka kufagia vinyesi mabarazani kila asubuhi bhana!
 
Back
Top Bottom