Hewaaaaa,.nilikuwa sijaiona hii mada,mwaka juzi nilianzisha mada kama hii mukanitukana kweli,mods nao inaonekana ni wakuja maana waliificha chit chat,kama kununa munune,kuanzia members hadi mods nasema hivi,kama wewe ni wakuja basi RUUUDI KWEENUUU,huyu anasema wapya wasije,mimi nasema wakuja wote muondoke murudi kweenu mutuachie Dar yetu inapumulia mashine jamani.Mutuache tuliozaliwa huku,na wale waliokuja miaka ya tisini,kama wewe umekuja kuanzia 2000 na kuendelea nasema ruudi kweenu,hamna pahala pa kujenga "pasipoti" tena,hadi jangwani imejaa,muruudi kweenu,december mukiendaga kwenu kamji ketu kanapoaga na kurudia "umalaika" wake,wezi wanapungua,matapeli wanapotea,gari za kuzimika kwenye madimbwi ya maji huwa hazionekani,Ubungo na buguruni panapitika bila vikumbo,vikwapa kwenye daladala hamna,matusi mitandaoni yanapungua,maji mabombani hutoka,transifoma za Ubungo hazilipuki kwa kuzidiwa "lodi",yaani kamji ketu kanarudi enzi zilee za "ochestre sambulumaa"!tena mukiendaga huko na haya maredio yenu sijui kilaudiz,mejiki muwe munafungia stoo,tumechoka kusikiliza ujinga,mufunge mutuachie RTD yetu na nyimbo zake za ngapulila na baba jeni.Muende kwenu eeh,mumesikia watoto wazuri eeh,mubaki huko huko,tutawaletea yote ya Dar huko!kama munataka mabomba bila maji tutaleta,umeme wa mgao tutaleta,tutaleta magari mengi ili na barabara zenu ziwe na foleni,mumesikia eh?musijali na mafuriko ya jangwani tutaleta,kifua kikuu,malaria,mishikaki,chips,tutaajiri vijana waje wapike huko,betting tutaleta,wapiga debe wa kuchangamsha miji yenu tutaleta,yaani kila kitu mutaletewa,hata bahari tutajenga muogelee ila mkioga muogelee usawa wa huko huko..no stowaway kuja Dar Please please.,tumeenea,tumetosha,tuacheni tupumuweee,nyie murudi kwenu,na hapa nazungumzia wakuja wote,wabara na wapem..mh huku ngoja niache nisionekane "serikali tatu" bure!muruudi kwenu,tumechoka kufagia vinyesi mabarazani kila asubuhi bhana!